Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,695
- 1,696
Hali katika sekta ya ardhi ikoje?
Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kumilikisha Ardhi kwa Watanzania?
- Watanzania wote ni wapangaji katika ardhi yao sheria za ardhi hazitoi mamlaka ya kumiliki ardhi kama mtu binafsi ama vikundi.
- Sheria hizi zinampa mgeni mamlaka makubwa juu ya ardhi kuliko mwananchi.
- Mfumo dume umetawala katika kumiliki ardhi wanawake na vijana hawajapata fursa ya kumiliki au kukodisha ardhi.
- Wageni wanauziwa ardhi kama khanga.
- Mfumo mbaya wa ugawaji na umiliki wa ardhi pamoja na rushwa imesababisha utitiri wa migogoro ya ardhi.
- Wananchi wanaporwa ardhi zao kwa visingizio vya kuendeleza maslahi ya Taifa.
- Utaratibu uliyopo wa milki ya ardhi hautoi uhakika kwa wanyonge na maskini kumiliki ardhi yao.
- Kuna urasimu mkubwa unaoshawishi rushwa katika kutoa haki za kumiliki ardhi.
Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kumilikisha Ardhi kwa Watanzania?
- Tutarejesha mamlaka ya asili ya wananchi kumiliki ardhi.
- Hatima ya ardhi ya kijiji itaachwa mikononi wa mamlaka ya Serikali ya kijiji.
- Rais hatokuwa na mamlaka ya kuhamisha ardhi kutoka kundi moja hadi jingine.
- Wageni watapatiwa ardhi kwa masharti yafuatayo - kutoimiliki, kutoiuza, kutoipora rasilimali na kutoitumia kwa namna itakayoharibu mazingira.
- Umilikaji wa ardhi kwa wanawake haitakuwa suala la mjadala tena. Mfumo dume wa kumiliki ardhi utatokomezwa na kufanywa historia.
- Utawekwa utaratibu wa kisheria utakaowawezesha wanawake kumiliki ardhi bila bughudha wala hofu ya kuporwa.
- Itaimarisha mabaraza ya ardhi ya vijiji na wilaya na kuhakikisha yanatoa haki kwa wananchi.
- Utawekwa utaratibu wa serikali kuwawekea mawakili wananchi wasio na uwezo katika mashauri ya ardhi katika ngazi ya mahakama kuu na mahakama ya rufaa.
- Tutatunga na kusimamia sheria zitakazo shughulikia uvamizi na ujenzi holela.
- Itatoa maelekezo kwa halmashauri kuendesha mipango ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu za wananchi.
- Itarejesha nyumba zote za serikali zilizouzwa kwa upendeleo.
- Tutaunda baraza la Taifa la ardhi litakalowajibika kwa Bunge.
- Mahitaji ya ardhi kwa jamii za vijijini yatapewa kipaumbele kuliko mahitaji ya wengine.
- Tutalinda ardhi za vijiji dhini ya umegaji mkubwa ili kuepuka matatizo ya kijamii.
- Itahakikisha vijiji vinakuwa ni vitengo vinavyojiendesha na kujitawala vyenyewe na tutawezesha wanavijiji kushiriki kikamilifu kuendesha masuala yote ya ardhi kupitia vikao vya mkutano mkuu wa kijiji.
- Tutahakikisha wanyonge na maskini wanamiliki ardhi ya nchi yao bila ubaguzi wa jinsi wala umri.
- Madaraka ya kutoa haki za kumiliki ardhi yatakuwa chini ya mikoa (majimbo).