Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Ila jamani nchi yetu ni masikini, khaa

Tanzania matajiri wa kweli WACHACHE sana, wengi wapigaji tu na 10% za udalali wa kila kitu, pamoja na Rushwa. Na ndo maana huwezi kuona impact sana ya hao wanaojiita so matajiri.Hauoni kila mtu anakimbilia kwenye siasa, awe mbunge, sasa hivi hadi Udiwani watu wanataka kutoana macho -ni ujanja ujanja.
Middle class hapo imejaa mikopo na madeni sio mchezo....
Hii bongo watu wamechoka sana, na usishtushwe na magari sijui nyumba, hivyo vinaficha umaskini na hofu ya maisha kwa walio wengi.
Umeongea pointi kubwa sana. Ndio maana huoni impact ya hao matajiri. Kwa sababu utajiri wao sio halisi.
 
Umeongea pointi kubwa sana. Ndio maana huoni impact ya hao matajiri. Kwa sababu utajiri wao sio halisi.
Utajiri wa wengi uko juu ya mchanga tu..
Mfano Mo ni tajiri lkn ukitaka kupata historia ya utajiri iko wazi kabisa....
Hawa weusi wenzetu: utaona migari ya 500M imetapakaa siku hizi kila kona, lkn huoni vice versa..meaning..huoni viwanda, huoni uzalishaji unaoeleweka, Hii nchi miujiza mingi sana.Miaka inavyoenda kuna bomu la ajira linakuja - maana hadi bodaboda kumejaa sasa....
 
Utajiri wa wengi uko juu ya mchanga tu..
Mfano Mo ni tajiri lkn ukitaka kupata historia ya utajiri iko wazi kabisa....
Hawa weusi wenzetu: utaona migari ya 500M imetapakaa siku hizi kila kona, lkn huoni vice versa..meaning..huoni viwanda, huoni uzalishaji unaoeleweka, Hii nchi miujiza mingi sana.Miaka inavyoenda kuna bomu la ajira linakuja - maana hadi bodaboda kumejaa sasa....
Wapo matajiri wa kilimo bwashee, hakuna kona kona ni wewe na mazao yako na soko lako tu.
 
Wapo matajiri wa kilimo bwashee, hakuna kona kona ni wewe na mazao yako na soko lako tu.
Yap, ni kweli na kuna wavuvi Mwanza kule, ukiwaona washambawashamba, ila wanamizigo hatari.
Shida ni wachache sana hao: si unaona mtoa mada anahuzunika maeneo makubwa lakini hayalimwi, hayaendelezwi etc..it means anaongelea mfumo ulioimara kuanzia kwenye taasisi za kifedha, venture capital ili kusaidia watu kupata mitaji.
Kuna microfinance mitaani huko zinakopesha wamama, hilo balaa lake si la nchi hii...KAUSHA DAMU..Sasa mtu wa kawaida aanze biashara na kausha damu??Mabank.wanahitaji watu formal, wakati asilimia kubwa ni informal na wanaishi unplanned settlements kwa wa mijini, vijijini huko wasubiri.
 
Yap, ni kweli na kuna wavuvi Mwanza kule, ukiwaona washambawashamba, ila wanamizigo hatari.
Shida ni wachache sana hao: si unaona mtoa mada anahuzunika maeneo makubwa lakini hayalimwi, hayaendelezwi etc..it means anaongelea mfumo ulioimara kuanzia kwenye taasisi za kifedha, venture capital ili kusaidia watu kupata mitaji.
Kuna microfinance mitaani huko zinakopesha wamama, hilo balaa lake si la nchi hii...KAUSHA DAMU..Sasa mtu wa kawaida aanze biashara na kausha damu??Mabank.wanahitaji watu formal, wakati asilimia kubwa ni informal na wanaishi unplanned settlements kwa wa mijini, vijijini huko wasubiri.
Ni kweli kabisa , ila naona wa Tanganyika wengi hatuna ile hamasa ya kufanikiwa sana , tofauti na wakenya na waganda
 
Kilimanjaro natamani nifike siku moja, kama chuo ningeenda ATC ingekuwa easy kwenda Kilimanjaro. Ila nina mpango wa kwenda mikoa yote ambayo sijakanyaga
Morogoro pale mjini tulipokatisha niliona pako poa tu kwa standard za Bongo, ila shida sanasana ni vijijini ambako ndio most of time unapaona ukiwa unasafiri
Hamna mkoa uliokosa vijiji/mitaa ya masikini hapa Tz.

Huko Lindi ndo balaa, kunasifika kwa umasikini wa kutupwa na miundombinu duni.

Kuna kijiji nilifika huko Shinyanga, wanakunywa maji kama wanayokunywa wanyama aisee, ni machafu, wageni wanapewa matikiti walau wapoze kiu maana yale maji wengi tuliyashindwa.

Na mbaya zaidi wengi huzeekea kwenye hali hiyohiyo bila kubadili mazingira, matokeo yake ni ngumu kupata mabadiriko.
 
Weeks ago nilikua na dada Fulani sio mtanzania Kuna watu alikua anaongea nao mtaani Mimi namsaidia,sasa Kuna mama tukapanga kuonana nae mfanya biashara ndogondogo akawa anamuuliza maswali,

Yule mama akaulizwa kipato chake kwa siku (siku nzuri) akasema buku 5,.. after the interview yule dada niliekua nae aliumwa mawazo week nzima story Ile ile..haamini inawezekana vipi??

Nikamuuliza swali ambalo mtoa mada nawewe unijibu,unafikiri wanaposema Pato la mtanzania ni chini ya dollar ulifikiri wanazungumzia Nini?? I've been in places bro watu masikini kuzidi ulivyoona Wala kusikia
 
Mtu akisha kula ugali mkubwa na mboga kiduchu hapo ameshamaliza matatizo yake
, mtu kila siku analima na anauza magunia ya kutosha lakini kila siku analala kwenye kinyumba cha matope kibovu....

Mimi nashangaa huku kwenye nyumba za matope kwani hawawezi kujitutumua ikawa ya kama hiyo hapo chini, hata vijiji vyetu vingependeza...
1761507230805.png


1761507314520.png

1761507397551.png

1761507430764.png
 
Hivi ni mimi peke yangu naliona hili?
Mbona nchi yetu masikini jamani. Mimi nimezaliwa Ruangwa huku Lindi mara nyingi nimeona watu wakipakandia Lindi kwa umasikini hususani mitandaoni, mimi nikadhani ni huku tu hali ni mbaya, mpaka nilivyopata exposure. Maeneo mengi nilizunguka zamani utotoni nikawa sipakumbuki ila miaka ya karibuni nimezunguka sana. So nilikuwa na observe, nione kwa nini watu wanasema Lindi masikini, huenda mikoa mingine ni tajiri

Advance nimesoma Mbeya, nikawa napita njia ya Ruangwa-Masasi-Songea-Mbeya
Kuanzia hapa Ruangwa ukiwa unaenda Songea, hapa kati watu wanaishi maporini kwenye nyumba za matope, nyingine wameezeka nyasi, mabati yana kutu maeneo mengine unaona kabisa hata huduma za msingi hawazipati. Yani kitu kizuri kuangalia ni nature tu, mazingira ya asili kweli Tanzania imebarikiwa

Ukifika Songea sasa, vijiji vyake udongo mwekundu halafu nyumba mbaya yani ukipaangalia kama Uganda. Bora Songea mjini pale kumeendelea halafu nyumba sio mbaya sana. Issue ipo kutoka Ruvuma kwenda Mbeya sasa, vijiji vyote humu kati vimejaa umasikini (bora hata Makambako niliona pana nyumba nzuri) ila nilipofika Mbeya nilibaki mdomo wazi, nikawa najiuliza hili ni jiji? Khaaa
Yani nyumba za matope zimetapakaa milimani kote mji umechafuka kila kona nikiangalia naona umasikini tu.

Sikuipenda hii njia, nikaanza kutumia route ya Dar, natoka home naenda Dar nakaa siku 2 au 3 hivi halafu ndo naenda Mbeya. Dar nilikuwa nafikia Kimara kwa bro, ana nyumba nzuri na mtaa wao mzuri ila umepoa sana. Nikawa natoka asubuhi naenda kuzurura maeneo mengine ya Dar. Aisee kumbe nako ni umasikini tu umejaa. Ila Dar bora kuna miundombinu ambayo inapendeza lakini kuna mitaa nilipita ina nyumba zina kutu, nyumba zimebanana yani hovyohovyo. Nikawa najiuliza ina maana ni mimi tu ndo naona hii nchi haiko sawa? Kutoka Dar hadi Mbeya nako nilisafiri mchana ili nione mazingira nako hivyohivyo tu ni umasikini, sikupenda hata nikawa nasafiri route za usiku

Mwezi May mwaka huu tulisafiri kwenda Kigoma. Jamani hii njia ndo niliona umasikini funga kazi, bora Lindi kwa kweli 🙌
Kuna vijiji vipo Morogoro huku mmh, utafikiri bado wanatawaliwa na mfalme. Tena bora Morogoro, Dodoma kuna vijiji niliona vijiji nyumba watu wamejenga na matofali ya kuchoma halafu juu wameegesha tu bati halafu juu ya bati wameweka matofali ili bati lisiezuliwe na upepo. Aisee, nilishangaa sana, Tabora kuna vijiji tumepita nikaona nyumba zimejengwa style kama nyumba za Kiafrika za nyasi ila tu zenyewe zimejengwa na bati kuanzia juu mpaka chini, zipo nyingi halafu zimekaa kama kambi za wakimbizi. Uzuri nilisafiri na treni, niliona kila kitu vizuri. Kutoka Dar to Kigoma kuna li ardhi likubwa tu limeachwa hamna hata mashamba, wala nini yani nchi kubwa ila hatujui kutumia ukubwa wetu. Nimefika Kigoma nako umasikini wa kutisha

Hata form 4 tulienda study tour Zanzibar, nako ni overrated. Ukitoa pale Stone Town, kuna maeneo ni mabaya. Mji umechoka mbaya, mabati yana kutu. Kuna sehemu Zenji ya masista inaitwa Machui ndo tulipata hostel za kulala sisi wanafunzi, yani hata internet shida, kubaya af ni dakika 30 tu kutoka Stone town. Pako kama Nachingwea. Network inasumbua, migomba mingi kama Bukoba yani pabaya tu.
Tulitoka Stone Town kwenda Nungwi, hapa kati yani nako ilikuwa ni umasikini mtupu. Nilichopenda Zanzibar ni beach ya Nungwi, bei ya vitu pale Darajani, na Forodhani wakati wa usiku kulikuwa na vyakula vya kutosha na watu wa kila race, ila walivyokuwa wanatuzungusha kwenye ma historical site huko nilikuwa naona mabaya tu. Hayavutii. Kamji kamejichokea kinoma

Hadi nimerudi mkoani kwetu Lindi, huku nako ni kubaya. Nyumba mbaya. Yani naona nchi yetu masikini tu kuanzia bara hadi visiwani

Hadi sasa mikoa ambayo sijafika ni Songwe, Rukwa, Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Labda mikoa hii itakuwa tofauti ila sijafika.

Lakini naona vita dhidi ya umasikini tumeishindwa kabisa. Nchi kubwa, resources nyingi ila inasikitisha. Tushukuru Mungu Bongo wananchi wake wavumilivu, wengi wanaonekana kuwa na furaha tu
Nawaza kwamba baina ya Ruangwa na nachingwea kuna maeneo mazuri sana kuanzisha kijiji mkiwa na watu kadhaa mnatafuta maeneo makubwa mnaweka mijengo ya maana na mifugo yote mnaanzisha kijiji chenu cha wastaarabu.

K
 
Sasa mpwapwa na kongwa dom huko ndani ndani kuna fursa gani hakuna umeme wala maji zaidi ya watu kuliwa funza bwashee?

Hapa umedanganya. Kongwa na Mpwapwa kumekua na umeme tangu ukoloni. Sema maeneo machache. Mpwapwa kuna madini pia. Majority ni wakulima na wafugaji lakini pia kuna taasisi za siku nyingi zimeajiri na kusomesha wengi e.g. Mpwapwa Sec, Mpwapwa Teachers College, Mpwapwa chuo cha mifugo, Kongwa Ranch, Kongwa Theological College. These institutions have existed since colonialism. Yes, barabara zao ni za vumbi karibu zote na majority ni masikini sana like most of Tanzania. But fursa zipo pia. Commercial farming is big in Kongwa. Kibaigwa ipo highway ya Dar Dom. Biashara inafanyika kwa wingi pale.
 
Iko hivyo boss. Hali inatisha. Ukitembelea mashule ya vijijini mwenye machozi ya kulia unaweza kulia. Hizo ofisi za gvnt ndo mtihani. Nyumba ni mtihani mwingine. Watu hawana magodoro wanalala chini. Mungu atusaidie!
Kilimo ndio dah mtu ana familia ya watu 5 ila analima kwa jembe la mkono
 
Back
Top Bottom