Ili kumaliza migogoro inayoendelea Congo, inabidi malalamiko yote ya waasi yasikilizwe

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,028
12,353
Nachopendekeza katika migogoro inayo endelea Congo DR ni kuwa malalamiko yote ya makundi ya waasi yasikilizwe.

Yale malalamiko yanayoweza kutatuliwa yatatuliwe yale yenye ugumu yaingiwe makubaliano ya pande mbili kufikia upatikanaji wa amani.

Lazima malalamiko ya waasi wajulishwe Wacongo na waafrika wote na ionekane je, wanachopigania kina maana au upuuzi tu?

Tusiwafunge midomo kabisa waasi na kuona hawana wanacho lalamikia hapo tutakuwa hatutatuwi matatizo kabisa zaidi ya kujidanganya.

Nchi zetu zinazotuma ndugu zetu( raia wenzetu) kwenda kupigana Congo lazima wananchi tujue majeshi yetu yanaenda kupigana na nani na hao wanaoenda kupigana nao wana malalamiko gani na majeshi yetu yapo sahihi kutumia mbinu za mapigano kutatua malalamiko ya hao wanao pigana nao (waasi) au laaah !

Narudia tena tusiwafunge midomo kabisa waasi na kuwapa majina mabaya pasipo kujua nini wanacho dai na kupigania.

Lazima tujurishwe nini wanadai katika mapigano yao.
 
Malalamiko ya waasi ni yepi hayo,
Sometimes hawa kenge wafyekwe tu waishe, hakuna justification ya kuua raia vile, wapelekewe moto
Ndio hayo malalamiko yao tuambiwe.

Mpaka sasa mbinu ya vita haijaleta haueni yoyote ile Congo na ni miaka mingi inatumika lakini hakuna kitu.

Vile vikao wanavyo kaa na waasi inabidi tujurishwe nini waasi wanataka na hapo ndipo tuangalie njia ya kutatua hayo matatizo
 
Waasi wanataka kujitawala mashariki, wanataka migodi ya madini,

Utaweza wapa hivyo,
 
Siasa ni ujinga mkubwa watue wanakufa kwa ufala wa watu wachache...Hii vita hapajatwa mlengo wa dini ila unajulikana hao jamaa ni dini gani.

Ingetokea somalia basi ingekuwa mzozo wa dini .

Tuacheni ujinga amani ni bora ona watu wanakufa ksa ujinga wa watu wachache.
 
M23 ni dini gani?
 
Nachopendekeza katika migogoro inayo endelea Congo DR ni kuwa malalamiko yote ya makundi ya waasi yasikilizwe.

Yale malalamiko yanayoweza kutatuliwa yatatuliwe yale yenye ugumu yaingiwe makubaliano ya pande mbili kufikia upatikanaji wa amani.

Lazima malalamiko ya waasi wajulishwe Wacongo na waafrika wote na uonekane je, wanachopigania kina maana au upuuzi tu?

Tusiwafunge midomo kabisa waasi na kuona hawana wancho lalamikia hapo tutakuwa hatutatuwi matatizo kabisa zaidi ya kujidanganya.

Nchi zetu zinazo tuma ndugu zetu( raia wenzetu) kwenda kupigana Congo lazima wananchi tujue majeshi yetu yanaenda kupigana na nani na hao wanaoenda kupigana nao wana malalamiko gani na majeshi yetu yapo sahihi kutumia mbinu za mapigano kutatua malalamiko ya hao wanao pigana nao (waasi) au laaah !

Narudia tena tusiwafunge midomo kabisa waasi na kuwapa majina mabaya pasipo kujua nini wanacho dai na kupigania.

Lazima tujurishwe nini wanadai katika mapigano yao.
Wale ni Tutsi wanataka hicho kipande chenye madini kiwe huru ili wakiunganishe na Rwanda ili watengeneze bahema impire mzee. Hao hakuna majibu zaid ya kuwaswaga.
 
Nachopendekeza katika migogoro inayo endelea Congo DR ni kuwa malalamiko yote ya makundi ya waasi yasikilizwe.

Yale malalamiko yanayoweza kutatuliwa yatatuliwe yale yenye ugumu yaingiwe makubaliano ya pande mbili kufikia upatikanaji wa amani.

Lazima malalamiko ya waasi wajulishwe Wacongo na waafrika wote na uonekane je, wanachopigania kina maana au upuuzi tu?

Tusiwafunge midomo kabisa waasi na kuona hawana wancho lalamikia hapo tutakuwa hatutatuwi matatizo kabisa zaidi ya kujidanganya.

Nchi zetu zinazo tuma ndugu zetu( raia wenzetu) kwenda kupigana Congo lazima wananchi tujue majeshi yetu yanaenda kupigana na nani na hao wanaoenda kupigana nao wana malalamiko gani na majeshi yetu yapo sahihi kutumia mbinu za mapigano kutatua malalamiko ya hao wanao pigana nao (waasi) au laaah !

Narudia tena tusiwafunge midomo kabisa waasi na kuwapa majina mabaya pasipo kujua nini wanacho dai na kupigania.

Lazima tujurishwe nini wanadai katika mapigano yao.
Hujaamua tu kujua ila Madai yao yanajulikana mbona
 
Ni wazo zuri. Bahati mbaya,si rahisi kuwezekana kwa sababu ya badhi ya mambo:

-Yapo makundi yanayopigania haki yao(M23). Hili ni kundi lenye historia ndefu kabla ya ukoloni. Lakini,ukiangalia, chanzo cha hili tatizo ni 1994, baada ya mauaji ya kimbali Rwanda. Wahutu,waliojawa na chuki,mpaka wa leo wapo huko,na M23 ni jamii ya watutsi. Hivyo,FDLR,ambayo ndo chanzo cha mgogoro,dhamila ya kuua watutsi Congo,iliwafanya wajitetee na wao.

-RED Tabara: Hili ni kundi la warundi,baada ya jaribio la kumpindua raisi Nkurunziza, limejitenga na kuanzisha mapigano wazi. Hili ni la kuongea na serikali ya Burundi,ikiwa serikali haitaki,watafanyaje!
-Lipo kundi la waasi wa serikali ya Uganda. La mda mrefu sana. Hilo,ni Waganda wapo DRC.

Kuna makundi mengine sasa,ya wa Congo wenyewe. Hawa,ma Boss wao huwa matajiri na wanajeshi wenye vyeo vikubwa. Huishi kwa kazi za machimbo. Watu wanapoingiliana anga zao,ndo hutokea vita kati ya makundi hayo.
Haya,yamekuwepo toka enzi,na si rahisi kuisha.

Nimalizie tu kwa kusema kwamba,inaonekana kama kuna mkono wa mzungu furani,anaependa watu wauwane,apate anachokitaka yeye. Na hapo, hutumia watu wengine ili yeye asionekane kahusika.
Lakini,yaliyotokea Libya, Afghanistan,Syria na kwingineko,ndo hayo hayo yanayotokea DRC.
Wa Afrika sisi wenyewe,kama vile akili hatuna.
Siku za nyuma,umemsikia mkuu wa African Union akibaliki Nigeria kuovamia Niger!! Kama kiongozi,mwenye akili za hivyo,ni wazi nae hupenda vurugu. Je,raia wengine unadhani itakuwaje?!
Wenye nguvu hawawezi kukubali vita viishe,maana ndo wao wanapopata soko la siraha zao.
 
Hakuna malalamiko ya waasi, ni vikundi vya wahuni wanaofadhiliwa na nchi jirani nchi za nje ya bara, makampuni makubwa kuleta fujo na kuondoa utawala wa sheria ila wakwapue madini, its never too late to wipe these MFs
But it's not that easy bro.
-Kama wenye pesa aanawatumia raia wa kawaida kufanikisha mambo yao,unategemea watakubali kumaliza biashara hivi hivi?

-Wazungu wangapi wanaomiliki makampuni ya kuchimba?! Unadhani wapo tayari kupoteza? Wanaiba! Wanashilikiana na viongozi,unategemea nani akibali biashara yake ilale?

UN,wanaojiita walinda amani,uliwahi sikia raia walivyowateka,vifaru vikapinduliwa,yakakutwa mawe kwenye mifuko?

Kwanza UN yenyewe ndo US. US hawatakii watu mafanikio,hasa pale anapopata chochote. Unategemea kitatokea nini!
 
Back
Top Bottom