Pre GE2025 Vyama vya upinzani Tanzania na siasa za maigizo ya kukipinga chama Tawala

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Angada

JF-Expert Member
May 19, 2024
469
872
Siasa za vyama vingi zilianza mwaka 1992 baada ya IMF na WB kutoa vipaumbele na masharti kwa nchi zitakazotaka kukopeshwa kwa wakati huo, masharti hayo ni pamoja na kuwa na soko huria na kuwa na demokrasia ya vyama vingi

Hapa Tanzania vikaundwa vyama siasa vikiwemo CUF, CHADEMA, UDP, NCCR kwaajiri ya uchaguzi wa mwaka 1995. Kwakuwa vyama vya upinzani viliundwa kwa shinikizo na si mahitaji ya raia ikapelekea waasisi na viongozi wa vyama hivyo kupandikizwa ili ionekane demokrasia ipo nchini
mfano

Mwasisi wa CHADEMA, ndg Edwin Mtei huyu alishakua waziri wa fedha enz za Nyerere CUF ikawa na Maalim Seif ambaye naye alishawahi kuwa waziri kule Zanzibar NCCR kulikuwa na Lytonga Mrema ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani. Kwahiyo wapinzani wa kisiasa walikua ni mamluki kutoka ktk serikali ya ccm

Siasa za maigizo na upinzani wa kutengenezwa ulianza 1992 na hadi leo upo watanzania kama wanategemea CCM kuondolewa na vyama upinzani hilo jambo haliwezi kutokea hadi upinzani wa kweli wa siasa uwepo

Itaendelea...
 
Siasa za maigizo na upinzani wa kutengenezwa ulianza 1992 na hadi leo upo

watanzania kama wanategemea CCM kuondolewa na vyama upinzani hilo jambo haliwezi kutokea hadi upinzani wa kweli wa siasa uwepo
Hizi ni hekaya za vijiweni. Nadhani mleta mada kabalehe hivi karibuni ndiyo akaenda kwenye vijiwe vya kahawa aubsaloon akazisikia.
 
Kwakuwa tokea mwanzo vyama vya siasa vilikuwa ni kuwaridhisha wale watoa mikopo na sio lengo la kushika mamlaka za nchi hali hiyo imeendelea kuwepo hadi sasa
watanzania tukisema nchi ina vyama vya upinzani ni kujidanganya
vyama vya siasa vilivyopo bado vina kasumba zile zile za kuigiza na kuonyesha demokrasia ipo nchini
Wananchi wengi wameichoka CCM na wanataka mabadiliko ktk serikali tatizo linakuja katika njia gani ya kukitoa chama tawala madarakani
Kwa kutegemea vyama vya upinzani jambo hilo halitawezekana kwa vyama vilivyopo sasa
 
Hizi ni hekaya za vijiweni. Nadhani mleta mada kabalehe hivi karibuni ndiyo akaenda kwenye vijiwe vya kahawa aubsaloon akazisikia.

Kama ni stor za vijiweni je ni kweli au ni uongo
na kama uongo weka wewe hapa ukweli unao ujua
 
CCM itang"oka Madarakani siku kukiwa na Mgombea huru asiyekuwa na chama chochote!

1. Mgombea binfsi/huru ni jambo la muhimu kama tunataka demokrasia ya kweli
nakumbuka mchungaji Mtikila alipambania sana jambo hilo kule mahakamani pekee yake na hakuna chama ambacho kilimpa ushirikiano au msaada wowote
2. Tume huru ya uchaguzi inapaswa iwe huru sio hii iliyopo sasa
 
Hizi ni hekaya za vijiweni. Nadhani mleta mada kabalehe hivi karibuni ndiyo akaenda kwenye vijiwe vya kahawa aubsaloon akazisikia.
Hao ni UVCCM wamemwagwa Kila Kona kuanzia kule x,lengo ni kuja ni hizi pigo zao zakiwaki
 
Siasa za vyama vingi zilianza mwaka 1992 baada ya IMF na WB kutoa vipaumbele na masharti kwa nchi zitakazotaka kukopeshwa kwa wakati huo, masharti hayo ni pamoja na kuwa na soko huria na kuwa na demokrasia ya vyama vingi
Hapa Tanzania vikaundwa vyama siasa vikiwemo CUF, CHADEMA, UDP, NCCR kwaajiri ya uchaguzi wa mwaka 1995
Kwakuwa vyama vya upinzani viliundwa kwa shinikizo na si mahitaji ya raia ikapelekea waasisi na viongozi wa vyama hivyo kuna vyama upinzani hilo jambo haliwezi kutokea hadi upinzani wa kweli wa siasa uwepo

itaendelea...
Huo upinzani wa kweli wa siasa utaanza lini? Au hadi hao IMF waje tena kuuanzisha?
 
Inaendelea...

vyama vya upinzani kama kweli wapo kwaajiri ya kuchukua madaraka ya serikali wangezingatia yafuatayo
1. Kudai tume huru ya uchaguzi

wapinzani wangedai kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi kwa kupeleka madai yao mahakamani na kuelimisha raia umuhimu wa tume huru, lakini kwakuwa wapinzani wengi ni mamluki hawawezi kudai tume huru

2. Mgombea binafsi, uhuru wa mtu binafsi unazuiwa kwa sababu mgombea binafsi anaweza kuwa tishio kwa chama tawala, mgombea binafsi anakuwa hana mtu wa kumnyamazisha kama inavyofanyika ndani ya vyama vya siasa

3. Kubadilisha sheria zote znazompa madaraka rais kuteua wakuu wa vyombo vya usalama na taasisi mbalimbali, rais anatakiwa ateue muhusika baada ya majina matatu kupendekezwa na bunge au kamati maalum

4. Katiba mpya wapinzani wanatakiwa kudai katiba mpya ambayo italeta mabadiliko kadhaa ktk sheria

5. Vyama vya upinzani waungane na kuunda chama kimoja chenye nguvu

6. Kushirikisha vijana ktk harakati za mabadiliko ya kisiasa na kuwaelezea umuhimu wa hayo mabadiliko
 
1. Mgombea binfsi/huru ni jambo la muhimu kama tunataka demokrasia ya kweli
nakumbuka mchungaji Mtikila alipambania sana jambo hilo kule mahakamani pekee yake na hakuna chama ambacho kilimpa ushirikiano au msaada wowote
2. Tume huru ya uchaguzi inapaswa iwe huru sio hii iliyopo sasa
Mkuu ww ulienda mahakamani kumuunga mkono Mtikila, au ww ni mchambuzi tu usiyekuwa na mbinu yoyote?
 
Siasa za vyama vingi zilianza mwaka 1992 baada ya IMF na WB kutoa vipaumbele na masharti kwa nchi zitakazotaka ondolewa na vyama upinzani hilo jambo haliwezi kutokea hadi upinzani wa kweli wa siasa uwepo

itaendelea...
Dogo uchambuzi wako ni dhaifu huenda ulikuwa hujazaliwa umesimuliwa au umesoma kwenye vitabu
Sisi baba zako tuliokuwepo na tumeshiriki mageuzi

Tuchukulie ni kweli usemacho,, tuitishe kura ya maon (referundum) sasa hivi tuwaulize raia wangali wanataka chama kimoja au vyama vingi tutapata majibu sahihi
 
Huo upinzani wa kweli wa siasa utaanza lini? Au hadi hao IMF waje tena kuuanzisha?

Upinzani wa kweli unatokea endapo
1. Mabadiliko ya uongozi yatatokea ndani ya vyama vya upinzani na kuwa na misimamo ya kweli ya kutaka kuchukua mamlaka ya serikali, sio hawa waliopo sasa
2. Kuunganisha vyama vya upinzani na kuwa na chama kimoja chenye nguvu. Kwa sasa wapinzani wanatumika kugawa kura za upinzani kwa kila chama
 
Dogo uchambuzi wako ni dhaifu huenda ulikuwa hujazaliwa umesimuliwa au umesoma kwenye vitabu
Sisi baba zako tuliokuwepo na tumeshiriki mageuzi

Tuchukulie ni kweli usemacho,, tuitishe kura ya maon (referundum) sasa hivi tuwaulize raia wangali wanataka chama kimoja au vyama vingi tutapata majibu sahihi

ni kosoe kwa hoja sio kutoa kashfa

Itungwe sheria kwamba kupiga kura iwe lazma kisheria uone itakavyokuwa, maana wapiga kura wengi wa sasa wananunuliwa na ccm kwa sababu ya njaa zao, wengi wenye akili na kujua maigizo yaliyopo nchini uwez ukamwona anaenda kupiga kura, na wale wanaochagua upinzani japo ni wachache lakini wamejitolea kindakindaki kutaka mabadiliko
 
Ok Ni conclude,
tunaopenda au kuvihitanji vyama vingi tuko wengi nkama huamini unaweza nipinga kwa tafiti kijana
 
Back
Top Bottom