Uchaguzi 2020 Ili kushinda uchaguzi, upinzani unatakiwa kutumia akili ya ziada

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu sana kwa pande zote mbili, CCM na upinzani, kwa CCM ni uchaguzi wa kufa na kupona, CCM itatumia mbinu zote halali na haramu kuhalalisha ushindi, ikiona inaelekea kushindwa kwa njia halali ya sanduku la kura itatumia mbinu mbadala hata kwa kufuta matokeo kama ilivyofanya Zanzibar 2015.

Mazingira ya sasa chini ya rais Magufuli ni tofauti sana na wakati wa utawala wa Kikwete, kwa sasa upinzani hauwezi kutunishiana misuli na chama tawala, hivyo hauna budi kutumia akili za ziada kumshinda adui.

Baadhi ya akili za ziada ni Upinzani kutoa tofauti zao na kusimamisha mgombea mmoja, kuzitumia jumuia za kimataifa kuilazimisha tume ya uchaguzi kutangaza matokeo halisi, kutumia nguvu ya umma, kutumia teknolojia ya kisasa kukusanya matokeo kutoka vituoni mapema na kwa haraka zaidi, ikiwezekana ku access system ya NEC kama ilivyotokea kwa system ya IEBC Kenya kuwa (hacked) kwenye uchaguzi uliopita.

Mbinu hizi na zingine zisizoonekana wazi (aggressive) zinaweza kusaidia kupata matokeo halisi na mazuri kwa Upinzani, vinginevyo ni ngumu sana kwa Upinzani kushinda uchaguzi kwa kutegemea mbinu za kawaida za kusubiri wakurugenzi na NEC kuwatangaza washindi.
 
Wagombea wote wa urais kupitia upinzani wapigiwe kura za maoni na kumpata mmoja tu. Iwe ni Magufuli vs Mr. X.
 
Hivi upinzani bado wana ndoto ya kushinda uchaguzi? Wakati mwingine tuache kujidanganya.
Chama kikuu cha upinzani 2020-2025 kitakuwa CCM, amini maneno yangu.
Na hakiwezi kurudi kwenye chati hadi kizaliwe upya kwani kimezeeka.

Uchaguzi wa mwaka gani ambao wapinzani wanampango wa kushinda?

Kama ni mwaka huu ,wapinzani wameifanyia nini nchi hii hadi wapewe nchi?
Kwani Ni UCHAGUZI upi Kati ya zilizopita OPPOSITION CANDIDATES wa Ubunge walitangazwa bila NGUVU YA UMA? TULIENI WASENGEMANYOYA NYIE KUDADADEKI
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hivi upinzani bado wana ndoto ya kushinda uchaguzi? Wakati mwingine tuache kujidanganya.
Siyo ndoto ni uhalisia,upinzani kushinda inawezekana kabisa ndiyo maana unaitwa uchaguzi.Hata kama CCM ikishinda kihalali,hatuoni tatizo ila ikiwa upinzani ukishinda kihalali na wasitangazwe kushinda,hapo kutakuwa hapakiliki.
Hebu Tume ya uchaguzi iruhusiwe kuwa Huru kutangaza chaguo la Wananchi bila external pressure. Sherehe za ushindi zifanywe na washindi halali,tunajenga nchi(nyumba) yetu sote tusigombee fito
 
Wagombea wote wa urais kupitia upinzani wapigiwe kura za maoni na kumpata mmoja tu. Iwe ni Magufuli vs Mr. X.
Hapa nina wazo tofauti kidogo wakuu, tuache kujipamba na kupeana moyo Tukumbuke ya kwamba "WAPIGA KURA WAKO KAMA WAJUMBE!!" kuna watu hawabadiliki ndani ya mioyo yao hivyo basi WAPINZANI WAWAZE NA KUWEKA NGUVU KUBWA SANA YA USHIRIKIANO KATIKA NAFASI ZA UDIWANI NA UBUNGE ILI IKIWEZEKANA BUNGE NA SM ZIBADILIKE NDIPO TUWAZE URAIS.
Mbinu KATIKA URAIS WASIMAME WENGI TU ILI SIKU ZA MWISHONI MWA KAMPENI WAAMUE MGOMBEA WA KUPIGIWA KURA.
Hii inasaidia adui kushambuliwa toka kila upande na pia watu wake itabidi wajibu hoja tofauti. AIDHA UPINZANI WANGELIKETI KABLA YA FUKUTO ILI WAFANYE MAKUBALIANO "memorandum of understanding" sio vikao vya ghafla mwisho wa siku watakwama tena.
Siasa ni sayansi... siasa ni hesabu...
 
Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu sana kwa pande zote mbili, CCM na upinzani, kwa CCM ni uchaguzi wa kufa na kupona, CCM itatumia mbinu zote halali na haramu kuhalalisha ushindi, ikiona inaelekea kushindwa kwa njia halali ya sanduku la kura itatumia mbinu mbadala hata kwa kufuta matokeo kama ilivyofanya Zanzibar 2015.

Mazingira ya sasa chini ya rais Magufuli ni tofauti sana na wakati wa utawala wa Kikwete, kwa sasa upinzani hauwezi kutunishiana misuli na chama tawala, hivyo hauna budi kutumia akili za ziada kumshinda adui.

Baadhi ya akili za ziada ni Upinzani kutoa tofauti zao na kusimamisha mgombea mmoja, kuzitumia jumuia za kimataifa kuilazimisha tume ya uchaguzi kutangaza matokeo halisi, kutumia nguvu ya umma, kutumia teknolojia ya kisasa kukusanya matokeo kutoka vituoni mapema na kwa haraka zaidi, ikiwezekana ku access system ya NEC kama ilivyotokea kwa system ya IEBC Kenya kuwa (hacked) kwenye uchaguzi uliopita.

Mbinu hizi na zingine zisizoonekana wazi (aggressive) zinaweza kusaidia kupata matokeo halisi na mazuri kwa Upinzani, vinginevyo ni ngumu sana kwa Upinzani kushinda uchaguzi kwa kutegemea mbinu za kawaida za kusubiri wakurugenzi na NEC kuwatangaza washindi.
Fuatilia uchaguzi za Zanzibar uone ni mwaka gani CCM iliwahi kushinda, pia pambao la Mrema na Mkapa lililosababisha uchaguzi kufutwa na kurudiwa kwa mafungumafugu.
 
Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu sana kwa pande zote mbili, CCM na upinzani, kwa CCM ni uchaguzi wa kufa na kupona, CCM itatumia mbinu zote halali na haramu kuhalalisha ushindi, ikiona inaelekea kushindwa kwa njia halali ya sanduku la kura itatumia mbinu mbadala hata kwa kufuta matokeo kama ilivyofanya Zanzibar 2015.

Mazingira ya sasa chini ya rais Magufuli ni tofauti sana na wakati wa utawala wa Kikwete, kwa sasa upinzani hauwezi kutunishiana misuli na chama tawala, hivyo hauna budi kutumia akili za ziada kumshinda adui.

Baadhi ya akili za ziada ni Upinzani kutoa tofauti zao na kusimamisha mgombea mmoja, kuzitumia jumuia za kimataifa kuilazimisha tume ya uchaguzi kutangaza matokeo halisi, kutumia nguvu ya umma, kutumia teknolojia ya kisasa kukusanya matokeo kutoka vituoni mapema na kwa haraka zaidi, ikiwezekana ku access system ya NEC kama ilivyotokea kwa system ya IEBC Kenya kuwa (hacked) kwenye uchaguzi uliopita.

Mbinu hizi na zingine zisizoonekana wazi (aggressive) zinaweza kusaidia kupata matokeo halisi na mazuri kwa Upinzani, vinginevyo ni ngumu sana kwa Upinzani kushinda uchaguzi kwa kutegemea mbinu za kawaida za kusubiri wakurugenzi na NEC kuwatangaza washindi.
Very good analysis.
 
Ni wakati wa kubadili dira na kuishi kinyume cha mazoea. Ni wakati wa CCM kukabidhi kijiti sasa, inaweza kuonekana ngumu kwa hatua hizi za awali lakini mwishowe itakuwa tu kama kumsukuma mlevi, kamba hukatikia pembamba.
Endelea kuota angalia usijikojolee tu
 
Chama kikuu cha upinzani 2020-2025 kitakuwa CCM, amini maneno yangu.
Na hakiwezi kurudi kwenye chati hadi kizaliwe upya kwani kimezeeka.

Kama ni hivyo mtaonhoza serikali ipi maana bunge lote ni CCM.
 
Back
Top Bottom