Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,095
- 43,307
...kama watu watapigia kura Ilani..
Mwanakijiji unaenda mbali saana kwa kuwaza Ilani.Huwa sishtuliwi na mambo mengi ya kisiasa; lakini kama nilichokiona kwa macho yangu ndicho kitakachokuwepo kwenye Ilani ya Chadema basi naweza kusema tu kuwa ni ya "kuthubutu, inatisha na inawaweka CCM pabaya". Kama ndiyo hiyo, basi itabidi CCM warudi darasani kuandika Ilani yao upya maana kama watu watapigia kura Ilani.. basi mtanange huu wa demokrasia 'UNOGILE".
Mwaka huu watu watapigia kura sura au watapigia sera!
Mkuu Ilani ndio sababu, nia na kuonyesha uwezo wa kutaka kushika madaraka ya kuongoza nchi..Mwanakijiji unaenda mbali saana kwa kuwaza Ilani.
Kamwe nchi hii, ilani haitaiangusha CCM. Leo hii tuulizane hapa hata kabla yakufika kule vijijini, ni nani aliisoma Ilani ya CCM ya 2005 na nani anaweza kuizungumzia utekelezaji wake! Jibu ni kuwa utashangaa saana. Wengi kati yetu tunapenda kusoma mistari miwili na kufunika na hao ndio tunajiita wasomi. Sasa, vipi kuhusu wanakijiji?
Matatizo ni makubwa saana katika kujisomea kwa Taifa letu na ndio maana hata umakini hakuna. Tena basi si kusoma tu hata kuandika. Jipe fursa upitie hata magazeti yetu utashangaa.
Kwahiyo binafsi naona CCM itaondoka madarakani kwa njia za kupayuka tu na kuzungumza na wananchi zaidi juu ya haki zao bila hata ya kuwaeleza ilani inasema nini!
Mama yangu anamiaka 75 na kajiandikisha kupiga kura yeye naye anadai hata iweje hakuna chama kama CCM anadai je wewe mwanagu unaweza kunikataa mimi kuwa si mamako, kwake yeye CCM ndiye mama wa siasa na vyama vyote kwa hiyo vyama vingine havina nguvu au ubavu wa kushindana na chama mama.WanaJF, mimi niko nje lakini najitahidi kukaa karibu na mikoa yote ya Tanzania kupitia mitandao mbali mbali kama hii, najaribu kuifutilia breaking news toka kwenu na vyanzo vingine vya habari. karibu wiki nzima nimejaribu kuhoji watu mbali mbali katika mikoa ya mbeya(kuna marafiki), Dodoma(kuna marafiki), Shinyanga [Kahama na Kishapu(Home)], mwanza(Nilisoma), Tabora (nilisoma), Dar es salaam ( ninakofanya kazi), Arusha (nimefanya kazi), na Manyara( nimefanya kazi). Watanzania wengi ni wavivu wa kujisomea ndo maana wenye vijarida vyenye vituko wanauza, haviitaji kufikiria sana ni kucheka tu na kusisimuka basi.
Kote huko nilikuwa naulizia jinsi Chadema ilivyojipanga au upinzani ulivyo nanguvu, cha kusikitisha mkoa wangu (Shinyanga) wanasema wanataka chama cha Nyerere. Iliniuma sana lakini nitafanyeje! nikabaki kutafuta sababu tu, ambayo nimeona niiweke hapa! CCM imefanikiwa kukaa muda mrefu kwa kuwanyima watu elimu bora, inawapa watu elimu ya kuendeleza umasikini badala ya kuwaondelea umaskini.
Inauma sana kuona mkoa kama shinyanga unakuwa ni kama jimbo la CCM vile. kwa hiyo chadema au vyama vya upinzani tuna kazi, ilani najua itasaidia kwa wajanja wachache, lakini kwenye mikoa kama shinyanga nadhani kuna haja ya kuwafanyia utafiti kabla ya kampeni ili kuweza kuwapa upeo.
Hiyo ni shinyanga, lakini kuna maeneo kibao,mikoa mingi ya namna ambayo ni kama majimbo ya ccm watu hawaelewei, wanatishiwa vita kama vya rwanda, wanaohongwa, wanaokamatwa na kubambikwa kesi yaani ni uonevu kwenda mbele. Lakini yanawezekana, maisha bila ccm yanawezekana kabisa. TWENDE KAZI chadema.
Kama watu hawatapigia kura pilau na pombe za kienyeji, na sh 5000 za kununulia kilo ya nyamaKama ndiyo hiyo, basi itabidi CCM warudi darasani kuandika Ilani yao upya maana kama watu watapigia kura Ilani.. basi mtanange huu wa demokrasia 'UNOGILE".
Mwanakijiji unaenda mbali saana kwa kuwaza Ilani.
Kamwe nchi hii, ilani haitaiangusha CCM. Leo hii tuulizane hapa hata kabla yakufika kule vijijini, ni nani aliisoma Ilani ya CCM ya 2005 na nani anaweza kuizungumzia utekelezaji wake! Jibu ni kuwa utashangaa saana. Wengi kati yetu tunapenda kusoma mistari miwili na kufunika na hao ndio tunajiita wasomi. Sasa, vipi kuhusu wanakijiji?
Matatizo ni makubwa saana katika kujisomea kwa Taifa letu na ndio maana hata umakini hakuna. Tena basi si kusoma tu hata kuandika. Jipe fursa upitie hata magazeti yetu utashangaa.
Kwahiyo binafsi naona CCM itaondoka madarakani kwa njia za kupayuka tu na kuzungumza na wananchi zaidi juu ya haki zao bila hata ya kuwaeleza ilani inasema nini!
Mama yangu anamiaka 75 na kajiandikisha kupiga kura yeye naye anadai hata iweje hakuna chama kama CCM anadai je wewe mwanagu unaweza kunikataa mimi kuwa si mamako, kwake yeye CCM ndiye mama wa siasa na vyama vyote kwa hiyo vyama vingine havina nguvu au ubavu wa kushindana na chama mama.
Loh nikaishiwa hamu,nikajaribu kumueleza maovu yote yanayofanywa na CCM kwani hata muda wa kunisikiliza hakuwa nao akaniambia we mwanangu lakini kwa hilo la kuisema CCM unaenda mbali akafunga mazungumzo, kwa hiyo ni kweli hata Chadema wangekuja na ilani ya uchaguzi nzuri kiasi gani bado kuna safari ndefu kwa wananchi walio wengi kujua ilani kwanza nini au ina manufaa gani.
Tukumbuke enzi za Mkapa alisema ilani ya CCM haitekelezeki na bado tukamchagua mgomnea wa CCM kwa kishindo, ingekuwa ni nchi zingine zenye uelewa juu ya Ilani, CCM ingekuwa ishazikwa zamani kwenye kaburi futi sita ardhini.