Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Mkuu,Binadamu hua anatabia ya kupenda au kushangaa kitu ambacho hana au kitu ambacho kwao hakipo,

Huo umasikini na hivyo vijumba vinavyoongelewa humu,ndio utalii wenyewe huo kwao,wanakuja kutalii/kuona vitu ambavyo kwao havipo,

Hata wewe,mfano ukienda nchi za wazungu ukaishi huko miaka kibao,utatamani kwenda huko kwenye umasikini ili kutalii,kutalii ni kuenjoy na kuona vitu ambavyo kwenu havipo au hujaviona kwa muda mrefu,

Kuna watu wanaishi kwenye majiji makubwa tu ila wakienda vijijini kwao hua wanaenjoy sana na kujihisi kua na amani ndani ya nafsi.
Acha kutetea upumbavu ,yaani MTU afurahie ufukara au kuja kutalii ufukara ? ,Una matatizo
Unajua hata mimi sielewi, kwa nini miji yetu imepangwa hovyo? Halafu tumeridhika nayo tu. Wazungu wa miaka 1900s walistaarabika kwenye jamii zao kuliko Watanzania wa 2025
We angalia Dar tu ilivyo ,taka taka kabisa .ptuuu
 
Sisi watanzania ni wavivu wa kutupwa nisiseme uongo.

Issue ya mtaji wala sio issue. Nipo kijijini huku nawahamasisha watu tuunde kikundi tusajili ili tuingie kwenye 10% ya halmashauri.
Nikiita kikao hakuna anayetokea. Huku nilipo fursa ya kilimo na ufugaji nje nje maana maji ni miezi 12. Vijana hawataki kufanya hizo kazi.

Hakuna wa kuwakomboa watanzania zaidi ya kujikomboa wenyewe kutoka kwenye confort zone. Mtu akiwa na gheto akawa na kashamba ka kahawa anaona ametoboa. Ni shida kwakweli
 
Acha kutetea upumbavu ,yaani MTU afurahie ufukara au kuja kutalii ufukara ? ,Una matatizo wewe
Wewe unaonekana una maisha magumu sana,wala huwezi kuelewa nilichokiandika,

Ni wapi nimetetea ufukara? Au unataka nikutetee wewe choko sio? Mwenye matatizo ni wewe choko unayetafunwa.
 
Kusema kweli bhana ulichokioandika ni kwa nchi zote za Africa,hayo mazingirau uliyoyaelezea hayatofautiani sana na nchi nyingine za Africa.Nchi zenye good welfare kwakweli hazizid hata 8 Zilizobaki zote ni muonekano wa kimaskini tu,bahat nzuri nimetembea sana Africa hasa Africa Mashariki Sijaona tofauti ya vijiji vya Kenya,Uganda,Tanzania,Ethiopia,Zambia,DRC,Malawi,Mozambique,Rwanda,Burundi kote huku nimetembea Tangu mwaka 1997 mazingira ni Yaleyale.

Kitu ambacho naweza nkaongezea ni kwamba Atleast nchi yetu ni nzuri na haina muonekano wa kimaskini sana kushinda nchi nyingine kama Congo na Burundi,hizi nchi ni case study ya umaskini aisee Congo bhana Miji yao ni mizuri mno kuzidi hata baadhi ya miji yetu ukiitoa Dar es salaam ila raia wake ni maskini mno,kuna gape kubwa sana kati ya tajiri wa Congo na maskini wa Congo.

Congo ni nchi ngumu sana aisee pale Border ya Kasumbalesa unaweza ukalala na demu ukimoa kilo moja ya mchele au kwa sisi matransporter tunajua kuna sehemu inaitwa Tangifungurume aisee pale ni balaa raia wamechoka kabisa wanasubiri uoate breakdown maeneo yale wavamie wachukue hata unga wa ugali watu wamechoka,au kuna sehemu inaitwa Kanyaka kabla ya Lubumbashi pale Unga ni dili kuliko kitu chochote utakuta kijana au mmama anadandia gar yako anakulazimisha umpe unga wa ugali.

Tanzania ukiwa na dola 100 kama 250,000 hivi TZS unaweza kuishi kwa siku 2 tatu bila shida ya aina yoyote lakini hii hela kwa Congo ni dk 2 tu imeisha,kuziba pancha tu ya gari utasikia dola 20 sijui kufanyaje dola 50 dk 2 tu dola 100 imeondoka,lakini dola 100 kwa Tz unavimba nayo.Wale maagent na marunners kasumbalesa utakuta wanakaa hadi na dola 40,000 ndani lakini utakuta mtu kapanga na hiyo dola 40,000 hajui hata aiwekeze wapi..
 
Hivi ni mimi peke yangu naliona hili?
Mbona nchi yetu masikini jamani. Mimi nimezaliwa Ruangwa huku Lindi mara nyingi nimeona watu wakipakandia Lindi kwa umasikini hususani mitandaoni, mimi nikadhani ni huku tu hali ni mbaya, mpaka nilivyopata exposure. Maeneo mengi nilizunguka zamani utotoni nikawa sipakumbuki ila miaka ya karibuni nimezunguka sana. So nilikuwa na observe, nione kwa nini watu wanasema Lindi masikini, huenda mikoa mingine ni tajiri

Advance nimesoma Mbeya, nikawa napita njia ya Ruangwa-Masasi-Songea-Mbeya
Kuanzia hapa Ruangwa ukiwa unaenda Songea, hapa kati watu wanaishi maporini kwenye nyumba za matope, nyingine wameezeka nyasi, mabati yana kutu maeneo mengine unaona kabisa hata huduma za msingi hawazipati. Yani kitu kizuri kuangalia ni nature tu, mazingira ya asili kweli Tanzania imebarikiwa

Ukifika Songea sasa, vijiji vyake udongo mwekundu halafu nyumba mbaya yani ukipaangalia kama Uganda. Bora Songea mjini pale kumeendelea halafu nyumba sio mbaya sana. Issue ipo kutoka Ruvuma kwenda Mbeya sasa, vijiji vyote humu kati vimejaa umasikini (bora hata Makambako niliona pana nyumba nzuri) ila nilipofika Mbeya nilibaki mdomo wazi, nikawa najiuliza hili ni jiji? Khaaa
Yani nyumba za matope zimetapakaa milimani kote mji umechafuka kila kona nikiangalia naona umasikini tu.

Sikuipenda hii njia, nikaanza kutumia route ya Dar, natoka home naenda Dar nakaa siku 2 au 3 hivi halafu ndo naenda Mbeya. Dar nilikuwa nafikia Kimara kwa bro, ana nyumba nzuri na mtaa wao mzuri ila umepoa sana. Nikawa natoka asubuhi naenda kuzurura maeneo mengine ya Dar. Aisee kumbe nako ni umasikini tu umejaa. Ila Dar bora kuna miundombinu ambayo inapendeza lakini kuna mitaa nilipita ina nyumba zina kutu, nyumba zimebanana yani hovyohovyo. Nikawa najiuliza ina maana ni mimi tu ndo naona hii nchi haiko sawa? Kutoka Dar hadi Mbeya nako nilisafiri mchana ili nione mazingira nako hivyohivyo tu ni umasikini, sikupenda hata nikawa nasafiri route za usiku

Mwezi May mwaka huu tulisafiri kwenda Kigoma. Jamani hii njia ndo niliona umasikini funga kazi, bora Lindi kwa kweli 🙌
Kuna vijiji vipo Morogoro huku mmh, utafikiri bado wanatawaliwa na mfalme. Tena bora Morogoro, Dodoma kuna vijiji niliona vijiji nyumba watu wamejenga na matofali ya kuchoma halafu juu wameegesha tu bati halafu juu ya bati wameweka matofali ili bati lisiezuliwe na upepo. Aisee, nilishangaa sana, Tabora kuna vijiji tumepita nikaona nyumba zimejengwa style kama nyumba za Kiafrika za nyasi ila tu zenyewe zimejengwa na bati kuanzia juu mpaka chini, zipo nyingi halafu zimekaa kama kambi za wakimbizi. Uzuri nilisafiri na treni, niliona kila kitu vizuri. Kutoka Dar to Kigoma kuna li ardhi likubwa tu limeachwa hamna hata mashamba, wala nini yani nchi kubwa ila hatujui kutumia ukubwa wetu. Nimefika Kigoma nako umasikini wa kutisha

Hata form 4 tulienda study tour Zanzibar, nako ni overrated. Ukitoa pale Stone Town, kuna maeneo ni mabaya. Mji umechoka mbaya, mabati yana kutu. Kuna sehemu Zenji ya masista inaitwa Machui ndo tulipata hostel za kulala sisi wanafunzi, yani hata internet shida, kubaya af ni dakika 30 tu kutoka Stone town. Pako kama Nachingwea. Network inasumbua, migomba mingi kama Bukoba yani pabaya tu.
Tulitoka Stone Town kwenda Nungwi, hapa kati yani nako ilikuwa ni umasikini mtupu. Nilichopenda Zanzibar ni beach ya Nungwi, bei ya vitu pale Darajani, na Forodhani wakati wa usiku kulikuwa na vyakula vya kutosha na watu wa kila race, ila walivyokuwa wanatuzungusha kwenye ma historical site huko nilikuwa naona mabaya tu. Hayavutii. Kamji kamejichokea kinoma

Hadi nimerudi mkoani kwetu Lindi, huku nako ni kubaya. Nyumba mbaya. Yani naona nchi yetu masikini tu kuanzia bara hadi visiwani

Hadi sasa mikoa ambayo sijafika ni Songwe, Rukwa, Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Labda mikoa hii itakuwa tofauti ila sijafika.

Lakini naona vita dhidi ya umasikini tumeishindwa kabisa. Nchi kubwa, resources nyingi ila inasikitisha. Tushukuru Mungu Bongo wananchi wake wavumilivu, wengi wanaonekana kuwa na furaha tu
Ukifika Kilimanjaro ndiyo utajua vizuri tafsiri ya neno umasikini.
Watu wamejichokea na wengi wamenyooka kama mnazi, sababu ya shida na njaa Kali.
Vijumba vyao vya nyasi au makuti au mabanzi ni kama vile vya stone age.
Vijana wako hoi, wao ni kunywa mbundi tu.
Xmas unakuta harrier Kali imepaki lakini nyumba ya udongo na makuti
Nafikiri umasikini ulianzia kilimanjaro
 
Punguza roho ya kwanini ww zunguka Tz nzima hii beach nzuri utazikuta Zanzibar tu bahari zinatunzwa
Lindi pia kuna beach nzuri na safi na hakuna watu wengi
Ni vile tu Lindi sio popular kama Zanzibar
Fika na Mafia pia uone beach nzuri safi na ndio best place for diving in Tanzania. Unadive unaona samaki wa kila aina
 
Ukizunguka hii nchi ndo utajua kama bado tuna safari ndefu.

Halafu raia wake hawana habari wala nini na waneridhika kuwa hivyo. Muhimu wanakula na kulala. Watake nini tena.
 
Mkoa ambao nauelewa na watu wake wameelimika kuhusu mazingira na makazi ni Kilimanjaro.Wachaga nawaheshimu kwa hilo.Makabila yote yajifunze kwa wenzetu wanapenda vitu vizuri.
 
Hivi ni mimi peke yangu naliona hili?
Mbona nchi yetu masikini jamani. Mimi nimezaliwa Ruangwa huku Lindi mara nyingi nimeona watu wakipakandia Lindi kwa umasikini hususani mitandaoni, mimi nikadhani ni huku tu hali ni mbaya, mpaka nilivyopata exposure. Maeneo mengi nilizunguka zamani utotoni nikawa sipakumbuki ila miaka ya karibuni nimezunguka sana. So nilikuwa na observe, nione kwa nini watu wanasema Lindi masikini, huenda mikoa mingine ni tajiri

Advance nimesoma Mbeya, nikawa napita njia ya Ruangwa-Masasi-Songea-Mbeya
Kuanzia hapa Ruangwa ukiwa unaenda Songea, hapa kati watu wanaishi maporini kwenye nyumba za matope, nyingine wameezeka nyasi, mabati yana kutu maeneo mengine unaona kabisa hata huduma za msingi hawazipati. Yani kitu kizuri kuangalia ni nature tu, mazingira ya asili kweli Tanzania imebarikiwa

Ukifika Songea sasa, vijiji vyake udongo mwekundu halafu nyumba mbaya yani ukipaangalia kama Uganda. Bora Songea mjini pale kumeendelea halafu nyumba sio mbaya sana. Issue ipo kutoka Ruvuma kwenda Mbeya sasa, vijiji vyote humu kati vimejaa umasikini (bora hata Makambako niliona pana nyumba nzuri) ila nilipofika Mbeya nilibaki mdomo wazi, nikawa najiuliza hili ni jiji? Khaaa
Yani nyumba za matope zimetapakaa milimani kote mji umechafuka kila kona nikiangalia naona umasikini tu.

Sikuipenda hii njia, nikaanza kutumia route ya Dar, natoka home naenda Dar nakaa siku 2 au 3 hivi halafu ndo naenda Mbeya. Dar nilikuwa nafikia Kimara kwa bro, ana nyumba nzuri na mtaa wao mzuri ila umepoa sana. Nikawa natoka asubuhi naenda kuzurura maeneo mengine ya Dar. Aisee kumbe nako ni umasikini tu umejaa. Ila Dar bora kuna miundombinu ambayo inapendeza lakini kuna mitaa nilipita ina nyumba zina kutu, nyumba zimebanana yani hovyohovyo. Nikawa najiuliza ina maana ni mimi tu ndo naona hii nchi haiko sawa? Kutoka Dar hadi Mbeya nako nilisafiri mchana ili nione mazingira nako hivyohivyo tu ni umasikini, sikupenda hata nikawa nasafiri route za usiku

Mwezi May mwaka huu tulisafiri kwenda Kigoma. Jamani hii njia ndo niliona umasikini funga kazi, bora Lindi kwa kweli 🙌
Kuna vijiji vipo Morogoro huku mmh, utafikiri bado wanatawaliwa na mfalme. Tena bora Morogoro, Dodoma kuna vijiji niliona vijiji nyumba watu wamejenga na matofali ya kuchoma halafu juu wameegesha tu bati halafu juu ya bati wameweka matofali ili bati lisiezuliwe na upepo. Aisee, nilishangaa sana, Tabora kuna vijiji tumepita nikaona nyumba zimejengwa style kama nyumba za Kiafrika za nyasi ila tu zenyewe zimejengwa na bati kuanzia juu mpaka chini, zipo nyingi halafu zimekaa kama kambi za wakimbizi. Uzuri nilisafiri na treni, niliona kila kitu vizuri. Kutoka Dar to Kigoma kuna li ardhi likubwa tu limeachwa hamna hata mashamba, wala nini yani nchi kubwa ila hatujui kutumia ukubwa wetu. Nimefika Kigoma nako umasikini wa kutisha

Hata form 4 tulienda study tour Zanzibar, nako ni overrated. Ukitoa pale Stone Town, kuna maeneo ni mabaya. Mji umechoka mbaya, mabati yana kutu. Kuna sehemu Zenji ya masista inaitwa Machui ndo tulipata hostel za kulala sisi wanafunzi, yani hata internet shida, kubaya af ni dakika 30 tu kutoka Stone town. Pako kama Nachingwea. Network inasumbua, migomba mingi kama Bukoba yani pabaya tu.
Tulitoka Stone Town kwenda Nungwi, hapa kati yani nako ilikuwa ni umasikini mtupu. Nilichopenda Zanzibar ni beach ya Nungwi, bei ya vitu pale Darajani, na Forodhani wakati wa usiku kulikuwa na vyakula vya kutosha na watu wa kila race, ila walivyokuwa wanatuzungusha kwenye ma historical site huko nilikuwa naona mabaya tu. Hayavutii. Kamji kamejichokea kinoma

Hadi nimerudi mkoani kwetu Lindi, huku nako ni kubaya. Nyumba mbaya. Yani naona nchi yetu masikini tu kuanzia bara hadi visiwani

Hadi sasa mikoa ambayo sijafika ni Songwe, Rukwa, Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Labda mikoa hii itakuwa tofauti ila sijafika.

Lakini naona vita dhidi ya umasikini tumeishindwa kabisa. Nchi kubwa, resources nyingi ila inasikitisha. Tushukuru Mungu Bongo wananchi wake wavumilivu, wengi wanaonekana kuwa na furaha tu
Correction mdau...
Nchi tajiri, raia maskini, viongozi wetu MATAJIRI...
 
Lindi pia kuna beach nzuri na safi na hakuna watu wengi
Ni vile tu Lindi sio popular kama Zanzibar
Fika na Mafia pia uone beach nzuri safi na ndio best place for diving in Tanzania. Unadive unaona samaki wa kila aina
Sawa mkuu
 
Ukizunguka hii nchi ndo utajua kama bado tuna safari ndefu.

Halafu raia wake hawana habari wala nini na waneridhika kuwa hivyo. Muhimu wanakula na kulala. Watake nini tena.
Hata hivyo vyakula vya maana vywenyewe ni shida. Proteini kama Nyama, Mayai, Maziwa, Samaki, Kuku na maharage ni anasa kwa wingi, watu wanashindia Sembe mchicha, kisamvu
 
Sisi watanzania ni wavivu wa kutupwa nisiseme uongo.

Issue ya mtaji wala sio issue. Nipo kijijini huku nawahamasisha watu tuunde kikundi tusajili ili tuingie kwenye 10% ya halmashauri.
Nikiita kikao hakuna anayetokea. Huku nilipo fursa ya kilimo na ufugaji nje nje maana maji ni miezi 12. Vijana hawataki kufanya hizo kazi.

Hakuna wa kuwakomboa watanzania zaidi ya kujikomboa wenyewe kutoka kwenye confort zone. Mtu akiwa na gheto akawa na kashamba ka kahawa anaona ametoboa. Ni shida kwakweli
Mikopo ya 10% ni uongo, porojo, ulaghai na propaganda za siasa za CCM, Wewe inawezekana ni kada wa chama.
 
Kutembea Ni Kuona Mengi
Umasikini Upo Tena Kwa Wengi
Tuendelee Kuzaana Tu, Elimu Ni Bure
 
Wilaya za moro , kwanzia mvomero , kilosa, ifakara , zote hizo zina fursa za mtu kutoka kimaisha ni uvivu tu wa wakazi wa huko .
Kile Chama Ni Tatizo
Maeneo Yapo Sawa Mpaka Ufike Kiwanda Cha Sukari ♥️ Unaona Uzuri Wa Nchi
 
Anza kwanza kuukimbiza umaskini kwenye FAMILY LEVEL.

Your still young ulikua utagundua ilivyo ngumu ku ufukuza umaskini katika national level it takes decades
We Mjinga acha ubinafsi. Yanahitajika magari mangapi yenye thamani ya milioni 500+ kujenga viwanda ambavyo vingeweza kupunguza umasikini? Mkiwa huko CCM mnawa kuiba tu?
 
Majority wana malnutrition...

Kukosa exposure ndio inazidi kudidimiza. Nao baada ya kugundua hili. Wanatunia huu udhaifu kuwafanya watakavyo.
 
Back
Top Bottom