Ilikuwa lazima BLOCK 89 Ifutwe/isimamishwe

Ilikuwa lazima BLOCK 89 Ifutwe/isimamishwe

Kipi kilianza !? KulikuWa na ulazima gani wa kuleta same program.

Nanusa harufu ya ujinga hapa.
Kulikuwa hakuna ulazima wa kuleta kipindi kama The switch labda walichotakiwa ni kuwaongezea nguvu the block 88.9 hii ndio shida ya kupenda vitu vilivyo tengenezwa.... sioni kipya kwa the switch na kamwe hawawezi kupata wasikilizaji wengi kama walio kuwa nao block 88.9
 
Uko sahihi kwanza walinikera sana mno kuiba jina la kipindi kutoka radio waliyokuwepo mwanzo.
Pale THE SWITCH hamna kitu kabisa.
Nngekuwa mm ndo program manager ambao wangefit kile kipindi n caliber ya watangazaji kama fifi, sam misago,kennedy the remedy,mbaba vc,aaliyah na cate nao sio wabaya kiviiile..
Ubunifu sifuri afu eti wanajicompare na clouds au ea radio.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana nasema Wasafi wamefanya kosa kubwa sana kuuwa kile kipindi cha jioni maana baada ya muda itabidi wakiue hata hicho cha mchana...... walitakiwa kuboresha kile cha jioni
 
Mzee kweli wale wasichana na yule mshikaji walikuwa hawaeleweki walikuwa wanajichanganya sana, pili kuna yule jamaa achana na johnjo alikuwa anawauliza wasanii maswali ya kuwadharau kinoma kwa mfano interview ya ENOCK BELLA aisee jamaa alikuwa anamhoji kwa dharau na kumkejeli.
Anajiita mtu Imara
 
MKUU KUNA MTOTO KANIULIZA ETI ANKO NENO BARAKOA LILIKUWEPO AU NI KISWAHILI KIPYA? 🤔
HUWEZI AMINI TOKA JANA NAITAFUTA NAMBA YA WAZIRI WA ELIMU
Tuwaulize BAKITA
 
Mimi natofautiana na wewe kabisa na sikuona ulazima wa kukifuta kipindi cha block 88.9 kwa sababu kipindi kilikuwa ndio kimepamba moto na ukweli ni kwamba kwa jioni ndicho kipindi kilikuwa cha pili kama sio cha kwanza kusikilizwa ukiacha kipindi cha genge cha E-FM.

Kipindi cha Block 88.9 kilikuwa ni kipindi kizuri na kingepata wadhamini tuu kwakuwa wadhamini kitu cha kwanza wanacho angalia ni wasikilizaji wa kipindi husika kama ni wakutosha au lah....halafu kama swala ni utangazaji mbaya watangazaji wale hawana huo ubaya unaosemwa na wengi bali watangazaji wale ni aina ile ile ya watangazaji tulionao kwenye radio zetu kubwa ....Watangazaji wale walipaswa kupewa muda na walisha improve kabisa ukilinganisha na wakati wana anza.

Shida waliyonayo wamiliki wa media zetu ni shida tuliyonayo watanzania wengi yani hatupendi kuvitengeneza vya kwetu bali tunapenda vilivyo tengenezwa na wengine..... wale watangazaji walipaswa kupewa muda na nafasi na nina hakika wange waprove wrong maana hata hivyo walishafanikiwa kupata mashabiki wengi wakipindi chao......

Shida ilikuwa ni kukosa ubunifu kabisa ndio maana wamekiua hicho kipindi walichofanya uwekezaji mkubwa maana ukwelio ni kwamba The Switch itapata wakati mgumu sana kupata wasikilizaji wengi ukilinganisha na ilivyokuwa block 88.9 maana muda ulikuwa ni mzuri...Shida ya wasafi media ni kukosa ubunifu maana ningekuwa wao nisingevunja hicho kipindi kabisa ilikuwa ni kuwapa assigment makundi yote mawili waweze kuvitofautisha vipindi vyao kabla havijaja hewani..... Wasafi walitakiwa kukaa na watangazaji wote wawape home work ya kuvitofautisha vipindi hivi...... pengine Lil Ommy angeliambiwa yeye ata deal na bongo fleva tuu.

Nakumbuka wakati Mina Ally anaanza kutangaza Amplifaya na Millard ...humu jFzilianzishwa nyuzi nyingi za kumkebehi na kumsema anapiga makelele mara ana sauti mbaya mara Clouds wameharibu kipindi lakini leo hii hizo kelele hazipo.....mimi niliwambia kuwa Mina Ally ni matangazaji mzuri sema anahitaji kupewa muda na nafasi ya kusikilizwa.... Lakini leo hii anapendwa kwa sababu Clouds waliamua kumpa nafasi pamoja na kelele nyingi za mashabiki mitandaoni.

Ukweli ni kwamba Block 88.9 haikupaswa kufutwa kwa sababu zozote zile bali walitakiwa kupewa nafasi....
Ni kweli unachosema, ila pressure ya ushindani imekuwa kubwa na wanataka kuonesha kila kitu wanajua
 
Kuna siku walikua wanamuhoji Innos B aliyeimba Yope, wakati anajibu swali lingine hata hajamaliza vizuri hako kajamaa kakadakia kakamuuliza "eti na wewe unakula nyani" Nilimuona innos B hajapendezwa na maswali ya kushambuliwa namna ile ila akawa mvumilivu tu.
Ethics za utangazaji wanazikiuka sana
 
Mzee kweli wale wasichana na yule mshikaji walikuwa hawaeleweki walikuwa wanajichanganya sana, pili kuna yule jamaa achana na johnjo alikuwa anawauliza wasanii maswali ya kuwadharau kinoma kwa mfano interview ya ENOCK BELLA aisee jamaa alikuwa anamhoji kwa dharau na kumkejeli.
Intavyuu ni sanaa na si wote wanaiweza
 
W
Walikuwa wanaropoka bila research
No research no right to speak, Walishaharibu intavyuu nyingi sana, kipindi kimoja kina kikiwa na Ushirawadu humohumo
 
Kulikuwa hakuna ulazima wa kuleta kipindi kama The switch labda walichotakiwa ni kuwaongezea nguvu the block 88.9 hii ndio shida ya kupenda vitu vilivyo tengenezwa.... sioni kipya kwa the switch na kamwe hawawezi kupata wasikilizaji wengi kama walio kuwa nao block 88.9
Nguvu ipi..?, wasikilizaji walikuwepo lakini wazamini hamna, Lil ommy kaja na team yake, je wote wanhewekwa block 89..?
 
Ni kweli unachosema, ila pressure ya ushindani imekuwa kubwa na wanataka kuonesha kila kitu wanajua

Wanatakiwa kuonesha ubunifu ndio wataweza ushindani sio kukurupuka kufuta vipindi na kuiga vipindi! Lazima Diamond akubali ana hitaji kuwa na vipaji vyake ambavyo atavikuza yeye mwenyewe


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Nguvu ipi..?, wasikilizaji walikuwepo lakini wazamini hamna, Lil ommy kaja na team yake, je wote wanhewekwa block 89..?

Sio kwamba wadhamini wanakuja haraka kiasi hicho kama ambavyo unajaribu kuonesha...lazima ujenge trust kwanza halafu kama ni wadhamini walikuwa nao kama Vodacom,pepsi !

Lazima tukubali kuwa kipindi cha The Switch itakuwa ngumu sana kupata wasikilizaji wengi !


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Cha mchana hawawezi, lengo ni ku beat Planet bongo na xxl

Ndio maana nasema wangeweza kukiboresha sana kipindi cha jioni hata Lil Ommy ange team up na baadhi ya watangazaji wa kipindi cha jioni na wengine wakatafutiwa vipindi vingine ... kulikuwa hakuna ulazima wa kuuwa block 88.9 wakati wanajua fika mchana hawawezi compete na wengine


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Joninijo wamemtema ?au amepelekwa kwenye kipindi kingine?

Jonijo anajua sema basi hajapata sehemu ya kutulia

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧

Wako kimya lakini mimi nilitegemea Lil Ommy ,Jonijo ,Cut na Ray Mshana wange unganishwa na kukipa nguvu kipindi cha block 88.9 halafu hawa wengine wangetafutiwa kipindi kingine


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom