Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Nchi nzima inanuka umasikini. Unakuta barabarani hapo pana ghorofa nzuri zimepaa hewani, Sasa zunguka mtaa wa pili tu hapo watu wamebanana kwenye vijumba wanaume na vitaulo vyao wanapishana kwenye korido za chumba kimoja na seble na watoto 6 wakubwa unajiuliza Hadi unachoka.
Nyama tunawaachia wengine sisi tunakula miguu ya kuku.
 
Ukitaka kujua utamu wa dafu hadi uchokonoe ndani.

Huwezi kupita ukiwa ndani ya basi uka judge umasikini au utajiri wa sehemu.
Definition ya utajiri au umasikini ina vigezo vingi mno hata Marekani tunasema ni taifa lililoendelea lakini kuna sehemu ukipita vijijini hata baadhi ya miji kama Memphis unaweza sema afadhali Dar Tandale.

Nikupe mfano kuna sehemu ukienda Zambia unaweza kuta nyumba za majani ila unakuta nje kuna VX Limepaki nje la milioni250.Ukienda Tabora unaweza kuta vijijini vingine nyumba za majani lakini madirisha ya vioo tinted a dish nje la mitandao.Kwa vigezo vyako hao huwezi kuwaita ni watu masikini ni utamaduni wao.
Je mtu kama ana uhakika wa kula kwa mwaka mzima chakula kizuri cha afya ila nyumba yake ni ya majani huwezi kumuweka huyo mtu kwenye kundi la umasikini.Usipime vigezo vya umasikini na utajiri kwa mijengo peke yake yapo mambo mengi ya kuangalia.

Mtu wa kijijini ana magunia 300 ya mahindi na 300 ya mchele 100 ya mtama.Na hayo magunia ni ajili yake tu kula na familia yake.Mifugo kadhaa ya kuku na ng'ombe 300 wako porini machungani.Ana tractor na analima chakula chake na cha kuuza cha ziada nyumba yake ni ya majani kulingana na jadi yao.Ana tractor la kulimia huyu utamuita masikini?.
Mwingine anaishi mjini ana nyumba ya ghorofa moja ila kajenga kwa mkopo na nyumba iko kwenye bondi.Madali wa Majembe auction mart wanakwepana anadaiwa kati ya mtu huyu na huyo mwenye nyumba ya majani ni nani tajiri na nani masikini?

Hata huko Lindi na Ruangwa unakokuongelea ukipita barabarani kwa vigezo vyako utaona ni masikini lakini ukiingia ndani ndani unaweza kuta watu wana maendeleo ya ajabu.Mara nyingi matajiri hawapendi kukaa sehemu zenye misongamano nenda hata Marekani ma Celebrity uone wanapoweka mijengo yao wanakuwa na hadi viwanja vyao vya ndege binafsi

Hata Kilimanjaro wanasifiwa wameendelea lakini mji wa Moshi wenyewe ukiuona utaona wa kawaida.Ukipita sehemu za wapare utaona mpauko na kama nusu jangwa.
Sasa kwa kilimanjaro na upareni kwa ujumla maendeleo hayako unavoona ukiwa kwenye basi panda kule juu milimani uone matusi yao.
Kule unakuta mtu ana umri wa miaka 65 amezaliwa amekuta bomba la maji nyumbani kwao hawajui kitu kinaitwa kuteka maji kichwani na kuna mijengo ya hatari maendeleo ya shule na vyuo ndio usiseme.Wajerumani walifika kule mapema sana wakajenga makanisa na shule za misheni hata Ndanda Mtwara.

Nenda kwa kina Nshomile utakuta hali kama ya Kilimanjaro na Mbeya
Usi judge maendeleo ya watu ukiwa umekaa kwenye basi pata muda teremka ingia ndani ndani.

Nimekuwekea picha moja chini nilikwenda siku moja Upareni acha pale chini Mwanga palipokauka ukame nilipanda sehemu moja inaitwa Usangi milimani kabisa juu hadi kule ni lami na ni kijani kibichi tulikwenda.
kwenye msiba nikaona nyumba kama hiyo hapo unaweza sehemu hao wapare ni masikini hawana maendeleo?.Cha ajabu sijakutana na nyumba ya majani hata moja achilia angalau iliyopigiliwa mabati ya madebe.
Tembea ujione usingoje kuambiwa aliimba marehemu Dr Remmy Ongala.
 
Attachments

  • uparekijijini.jpg
    uparekijijini.jpg
    207.1 KB · Views: 20

Unasema nyumba na majengo hazipimi umasikini halafu chini unaniwekea picha ya jengo zuri kijijini kuonesha kuwa umasikini upo chini
Make it make sense please
 
Tanzania matajiri wa kweli WACHACHE sana, wengi wapigaji tu na 10% za udalali wa kila kitu, pamoja na Rushwa. Na ndo maana huwezi kuona impact sana ya hao wanaojiita so matajiri.Hauoni kila mtu anakimbilia kwenye siasa, awe mbunge, sasa hivi hadi Udiwani watu wanataka kutoana macho -ni ujanja ujanja.
Middle class hapo imejaa mikopo na madeni sio mchezo....
Hii bongo watu wamechoka sana, na usishtushwe na magari sijui nyumba, hivyo vinaficha umaskini na hofu ya maisha kwa walio wengi.
Matajiri wa kweli wapo bana sio kweli na wanaogombea udiwani ni wangapi bwashee mpaka useme matajiri hakuna aisee mtu anunue Ford Raptor la 2023 kodi Tsh 46m harafu useme wananunua kuficha umasikini sio kweli aisee.
 
Unasema nyumba na majengo hazipimi umasikini halafu chini unaniwekea picha ya jengo zuri kijijini kuonesha kuwa umasikini upo chini
Make it make sense please
hili nalijua sana na najua nilichofanya
Nia yangu nikukuonyesha kuwa usipite kwenye basi tu unaona nyumba za ajabu uka conclude umasikini wa nchi nzima.
Tembea interior zaidi
Hata kwenye statistics utafiti wako haujakaa sawa ulichofanya ni random sampling
Na inategemea wakati unafanya hiyo sampling ulipita maeneo gani.
Collect enough data to make a conclusion.
Hata hivyo ndugu yangu nikupongeze na nisikukatishe tamaa umefanya vizuri kutuamsha kwa kweli kazi yako nzuri
 
Sawa mkuu nimekuelewa. Nitafanya utafiti lakini hili suala tunasoma hata shuleni na vyuoni kuwa umasikini Tanzania upo kwa kiwango kikubwa na ni moja ya nchi zenye masikini wengi zaidi Africa (takribani milioni 28) meaning kila utafiti unaofanyika unaleta matokeo yaleyale
 
Halafu upande mwingine wa shillingi ni ajabu kwa kweli halafu moja ya nchi zenye utajiri mkubwa wa mali asili ni Tanzania.
Kwa nchi za Africa mashariki chukua Burundi,Rwanda,Kenya,Uganda,Tanzania sisi tunaongoza kwa rasilimali misitu,madini,mbuga za wanyama.
Ajabu ni masikini ukiiachia Burundi
Uganda wakianza kuchimba mafuta yao watatuzidi mbali sana.
Je sababu ni nini?
Siasa?
Baba wa taifa moja ya mistake aliyofanya ni kuleta ile siasa ya ujamaa na siasa nyingi sana.Hii imetu affect vizazi hadi vizazi tumeshaamka ila tumechelewa.
Sisi maneno ni mengi mno kuliko vitendo.
Tunatumia hela nyingi mno kwenye mambo ya chaguzi sisizo na mashiko kisa tu chama flani kisishinde.
Ndio maana watani jirani zetu Kenya wanapenda kututania kuwa wa TZ longo longo nyingi sana.
Askari wa Kenya akimkamata mtanzania hataki kubishana naye anajua atamshinda.
 
Hivi ni mimi peke yangu naliona hili?
Mbona nchi yetu masikini jamani. Mimi nimezaliwa Ruangwa huku Lindi mara nyingi nimeona watu wakipakandia Lindi kwa umasikini hususani mitandaoni, mimi nikadhani ni huku tu hali ni mbaya, mpaka nilivyopata exposure. Maeneo mengi nilizunguka zamani utotoni nikawa sipakumbuki ila miaka ya karibuni nimezunguka sana. So nilikuwa na observe, nione kwa nini watu wanasema Lindi masikini, huenda mikoa mingine ni tajiri

Advance nimesoma Mbeya, nikawa napita njia ya Ruangwa-Masasi-Songea-Mbeya
Kuanzia hapa Ruangwa ukiwa unaenda Songea, hapa kati watu wanaishi maporini kwenye nyumba za matope, nyingine wameezeka nyasi, mabati yana kutu maeneo mengine unaona kabisa hata huduma za msingi hawazipati. Yani kitu kizuri kuangalia ni nature tu, mazingira ya asili kweli Tanzania imebarikiwa

Ukifika Songea sasa, vijiji vyake udongo mwekundu halafu nyumba mbaya yani ukipaangalia kama Uganda. Bora Songea mjini pale kumeendelea halafu nyumba sio mbaya sana. Issue ipo kutoka Ruvuma kwenda Mbeya sasa, vijiji vyote humu kati vimejaa umasikini (bora hata Makambako niliona pana nyumba nzuri) ila nilipofika Mbeya nilibaki mdomo wazi, nikawa najiuliza hili ni jiji? Khaaa
Yani nyumba za matope zimetapakaa milimani kote mji umechafuka kila kona nikiangalia naona umasikini tu.

Sikuipenda hii njia, nikaanza kutumia route ya Dar, natoka home naenda Dar nakaa siku 2 au 3 hivi halafu ndo naenda Mbeya. Dar nilikuwa nafikia Kimara kwa bro, ana nyumba nzuri na mtaa wao mzuri ila umepoa sana. Nikawa natoka asubuhi naenda kuzurura maeneo mengine ya Dar. Aisee kumbe nako ni umasikini tu umejaa. Ila Dar bora kuna miundombinu ambayo inapendeza lakini kuna mitaa nilipita ina nyumba zina kutu, nyumba zimebanana yani hovyohovyo. Nikawa najiuliza ina maana ni mimi tu ndo naona hii nchi haiko sawa? Kutoka Dar hadi Mbeya nako nilisafiri mchana ili nione mazingira nako hivyohivyo tu ni umasikini, sikupenda hata nikawa nasafiri route za usiku

Mwezi May mwaka huu tulisafiri kwenda Kigoma. Jamani hii njia ndo niliona umasikini funga kazi, bora Lindi kwa kweli 🙌
Kuna vijiji vipo Morogoro huku mmh, utafikiri bado wanatawaliwa na mfalme. Tena bora Morogoro, Dodoma kuna vijiji niliona vijiji nyumba watu wamejenga na matofali ya kuchoma halafu juu wameegesha tu bati halafu juu ya bati wameweka matofali ili bati lisiezuliwe na upepo. Aisee, nilishangaa sana, Tabora kuna vijiji tumepita nikaona nyumba zimejengwa style kama nyumba za Kiafrika za nyasi ila tu zenyewe zimejengwa na bati kuanzia juu mpaka chini, zipo nyingi halafu zimekaa kama kambi za wakimbizi. Uzuri nilisafiri na treni, niliona kila kitu vizuri. Kutoka Dar to Kigoma kuna li ardhi likubwa tu limeachwa hamna hata mashamba, wala nini yani nchi kubwa ila hatujui kutumia ukubwa wetu. Nimefika Kigoma nako umasikini wa kutisha

Hata form 4 tulienda study tour Zanzibar, nako ni overrated. Ukitoa pale Stone Town, kuna maeneo ni mabaya. Mji umechoka mbaya, mabati yana kutu. Kuna sehemu Zenji ya masista inaitwa Machui ndo tulipata hostel za kulala sisi wanafunzi, yani hata internet shida, kubaya af ni dakika 30 tu kutoka Stone town. Pako kama Nachingwea. Network inasumbua, migomba mingi kama Bukoba yani pabaya tu.
Tulitoka Stone Town kwenda Nungwi, hapa kati yani nako ilikuwa ni umasikini mtupu. Nilichopenda Zanzibar ni beach ya Nungwi, bei ya vitu pale Darajani, na Forodhani wakati wa usiku kulikuwa na vyakula vya kutosha na watu wa kila race, ila walivyokuwa wanatuzungusha kwenye ma historical site huko nilikuwa naona mabaya tu. Hayavutii. Kamji kamejichokea kinoma

Hadi nimerudi mkoani kwetu Lindi, huku nako ni kubaya. Nyumba mbaya. Yani naona nchi yetu masikini tu kuanzia bara hadi visiwani

Hadi sasa mikoa ambayo sijafika ni Songwe, Rukwa, Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Labda mikoa hii itakuwa tofauti ila sijafika.

Lakini naona vita dhidi ya umasikini tumeishindwa kabisa. Nchi kubwa, resources nyingi ila inasikitisha. Tushukuru Mungu Bongo wananchi wake wavumilivu, wengi wanaonekana kuwa na furaha tu
Mimi nilisafiri kwenda Kilimanjaro 2023.
Sababu ni kudhibitisha niliyokuwa naambiwa kwamba wachaga ni matajiri sana.
Kwamba kila mchagga ana nyumba nzuri ya kisasa, gari, umeme, maji na shule zenye majengo mazuri kama ulaya au marekani.

1. HIMO
Nilianzia soko la Himo....na siku hiyo ilikuwa siku ya soko na mvua ilikuwa imenyesha muda mfupi uliopita. Hayo matope na uchafu sasa utafikiri siyo soko ni dampo.
Watu wamechoka kiafya na kimavazi.
Kwa hali ya soko ilivyo mbaya na ya watu unaweza kufikiri uko mwaka wa 500BC.

Wakati natoka soko la himo , nikamuomba mwenyeji wangu anipekeke Himo mjini nipaone.
Kifupi Himo hakuna mji ni vijumba vya ovyo ovyo, vichafu na vilivyozeeka. Vingi vikiwa vimejengwa miaka 50 au zaidi iliyopita.

2. MARANGU, MAMBA, MWIKA
Kuanzia marangu, mamba, mwika ambako ndiyo kwa wachaga wenyewe, umaskini ni wa kutisha. Nyumba na watu wamechakaa... Ispokuwa nyumba mbili tu sikuona nyumba ya kuitwa nyumba.
Magari ndiyo kabisaa sikuyaona...na shule zote za serikali ziko hoi.

Cha kushangaza na hii ni kwa sehemu zote nilizopita—Marangu, Mamba, na Mwika— kuna Makanisa makubwa, mazuri na ya kufa mtu.

Huwezi kuamini majengo hayo ya makanisa yamejengwa in the midst of poverty kwa faida gani.

Ni kama vile yalijengwa hivyo ili kuudhihaki umaskini wa wenyeji wanayoyazunguka makanisa hayo.
 
Ukitaka kupata tafsiri sahihi ya umaskini wa Tanzani nenda Moshi vijijini.

Wachaga wa miaka hii ya CCM wamepigika siyo mchezo.

Vijana wa huko wamenyooka kama mnazi kwa sababu ya kunywa mbundi, "kongo", highlife.

Yale majengo mazuri yaliyojengwa miaka ya 1960/70 yote yako hoi. Bati na rangi zimechakaa kama watu wenyewe.

Kwa kifupi, Moshi vijijini ya miaka hii ni sawa na stone age.

Ukienda Rombo sasa: mama weee. Utafikiri uko pori la Ruangwa kule Lindi.

Nyumba nyingi ni za mabanzi na bati chafu chafu za kuokoteza kwa wauzaji wa chuma chavu.

Nyie Warombo hizo pesa mnazotulangua kwenye mishikaki na bia hapa saridalamu mnzipeleka wapi?

NB
Kuna kitu kimoja tu wachaga wamejitahidi: kujenga makanisa ya kufa mtu.

Hiyo mijengo bwashee ni kufuru bin kufuru.

Na kwa hili, wachaga wote wataenda mbinguni. Nawahakikishieni.
 
Kuna gepu kubwa sana kati ya tajiri na masikini Tanzania. Kubwa sana.
Kubwa mno mkuu..
Hii kauli yako niliwahi semaga kipindi flani..
Gepu kubwa sana sana sana aiseee
Kuna jamaa angu nilikua naongea nae anasema "" kaka unajua kuna mtu ananunua gari la million 80 wakati mimi katika kupambana kwangu natakiwa nipate million moja tu ili nitoboe""

Angalia hapo ndo utaamini gape ni kubwa mno...

Yote kwa yote sapport zenu wakuu
608702.png
 
Masisiemu ndio yameifikisha nchi ktk kiwango hiki kikubwa cha umasikini. WALAANIWE MASISIEMU WOTE WAO NA VIZAZI VYAO MILELE NA MILELE
 
Hadi sasa mikoa ambayo sijafika ni Songwe, Rukwa, Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Labda mikoa hii itakuwa tofauti ila sijafika.
Ni kweli umasikini ni mkubwa sana na viongozi wetu hawaoni hilo kwasababu ndio mazingira waliyozaliwa na kukulia tena wanasema vijana wa siku hizi hamuujui umaskini, miaka ya 60 hadi 90 kulikuwa na umaskini kweli kweli.

Safiri hadi Kilimanjaro huko kuna nafuu kubwa.
 
Back
Top Bottom