Ilani ya CHADEMA 2010-2015

Ilani ya CHADEMA 2010-2015

Source: Sera ya Vijana ya CHADEMA

Sera ya Vijana
Masikini Vijana wa Tanzania, kwa nini lakini?

  1. Vijana, wasichana na wavulana ni sehemu kubwa ya Taifa – zaidi ya nusu ya Watanzania wote.
  2. Vijana bado wanaonekana ni Taifa la kesho.
  3. Vijana wanatumiwa kama washabiki katika siasa - ushiriki wao katika uongozi ni finyu.
  4. Ukosefu wa ajira kwa vijana unazidi kuongezeka – Hasa vijana wa kike hawana ajira na kujikuta wanajiingiza katika vitendo vya biashara ya ngono.
  5. Vijana wenye vipaji wametelekezwa – vipaji vya vijana haviendelezwi.
  6. Vijana wengi ni hohehahe – vijana wako duni zaidi kiuchumi.
  7. Vijana wanabugudhiwa – wanakamatwa kwa uzururaji, wafanyabiashara ndogondogo wanatimuliwa!
  8. Vijana wanateketea kwa UKIMWI na madawa ya kulevya.
  9. Michezo imepuuzwa na vijana hawana cha kufanya hivo kujiingiza katika uhalifu.


Serikali ya CHADEMA na sura mpya ya Vijana wa Tanzania
  1. Tunaamini kwa vitendo kuwa kijana ni Taifa la Leo.
  2. Tutatoa fursa na kuwezesha kizazi kipya kuwa mstari wa mbele katika siasa, uchumi na sekta nyingine.
  3. Tutaweka mazingira ya kuundwa kwa Baraza Huru la Vijana Tanzania.
  4. Tutawezesha vijana wa kike na wa kiume kumiliki ardhi na rasilimali nyingine kwa kutenga maeneo kadhaa ya biashara kwa vijana tu.
  5. Tutaweka kipaumbele katika kukuza ajira kwa vijana kupitia vipaji vyao katika nyanja mbalimbali – tutazielekeza halmashauri kuanzisha mifuko ya ukuzaji vipaji vya Vijana.
  6. Tutaweka mazingira ya kuboreshwa kwa malezi ya Vijana katika familia na mashuleni ili kukabiliana na UKIMWI na madawa ya kulevya.
  7. Tutatoa leseni za bure na likizo ya kodi kwa Vijana wafanyabiashara ndogondogo na Vijana wanayojishughulisha na uzalishaji mali.
  8. Muziki wa kizazi kipya utapewa kipaumbele ili soko la muziki huu litakuzwa nje ya Tanzania.
 
Source: Sera ya Viwanda ya CHADEMA

Sera ya Viwanda
Hali mbaya sana, kwa nini?

  1. Viwanda vimeuwawa kufuatia utawala mbovu.
  2. Vichache vilivyobaki vimemilikishwa na wageni.
  3. Hakuna sera dhabiti ya maendeleo ya viwanda.
  4. Hakuna sera ya kulinda viwanda vya ndani.
  5. Viwanda vidogovidogo huko Vijijini havijalwi.


Serikali ya CHADEMA itatatua tatizo la Viwanda kwa kufanya yafuatayo
  1. Tutatoa kipaumbele kwenye viwanda vya bidhaa za kilimo.
  2. Tutaimarisha SIDO kuwawezesha wananchi kuanzisha viwanda vidogovidogo vya usindikaji katika maeneo ya vijijini.
  3. Tutaimarisha VETA kutao mafunzo ya ufundi kwa vijana wetu wa kike na wa kiume.
  4. Tutalinda viwanda vya ndani mpaka vikue ili viweze kushindana.
  5. Tutatunga sera dhabiti za maendeleo ya viwanda na hasa viwanda vidogovidogo vya wananchi.
 
Yale yale....... this is just another wishful thinking. Eg Itawezesha vijiji kutunza vyanzo vya maji, tutahakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama katika kipindi kifupi etc. How this wishes could be made practical? Mtafanya nini kivitendo?

Unataka mlolongo wote wa jinsi ya kufanya practically wauandike kwenye ilani ya uchaguzi, kweli? Hiyo ilani si itakuwa kam bible kama unataka waweke na michoro kabisa. Ilani ni outline, utekelezaji wake ni another document na huwezi kukuta kwenye ilani. And right, ilani ni wishful thinking, kwamba tunakusudia kufanya hivi na vile etc. Hata ccm wanasema watajenga uwanja wa kimataifa Kigoma, sasa ulitaka wasema kuwa hata KLM, Emirates wamekubali kutua kigoma? Unless mimi sielewi mana ya international airport, ina maana KLM, KQ etc zitakuwa zinatua Kigoma, na kutakuwa na custom clearence etc,lol
 
Sera za Chadema ni nzuri sana kama zilivyo za wanasiasa wengineo, tatizo bado lipo palepale, sera hizo hazinipi mimi mwananchi assurance ya kutekelezeka, Chadema nao bado hawajaonesha kuwa THERE IS A REAL WORLD ambamo juhudi za kutekeleza sera hufanywa. Na kama walivyo wanasiasa wengi wa nchi maskini, FORCES ZINAZOTAWALA DUNIA ndiyo zimewafikisha katika mapungufu hayo yaliyoelezwa na SUPERMAN. All politicians are the same the only difference is in crafting nice words, they are really good on that. No politician preaches bad policies, only reality drags them differently. Probably the form of politics the colonial powers left us with needs re-engineering.

Anyway SUPERMAN KEEP TALKING !!
 
But I think Chadema policies are realisable and there is a clear way you can see them realised and easily measurable. It is not about counting how many holes of the it latrines were done in the last 33years of the ruling regime. We can only use policies to choose who is good and we will measure them on the metrics they have put in place and agreed in advance during campaigns. We can do much than what we are currently doing.
 
Unataka mlolongo wote wa jinsi ya kufanya practically wauandike kwenye ilani ya uchaguzi, kweli? Hiyo ilani si itakuwa kam bible kama unataka waweke na michoro kabisa. Ilani ni outline, utekelezaji wake ni another document na huwezi kukuta kwenye ilani. And right, ilani ni wishful thinking, kwamba tunakusudia kufanya hivi na vile etc. Hata ccm wanasema watajenga uwanja wa kimataifa Kigoma, sasa ulitaka wasema kuwa hata KLM, Emirates wamekubali kutua kigoma? Unless mimi sielewi mana ya international airport, ina maana KLM, KQ etc zitakuwa zinatua Kigoma, na kutakuwa na custom clearence etc,lol

Ya CCM yenyewe haina jinsi ya kutekeleza lakini it is already 141 A4 pages. Just imagine, how is normal person going to read through without being lost in the bush?
 
Kijana heri ungechagua sera ingine iyo ya maji kivitendo mbona ndo the simplest.
Unajua kwa east africa twaongoza kwa kuwa na mito na lakes.
Mfano DSM Temeke kuna maji safi hasa ya visima then chimba visima vingi ili uweze lisha watu wa Kimara,Tabata ambao hawana maji au wanayo ila ya Chumvi.Au ondoa supply ya maji ya Ruvu Temeke ili watu wasio na maji wapewe hayo ya Ruvu kama sinza,ubungo.
Kyela ina mito zaidi ya minne ila kuna maeneo mpaka leo hawana maji safi unaitaji nini apo kama sio utashi wa viongozi ambao wako serious na matatizo ya watu wao
 
Aise. Hii ilani ni nzuri mno. Tatizo watanzania wengi hawasomi. Unless waichapishe kwenye magazeti ya udaku.
 
Bravo, ilani ime imekaa vyema. The ball is on our side, tuwape uwanja wazitekleze.. how? hamasiha ndugu jamaa na marafiki, kufanya maamzi sahihi ya kuipigia kura CHADEMA October
 
Takribani wiki kadhaa kuna member aliandika post ya kusifia ilani ya CHADEMA. Kiuhalisia wengi hatuna kawaida ya kupitia yaliyoandikwa na hawa wanasiasa. Nimeanza kuingalia CHADEMA baadae tutaangalia ya vyama vingine pia.
Mf wa kurasa chache za mwanzo ni huu.

"Tumekuwa na miaka takribani 50 ya CCM. Wameahidi kila aina ya ahadi na wamefanya kila makosa, lakini tukawavumilia na tukawapa nafasi nyingine tukiamini kwamba mambo yatabadilika. Kila tulipowapa nafasi, hali ilizidi kuwa mbaya, tukasogea kutoka kubaya kwenda kubaya zaidi". (ukr 6-7).

Je ni kweli kuwa CCM imetawala miaka 50 kama ilani hii inavyotaka kutueleza.Lakini pia huku ilani hiyo ikiwa imesheheni quotations mbalimbali za mwl Nyerere na kumuona km mtu mwenye kupigiwa mfano kwao, bado ilani hiyo inajichanganya kwa kusahau kuwa kati ya takribani miaka 50 ya uhuru nusu ya miaka hiyo Mwl Nyerere ndiyo alikuwa kiongozi wa nchi.

"Pili, Watanzania tutambue kwamba tukiamua kwa dhati na kuchukua hatua katika uchaguzi huu wa 2010 tunaweza kabisa na kwa hakika tuna uwezo wa kubadili hali tuliyo nayo kutoka taifa linaloendelea taratibu na kuwa taifa linaloendelea kwa kasi" (Ukr 10)

Katika Dibaji ilani inaeleza kuwa idadi ya Watanzania kuwa masikini wameongezeka hadi kufikia mil 13 (hapa mtu anaweza kuhoji chanzo cha takwimu ingawa si malengo yangu). Lakini ukisoma ukr 10 wanasema wanataka kuifanya Tanzania liwe Taifa linaloendelea kwa haraka badala ya kuendelea taratibu. Kwahiyo utaona kunakujichanganya hapa.Pia ukurasa huo wa 10 wanaendelea kusema kuwa Watanzania wanaendelea kuwa masikini wa kutupwa????

Pia ilani ya CHADEMA inajikita kwenye misingi ya UZALENDO, MAADILI NA UADILIFU.

Hapa naweka mtazamo wangu kuwa uwepo wa uadilifu ndiyo unatengeneza maadili. Palikuwa hamna haja ya kurudiarudia.
 
"Serikali ya CHADEMA itaweka utaratibu ili kuhakikisha kuwa wanafunzi ambao wanajikuta wanalazimika kukatisha masomo kwa sababu ya ujauzito wanaruhusiwa kuendelea na masomo mara baada ya kujifungua bila kulazimika kuhama maeneo yao kwa sababu ya unyanyapaa. Tanzania imepoteza mabinti wengi ambao wangeweza kutoa mchango kwa taifa kwa sababu ya kupata ujauzito. Pamoja na hilo, Serikali ya CHADEMA itahakikisha kuwa wale wote wanaowapatia wanafunzi mimba wanawajibishwa kisheria pamoja na kulazimishwa kulipia gharama yote ya kukatisha masomo na malezi ya mtoto hadi afikapo miaka 18. Na wale ambao wanafanya vitendo hivyo kwa mabinti wa chini ya miaka 18 watashtakiwa kwa mujibu wa sheria"( Ukr 15-16).

Kabla ya hii paragraph CHADEMA wameeleza kwa ufasaha kabisa tatizo la mimba kwa watoto wa shule. Hii paragraph ndio ikaja na suluhisho eti CHADEMA wataweka utaratibu. Hii haitoshi kwa ilani. Utaratibu upi unaozungumziwa hapa. Kwanini hawakuainisha basi. Ukiendelea mbele wanazungumzia kuwa wataendelea wanafunzi hao kusoma maeneo hayo bila kulazimika kuhama kwa sababu ya unyanyapaa. Ahh! Unazuia vipi unyanyapaa??? Pia wao wanalizungumza tatizo kuanzia kwenye ujauzito wanasahau kulizungumzia kwenye preventive aspects.
 
Kuna post no 2 nilioverlook. Wametoa solution ya ujauzito kama ifuatavyo.
 
Kuingiza katika mitaala elimu ya uzazi na mahusiano kuwiana na umri wa wanafunzi. Ufundishwaji wa somo hili litawapatia vijana wa kike stadi za kuweza kujikinga na tatizo la kuanza ngono katika umri mdogo. Nchi nyingi zilizofanikiwa kupunguza au kumaliza tatizo la mimba utotoni ni zile zinazozingatia utolewaji wa elimu ya uzazi na mahusiano mashuleni. Elimu hii itazingatia uelewa wa kisayansi kuhusu maisha ya watu, lakini vile vile utazingatia umuhimu wa kulinda familia na maamuzi ya wazazi juu ya watoto wao kwa kuhakikisha elimu inayotolewa ni ile yenye kuzingatia heshima, kujiamini na kujilinda katika mahusiano ya kijinsia. pg 20
 
Katika ukurasa wa 20 ilani inasema hivi
"Tutazihuisha na kuanzisha shule mpya za kitaifa za bweni za sekondari. Shule hizi zitachukua wanafunzi wote waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya mwisho darasa la saba. Katika kila mkoa kutakuwa na angalau shule moja ya kitaifa itakayochukua wanafunzi kutoka katika mikoa mingine kwa lengo la kujenga utaifa na uzalendo miongoni mwa wanafunzi, na CHADEMA itarejesha utaratibu wa usafiri wa "Warrant" kwa wanafunzi hao ili kuondoa makali ya gharama za nauli kwa wazazi. Ni wazi kuwa utaratibu huu ni ghali, lakini kuua utaifa ni ghali zaidi!"

Utaona kuwa wale watakaopata alama nzuri watatengwa peke yao ili kujenga Utaifa ila wale wasiofanya vizuri watabaki kwenye shule hizo nyingine. Na haipingiki kuwa mwisho wa siku hawa ndiyo watakaofanya vizuri. Basi ilani inaendelea kusema hivi kuhusu elimu ya juu:
 
"Kulipiwa gharama kamili ya masomo ya Chuo Kikuu (Full Scholarship). Serikali ya CHADEMA itaanzisha mfuko wa elimu uitwao "Uhuru Scholarship Fund". Hii ni programu ambayo Serikali ya CHADEMA itaanzisha ili kumlipia (grant) kijana yeyote wa Tanzania ambaye amesoma nchini kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita na amepata alama za daraja la kwanza au la pili asilimia 100 ya ada na malipo mengine ya lazima kwenye Chuo Kikuu chochote cha umma cha Tanzania" ukr . 21.
Kwahiyo hao watoto watakaofanya vizuri very likely watapata fund za kuendelea na elimu ya juu ila hawa wengine wanaambiwa katika ukurasa huo watawekewea UTARATIBU kutoka katika halmashauri na blah blah nyingine.
 
Mpinzani yeyote anayemuona Nyerere hero wa kupigiwa mfano ana upinzani superficial na haelewi maana ya demokrasia halisi.

Haya maswala ya kutaka kulipia watu bila kuangalia need hata huyo Nyerere wao aliyaponda kwenye hotuba yake ya Mei Mosi 1995 Mbeya.
 
Kwa ujumla sura ya pili ya ilani hiyo inazungumzia elimu na imejitahidi kuahinisha hali ya sasa na nini watakachokifanya baadae. Licha ya kuwa wao wanasema ilani si ahadi bali ni mpango kazi. Kwa ujumla vitu vingi havionyeshi time frame. Maana km ni mpango kazi, muda wa utekelezaji ulitegemewa uonekane.
Lakini pia pamoja kuonyesha nia ya kufanya mabadiliko katika elimu hiyo kutoka kwa ile voda fasta, ilani haijazungumza kabisa hawa walimu wa voda fasta itawafanya nini maana wao ndio wanaotoa elimu yetu sasa hivi. Haijaonyesha mkakati wowote wa kuwaendeleza kielimu na wala hatma yao.
 
Back
Top Bottom