Ili tukubali uongo wa Polepole, CCM, INEC, NIDA jitokezeni hadharani

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
580
Rungu la Polepole limerushwa na kuangukia CCM, NIDA na INEC. Kwamba watatu hawa ndio wapindishaji wa haki na maamuzi ya watanzania kwa viongozi wanaowataka kupitia sanduku la kura.

Baada ya madai haya ya Polepole, mapema tu ukaanza mtifuano na majibizano humu.

Wapo wanaopinga hoja za Polepole kwa kudai kuwa ni muongo, mzushi, mnafiki, anatamaa ya madaraka, kwa nini aseme sasa kwani baadhi ya mambo anayoyasema yalikuwepo kwenye Serikali iliyopita wakati yeye akiwa kiongozi, wapo wanaosema akawatafute au aseme wapi alipo Ben Saa nane na wengine. Mwisho wanasema October 29 twende tukatiiki. Ali mradi kila mmoja anapuyanga kivyake.

Wapo wanaosema, Pole pole asikilizwe, wengine wanasema hakuna haja ya kushiriki uchaguzi.maana kwa mjibu wa Polepole, hata wakienda kupiga kura, hakuna maana kutokana na kuunganishwa kwa mifumo CCM, NIDA na INEC mshindi anajulikana.

Kutokana na hayo, ili tuamini kuwa Polepole ni muongo, Hawa wajitokeze ili tuwasikilize, tutajua nani muongo na nani mkweli. Wakiamua kukaa kimya, ni juu yao. Maana ukimya nalo ni jibu, wenye kuelewa tutakuwa tumeelewa nani mkweli! Watu wataamua cha kufanya kama ni kutiki au No reform no election.
 
...limerushwa na kuangukia ...,
Najaribu kukaa pembeni kidogo na kutafakari. Hivi dhana ya Chama kilichoshinda uchaguzi mkuu ndicho chama kinaongoza ama tawala serikali maana yake nini? Kama chama kinatawala serikali na kuiagiza serikali ifanye hiki ama kile, sasa hao NiDa na IEC wanakiukaji kuunganishwa? si ni maelekezo? Halafu, ameeleza utaratibu ilikuwa kuunganisha kwa nia njema? Hiyo nia njema haijafafanuliwa vizuri nadhani. Nahitaji maelezo ya kina.
 
Mkuu unashangaza, yaani kabisa unategemea NEC na NIDA watoke kuja kukanusha...hiyo mbona iko wazi kabisa, lazima watatoka kuja kujikosha lakini kikubwa tushaujua ukweli...full stop!!!.
 
Rungu la Polepole limerushwa na kuangukia CCM, NIDA na INEC. Kwamba watatu hawa ndio wapindishaji wa haki na maamuzi ya watanzania kwa viongozi wanaowataka kupitia sanduku la kura.

Baada ya madai haya ya Polepole, mapema tu ukaanza mtifuano na majibizano humu.

Wapo wanaopinga hoja za Polepole kwa kudai kuwa ni muongo, mzushi, mnafiki, anatamaa ya madaraka, kwa nini aseme sasa kwani baadhi ya mambo anayoyasema yalikuwepo kwenye Serikali iliyopita wakati yeye akiwa kiongozi, wapo wanaosema akawatafute au aseme wapi alipo Ben Saa nane na wengine. Mwisho wanasema October 29 twende tukatiiki. Ali mradi kila mmoja anapuyanga kivyake.

Wapo wanaosema, Pole pole asikilizwe, wengine wanasema hakuna haja ya kushiriki uchaguzi.maana kwa mjibu wa Polepole, hata wakienda kupiga kura, hakuna maana kutokana na kuunganishwa kwa mifumo CCM, NIDA na INEC mshindi anajulikana.

Kutokana na hayo, ili tuamini kuwa Polepole ni muongo, Hawa wajitokeze ili tuwasikilize, tutajua nani muongo na nani mkweli. Wakiamua kukaa kimya, ni juu yao. Maana ukimya nalo ni jibu, wenye kuelewa tutakuwa tumeelewa nani mkweli! Watu wataamua cha kufanya kama ni kutiki au No reform no election.
HAKUNA MTU WENYE AKILI TIMAMU ANAWEZA KUKAA NA KUJIBU UJINGA WA MPUUZI MMOJA POLEPOLE TUNA MAMBO MENGI YA KUFANYA KWA TAIFA HILIO SIYO KUSIKILIZA NA KUJIBU UJINGA WA MTU ANAYEOTA AWAMU YA JPM
 
Wewe ni nani katika NIDA?
Wewe ni nani katika CCM?
Wewe ni nani katika INEC?

Kama siyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Mkurugenzi wa INEC, Bosi wa NIDA, unajibu kama nani? Ili iweje? Kwa sababu zipi? Kwa faida ya nani?
 
Polepole ambaye alikuwa kiongozi mwandamizi kwenye serikali na Chama amesema uchafu wa NIDA, kuunganisha namba na taarifa za Watanzania kwenye INEC ili kuwapa CCM ushindi katika chaguza za dhulumat

NIDA hawajatoka kukanusha Kwa maana wanakiri kuwa kauli za polepole ni kweli
Kwanini serikali iliwahadaa Watanzania kupata NIDA lakini wakijua Nia Yao ni kujinufaisha kwenye chaguzi

Wananchi wataanza kupuuza hata SENSA wakihofia taarifa zao kutumika isivo sahihi

INEC hiyo tushaikatia tushaikatia tamaa zamani
 
Hata wengine kwenye hiyo CCM hawajui hiyo ishu ya wachache stakeholders only
 
Back
Top Bottom