Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Hii inaitwa kipofu kaona mwezi.Au mshamba naye ametoka kidogo.
Usije dhani Marekani ilivyo kubwa nako hakuna vijiji na watu wana nyumba za hovyo.
Hebu nenda Kilimanjaro ila usije ku i judge ukiwa umekaa kwenye basi ka mji ka Moshi utakaona kahovyo sana sasa wewe mtafute rafiki yeyote akupandishe kule milimani Machame na Marangu.
Ukipita kwa wapare utapita sehemu inaitwa Mwanga usije ku i judge palivyo pakame wapare na wachaga huwa wako milimani panda kule juu mfano kwa Wapare Usangi uone maendeleo ya huko kisha rudi hapa toa comment tena.Wajerumani hizi sehemu walizipendelea sana ndio maana wakatangulia sana kimaendeleo hasa miungo mbinu.
Uzuri wa dafu hadi ulipasue uone kilicho ndani
 
"Mshamba naye katoka kidogo"
Ingekuwa nimeenda sehemu nzuri nikaja kuipamba huku ningekuelewa kuniita mshamba. Sasa nimetoka nje nimekutana na umasikini wa kutisha, nakuja kusema humu ndio unaniita mshamba?
 
Sio suala la uchumi tu, hata mambo ya msingi na ya kawaida kama kupanga miji yametushinda. Kuna nchi hazina uchumi mkubwa sana mfano Cuba ila miji imepangwa ikapangika. Wazungu hata kabla hawajaendelea walikuwa wanapanga miji vizuri
Unajua hata mimi sielewi, kwa nini miji yetu imepangwa hovyo? Halafu tumeridhika nayo tu. Wazungu wa miaka 1900s walistaarabika kwenye jamii zao kuliko Watanzania wa 2025
 
Ila ni kweli Tanzania na Africa yote hii umasikini umezidi na hapo umasikini wa Tanzania tu unaushangaa hivi. Nenda Kenya huko ukutane na Kibera, Mathare, Uthiru, Githurai na Pipeline ndio utazimia kabisa 😂😂😂

Angalia hii video, hapa ni Mbweni, Dar es Salaam. Cha muhimu Tanzania tuwe na mitaa mingi kama hii. Na ili tuwe na mitaa mingi kama Mbweni lazima Watanzania wengi wawe na hela so tufikirie jinsi ya kuongeza mzunguko wa hela hususani mikoani maana hali ni mbaya zaidi huko, ili Watanzania wajiajiri waishi sehemu nzuri.
 
Wewe unaona huu ni umasikini ?!!!! Ngoja hawa machinga na wabangaizaji wafikie uzee ndio utaona umasikini wenyewe wa ombaomba mpaka mlangoni kwako (kwa kasi hii tutawazidi India)

Mkuu,umesoma ili ufaulu mitihani haukusoma ili uondoe ujinga kichwani mwako. Unajua vipimo vya umasikini wewe au unajua ukiona nyumba mbaya tayari huyo mtu ni masikini? Rudi darasani ukajifunze upya hasa hasa ukianza kidato cha kwanza itapendeza zaidi. Cc mtaalamu wa uchumi tlatlaa
 
Nchi hii, hasa Dar kuna masikini wengi sana. Imagine wastani wa pato la mtu wa Dar ni kama 5m. Hapo hapo wamejumuishwa wakina Bakhresa, Mo, GSM na matajiri wengine wote wa mjini. Ukitoa matajiri 10,000 utakuta wastani wa pato la watu ni kama watu wa Burundi.
 
Mkuu,umesoma ili ufaulu mitihani haukusoma ili uondoe ujinga kichwani mwako. Unajua vipimo vya umasikini wewe au unajua ukiona nyumba mbaya tayari huyo mtu ni masikini? Rudi darasani ukajifunze upya hasa hasa ukianza kidato cha kwanza itapendeza zaidi. Cc mtaalamu wa uchumi tlatlaa
Swali rahisi tu, kama nyumba (makazi) sio kigezo cha kuangalia umasikini basi nijibu kwa nini nchi masikini maeneo mengi yapo hivi
FB_IMG_1761550480887.jpg
Screenshot_2025-10-27-10-36-40-736_com.facebook.katana-edit.jpg
Screenshot_2025-10-27-10-38-20-102_com.android.chrome.png

Na kwa nini kwenye nchi tajiri maeneo mengi yapo hivi
53995d26c7f8fc64420b25a88372632d.webp
typical-american-new-construction-neighborhood-single-family-homes-usa-real-estate-302924048.jpg
200720041511-suburban-homes-restricted.jpg
What-are-the-Wealthiest-Chicago-Suburbs-Top-HighEnd-Communities-s.jpg

Na swali lingine, ni vigezo gani vinatumika kupima umasikini? Nitajie vigezo hivyo halafu nikuonesha kuwa hata kupitia vigezo vyako Tanzania bado ni masikini
 
Nazungumzia asili yaan nature mazingira muonekano wa huko bush machakani hewa safi sizungumzii miundombinu ambako mpaka leo ukiondoa Lindi na Ruangwa huko Tandahimba vijijini, Newala vijijini, Masasi vijijini mpaka Chetekete huko Chitangali mpaka Mkoma barabara ya lami ni anasa ni vumbi kwa kwenda mbele
Mahali popote pa asili ni pazuri na kuna hewa safi, hata pakiwa jangwani kama huko Sahara na Uarabuni au kwenye barafu kama huko Marekani na Ulaya.
 
Mahali popote pa asili ni pazuri na kuna hewa safi, hata pakiwa jangwani kama huko Sahara na Uarabuni au kwenye barafu kama huko Marekani na Ulaya.
Ndio, kuna sehemu nimepita Safari kutalii huko vijijini kuna miti mizuri imenyooka juu sana mpaka nikatamani kupiga picha then nikavuta picha km ningeishi pale kuna hewa safi saaana na pametulia sio kawaida ni sauti za ndege tu eneo kubwaaaa limejaa miti mirefuuuu mizuriiiiiii
 
Kama Kuna mtu tu analipwa milioni 500 kwa kibarua cha siku.moja tu nchi hii, na nchi hii hii tu Kuna mtu analipwa elfu 3 kwa kibarua Cha siku Moja tu...tabaka la maskin na matajiri nchi hii ni kubwa sana ..na ndio mana watu wameamka na unaona Kuna movement za kuikomboa nchi na ndio mana wanalindwa kwa nguvu zote
 
Swali rahisi tu, kama nyumba (makazi) sio kigezo cha kuangalia umasikini basi nijibu kwa nini nchi masikini maeneo mengi yapo hivi
View attachment 3494466View attachment 3494467View attachment 3494468
Na kwa nini kwenye nchi tajiri maeneo mengi yapo hivi
View attachment 3494469View attachment 3494470View attachment 3494471View attachment 3494472

Na swali lingine, ni vigezo gani vinatumika kupima umasikini? Nitajie vigezo hivyo halafu nikuonesha kuwa hata kupitia vigezo vyako Tanzania bado ni masikini
Hana akili timamu huyo, elimu yake ndiyo itakuwa haijamsaidia kitu.
 
Kwa afya yake, usafi wake, mavazi yake, makazi yake, chakula chake, maji yake n.k
mtu anaishi nyumba ya nyasi,ana gunia 200 za mpunga ndani,ana gunia 150 za mahindi,ana ng'ombe 300 wengine kawapeleka sehemu nyingine malishoni huyo mtu unaweza kumweka kundi gani. Wengi wanaongelea mtu masikini ni yule hana nyumba nzuri ya kuishi,lakini ukweli ni kwamba wanajidanganya, mleta mada huwa anapita tu vijijini anachungulia dirishani na kuona nyumba zilizoezekwa kwa makuti na kutoa picha ya jamii yote ni maskini,hataki kujifunza tamaduni na mwenendo mnzima wa maisha ya watu. Naweza kuta mtu amejenga nyumba nzuri lakini life style yake haiko sawa,nyumba hiyo ameiweka bond,hana kitu zaidi ya kufanya biashara ya mkopo, unamlinganishaje mtu huyo na mfugaji,mwenye mashamba,mkulima aliyeamua kujenga nyumba zilizoezekwa kwa makutu? Lazima unapoleta mada yako ufanye na utafiti kidogo ufuatilie life style za watu hao unaowazungumzia. Afya bora,mavazi si kipimo cha umas
 
Back
Top Bottom