Ikulu watakubali kunipa kibarua nilichoomba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu watakubali kunipa kibarua nilichoomba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 5, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  MPENDWA msomaji, unafikiri Rais Jakaya Kikwete ana watu wanaomshauri juu ya mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa?

  Unafikiri wapo watu wanaomshauri kuhusu masuala ya kisiasa na kiuchumi?

  Kwa kuangalia mambo mbalimbali yanayoendelea leo nchini unaweza kuamini kuwa kuna watu wanalipwa mamilioni kumshauri rais? Kwa kupima yale yanayofanywa na serikali unaweza kufikiria kuwa ushauri unaotolewa kwa rais ni mzuri?

  Kama tukiweka kipimo cha uzuri na ubaya kati ya moja na kumi, moja ikiwa ni mbaya sana na kumi ni mzuri sana; utaupa namba gani ushauri anaopewa Kikwete kuhusu masuala mbalimbali ya nchi?

  Ukiniuliza mimi maswali hayo, jibu langu ni jepesi; yeyote anayemshauri rais leo hii angekuwa hana kazi siku ya kwanza alipofungua mdomo wake. Sitanii.

  Kuna mlolongo wa mambo ambayo yamefanywa na Ikulu ambayo kwa hakika yamenifanya nijihoji kama ninaota au nasinzia; mambo ambayo tukiyaangalia kwa karibu tutaona kuwa kuna mtu aidha hatoi ushauri mzuri au ushauri wake ni mbaya.

  Ni kwa sababu basi, nimeamua kujitolea kwa mara nyingi kuwa mshauri wa bure wa rais na naahidi kumshauri vizuri na kwa manufaa ya taifa tu.

  Sitampa ushauri wowote ule wa kumfanya aonekane mzuri au kufanya Ikulu ionekane vizuri. Nitampa ushauri ambao utamhakikishia mambo anayoyafanya na maamuzi anayochukua yote ni kwa masilahi ya taifa tu.

  Ushauri huo nitautoa kwa uwazi na ukweli lakini vile vile kwa usiri mkubwa. Naahidi sitatoa siri za ushauri ninaompa rais na hivyo kumhakikishia mazungumzo yetu yanabakia kifuani mwangu daima.

  Hivyo nimeamua kuomba kuwa mshauri wa bure wa rais. Ili kuonyesha kuwa ushauri wangu yawezekana ukawa ni bora kuliko ule uliotolewa hadi hivi nitatoa mifano michache ambayo ningemshauri rais tofauti na inavyoonekana alishauriwa hivi sasa.


  Kuhusu uamuzi wa Bunge juu ya Richmond
  Badala ya kumwachia waziri mkuu kuanzisha uchunguzi mwingine nje ya ule uliofanywa na Bunge, ningemshauri rais kuagiza kuwa uamuzi wote uliotolewa na Bunge uwe umetekelezwa ndani ya siku saba.

  Ningemshauri kuwa kwa vile Bunge ndilo lina jukumu la kuisimamia serikali, basi uamuzi wowote wa waziri mkuu au mtu mwingine kuanzisha uchunguzi mwingine wa jambo lililochunguzwa na kuamuliwa na Bunge utakuwa ni uvunjaji wa katiba na dharau kwa Bunge.

  Hivyo, ningemshauri rais kuwataka Johnson Mwanyika, Edward Hosea na wengine wote waliotakiwa kuwajibishwa kuwasilisha barua zao za kujiuzulu mara moja.

  Kama angesikiliza ushauri huo, hili suala la Richmond lingekuwa limemalizwa mwezi Machi mwaka jana. Hivyo, ushauri wangu kwa rais ungekuwa wa kutii kwa kutekeleza uamuzi wa Bunge bila kusita (without reservation).

  Kuhusu ufisadi Benki Kuu
  Kwa vile mimi ndiye ningekuwa mshauri mkuu wa rais, basi jambo la kwanza ambalo ningemshauri kuhusu Benki Kuu ni kuwasimamisha mara moja watumishi wote wa umma pale ripoti ya Deloitte & Touche ilipotoka na mapendekezo ya kuanzisha uchunguzi.

  Ningemshauri asipoteze muda kwa kuwavumilia, bali kufanya haraka na kwa wepesi uchunguzi huru na kuhakikisha wahusika wote wanashughulikiwa mara moja.

  Hivyo, nisingemshauri kuunda kamati nyingine, bali kumshauri amuagize Mwendesha Mashitaka Mkuu kuleta mashitaka kwa wahusika wote, akipata ushirikiano wa kipelelezi kutoka Idara ya Upelelezi (CID).

  Kwa vile suala la Benki Kuu ni nyeti na linahusu moyo hasa wa uchumi wa taifa letu, ningemshauri aialike taasisi kama Scotland Yard au SFO kuendesha uchunguzi wa suala zima la EPA na CIS na madudu mengine yote yanayodaiwa kuendelea Benki Kuu.

  Kwa kufanya hivyo, rais angeonekana ni mwamuzi asiyesita (decisive) na angeonyesha amelipa uzito unaostahili jambo hilo. Kama angenisikiliza, basi mambo yote ya Benki Kuu yangekuwa yamefikia mahali patamu leo hii.


  Kuhusu suala la Kagoda
  Kwa vile suala la Kagoda katika EPA linaonekana kuwatatiza watendaji, ningemshauri atumie kanuni ya "liwalo na liwe". Kwamba haiwezekani kampuni moja ichote sh bilioni 40 halafu watu waendelee kuremburiana macho na kutomasana huku wakicheka cheka.

  Ningemshauri kumwagiza Mwendesha Mashitaka kuleta mashitaka yanayostahili mara moja dhidi ya wale ambao tayari anajua wanahusika kwa namna moja au nyingine na suala la Kagoda.

  Kama Mwendesha Mashitaka angesema kuwa anaogopa kuwakamata wahusika kwa sababu wataitikisa nchi, basi ningemshauri rais amwajibishe mara moja na kumweka mtu ambaye yuko tayari kuitii sheria kwa gharama yoyote na si mawazo yake.

  Suala la Meremeta
  Kwanza ningemshauri Rais amwambie Waziri Mkuu asiwaongopee wananchi. Ningemshauri amwambie Waziri Mkuu afute kauli yake kuwa suala la Meremeta ni suala la ulinzi na kama angekataa basi ningemshauri rais amwondoe waziri mkuu na kuunda baraza jipya la mawaziri.

  Ningemshauri rais alihutubie taifa juu ya machafu ya Meremeta yaliyofanywa na utawala uliopita na kuliambia kuhusu uhusiano wa aibu ya serikali na watu ambao huko nyuma wamekuwa ni mamluki wa kivita kwenye machafuko ya Angola, Sierra Leone, DRC na Liberia.

  Ningemshauri rais awaambie wananchi kuwa suala la Meremeta ni la aibu na kuwa viongozi waliopita waliruhusu mamluki kutumia ardhi yetu kuchota utajiri wetu ili kufadhili shughuli zao haramu!

  Ningemshauri rais kuwaambia wananchi kuwa ule uwanja wa ndege ambao ulijengwa katika moja ya migodi yetu hapa nchini ulikuwa unatumika kwa shughuli za kusafirisha nje utajiri wetu kama watu hao hao walivyofanya huko Uganda.

  Hivyo, ningemshauri kufuta makubaliano yoyote kati ya Tanzania na watu hawa au makampuni yao mengine ambayo leo yamepewa maeneo mengine ya kutafuta mafuta na dhahabu. Hii, ningemwambia ingeirudishia Tanzania heshima yake inayostahili.

  Kuhusu Muungano
  Suala la Muungano nisingemshauri lolote kwani sidhani kama ana nia, uwezo au uthubutu wa kulishughulikia kwa jinsi ambavyo naamini ingeweza kuulinda Muungano wetu, kudumisha udugu na kuhakikisha kuwa Bara wanafurahi, Zanzibar wanafurahi na Watanzania wote wanafurahia, na wakati huo huo kila mmoja anajijua kuna kitu amepungukiwa lakini wanakubali upungufu huo kwani katika kupungukiwa kwao wanaweza kuona haja ya umoja wao.

  Kuhusu CCM

  Sasa kwa vile nitakuwa mshauri wa rais nadhani haitakuwa vibaya kumshauri pia kuhusu chama chake. Kwa sababu utawala ulioko madarakani unatokana na chama chake, basi nitamtendea hisani nikimshauri jambo moja kubwa, nalo ni kuitisha mkutano mkuu maalumu wa CCM ili wafukuzane uanachama.

  Kabla ya hapo, kwanza ningemshauri amshawishi Andrew Chenge, Rostam Aziz na wengine kujiuzulu nyadhifa zao. Tena, sasa hivi itakuwa vizuri kwani hakuna uchaguzi mdogo wowote unaoweza kufanyika hadi uchaguzi mkuu. Katika kufanya hivyo atajionyesha kuwa amekidhibiti chama na anaonyesha uongozi.


  Kuhusu washauri wake wa sasa
  Kwa jinsi walivyoboronga masuala mbalimbali, ningemshauri kabla hatujaenda mbali awatimue kwanza washauri wake wa sasa na wale wanaoitwa ‘wasemaji' wake. Kwa sababu kundi hilo linatia aibu katika fani nzima ya kuwa mzungumzaji wa ofisi ya juu kabisa nchini.

  Wakati mwingine nafikiria hawa jamaa wanafanya makusudi ili kumuaibisha Rais au wamelewa ving'ora vya pale Ikulu kiasi kwamba wanafikiri wanaweza kusema lolote kwa jina la rais!

  Nina mambo mengine mengi ya kuweza kumshauri. Najua kwa kufanya hivyo sasa tatizo litakuja, je, atakubali?
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mkuu,mimi ninaona kama inawezekana kabisa washauri wake wana fikra na mitizamo kama yako.
  ...........lakini hapo kila hoja naona kama ITAMUINGIZA KWENYE CHAIN HATA YEYE!ndio maana anasuasua
   
 3. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanaweza wakupatie kazi kwani inaonekana Kikwete anahitaji washauri wapya.
   
 4. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  MM, Ukiipata kazi hiyo utabadilika tu ..lol..kama ndugu yetu Salva.
  Ungemshauri nini kuhusu kilimo, mawasiliano na elimu ya juu?
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  hawawezi kukupatia kwasababu unavyoyaona mambo sivyo wanavyoona wao.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Mkuu wangu vipi tena kutaka kuwa mshauri wakati hujui JK alikuwa akicheza nafasi gani ktk team nzima ya maswala ulozungumza!..

  Hivi kweli ikiwa JK ndiye aliyefungisha magoli yote unataka yeye tena asimamie maswala ambayo yakitazamwa ktk video itaonekana wazi yeye ndio kajifunga!..Mkuu wangu huyo Balali na Meghji hawakuwa BoT na wizara ya fedha kwa bahati mbaya!.. Meremeta yeye ni mwanajeshi tena alikuwa wizara hiyo..anaelewa fika uzito wa jeshi letu kama hawakukatiwa kitu ktk uporoji ulioendelea wakati wa Mkapa. Anayajua madudu yote ya Mkapa na ndicho kilikuwa kitanzi (blackmail strategy) walichomnyongea Mkapa kukubali JK kusimama kama chaguo la chama CCM..
  JK hakufika alipofika kwa nguvu zake mkuu wangu na wala hakuna kiongozi aliyewahi kufanya hivyo dunia nzima. Wale walioweza kuyafanya unayoshauri wewe ni kina Hitler, Idd Amin, Saadam Hussein na wengineo wengi tu ambao mwisho wa safari wameonekana washenzi kuliko binadamu wote..
  JK ana kazi kubwa sana na haiwezi wala hakuna mshauri ambaye anaweza kumwambia kinyume kwani kama hujui chanzo cha kitu utaweza vipi kushauri against!..
  Nakuhakikishia kuwa, bora amekaa kimyaaa kuliko kufikiria hatua dhidi ya wachezaji wenzake kwani mfumo wa CCM, huyo JK ni captain tu wa team nzima sii owner wala team coach...

  Binafsi naamini kabisa JK kashauriwa mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua dhidi ya MAFISADI lakini kama ujuavyo he was in those ministries ambazo zimezua mengi yanayowekewa mashaka leo..He knows what happened, yawezekana mnamwona mjinga lakini nasema hivi wakuu zangu - JK sii mjinga hivyo!
   
  Last edited: Aug 6, 2009
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kikwete hawezi kukupa kibarua wewe kwasababu ataonekana hajui kitu; yeye anataka washauri wanaomsikiliza na wanaomuogopa na sio wale watakaomwambia ukweli. Washauri wake ni vijana wanaojifunza kazi kama wakina Mwinyimvua na January; wakimwambia kuwa GLOBAL ECONOMIC MELTDOWN HAITAITHIRI TANZANIA nae anakubali akijua dhahili kuwa nchi hii inategemea uchumi wa nchi zilizokumbwa na mtikisiko wa uchumi!!! Huyo ndio JAKAYA MRISHO KIKWETE mkulu!!
   
 8. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ushauri wako MKJJ ni very reactive. Yote uliyosema ni kama kujaribu kubadili the past. Yaani yote hayo ni "ANGE-paswa kufanya hivi....". Tunachotaka ni je afanye nini as from now on?

  Ushauri wangu ni kwamba kutokana na uongozi mzima wa CCM kuwa ndio umetuletea haya matatizo, na ndio uliomuweka yeye hapo alipo, na ndio kwa sasa unaomkwamisha kutekeleza ajenda zake za kusafisha ufisadi na kuondoa kero nyingi kama za muungano, nk. basi the best way ni kuhakikisha timu itakayoingia uongozini 2010 aiandae mwenyewe na kuhakikisha inakuwa ni mpya kabisa.

  Kutokana na mikakati yake mwenyewe ni kwamba uchaguzi ndani ya CCM unatayarishwa kuondoa vigogo mafisadi na wenye fedha za kumwaga. Yeye mwenyewe JK ndio anasimamia na kuzivalia njuga sera mpya za chama chake kuhusu chaguzi mbali mbali zijazo. Hakutakuwa na individual kampeni wala takrima, according to him. Wajumbe wote watatambulishwa na chama kwa kutumia resource za chama tu. Ni habari nzuri hii!

  Ukweli ni kwamba ikifanyika hivyo, kutakuwa na timu mpya ya uongozi na haitakuwa na kuogopana kwamba fulani siwezi kumgusa kwa sababu alinifadhili kwenye kampeni. Hapo kila kitu kuanzia bungeni, ndani ya chama na serikalini kitawezekana bila kuoneana aibu, kuogopana wala kusukumana.

  Hapo ndipo JK atakapochomokea kutoka katika makucha ya mafisadi waliomsaidia 2005. hatakuwa tena na sababu ya kusitasita kwingi kama ilivyo sasa.

  Otherwise ikishindikana tena, basi JK kwa msemo wa wachaga atapaswa akaogeshwe kwa magadi tu kwani atakuwa ana nuksi isiyosafishika.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,876
  Trophy Points: 280
  They know every right thing to do! if head has problem the whole body will respond to it!

  Kikwete ndie tatizo twende kulia twende kushoto, kama rais mzuri hata kama kuna mawaziri wanapwaya anawabeba!

  kazi watakupa, lakini you are in best position now! you say and write what you believe that what makes you!

   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kufikiri kwamba Kikwete anakosa ushauri, na kwamba hili jambo ndilo linaleta matatizo yetu, ni kukosa kuielewa picha nzima ya jinsi mambo yanavyoendelea Tanzania.

  Kikwete ana / ana access na better information pengine kuliko mtu yeyote Tanzania.Tatizo hana nia wala uwezo wa kutatua matatizo yetu.
   
 11. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mzee naamini ushauri wako ni mzuri lakini kulingana na wanaJF waliochangia hapo juu JK inawezekana anashauriwa vizuri lakini anashindwa kufanya kitu kwa sababu naye alihusika kwenye baadhi ya michezo hiyo michafu iliyomwezesha kuingia ikulu. Hata hivyo naomba uendelee kutoa ushauri wako wa bure kutumia vyombo vya habari hasa kona hii hapa JF. Thanks a lot for knowing that you are a Tanzanian. Keep on Babu.
   
 12. T

  Tom JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wamecheza na chama chao mpaka wamefika mahala pabaya ambapo haiwezekani tena kurekebisha mambo.
  JK anao washauri na yanayoendelea anayaona na ameshiriki, tunayoyalalamikia ni matokeo tu ya mchezo wa CCM ambao wanategemea kueendeleza.
  JK hahitaji ushauri, dawa ni kuing'oa CCM.
   
 13. M

  MC JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  MM

  System imechafuka kupita kiasi, Ukishaingia kwenye hiyo System, unakuwa kama umelogwa, whether you like it or not!
  Yale unayopenda kusema/hayo uliyosema hutayasema kule.!
   
 14. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji;

  Mzee mwenzangu, AMINI AMINI nakwambia JK is smarter than that!

  JK ni sehemu ya tatizo kwahiyo hawezi kuwa sehemu ya suluhisho!
   
 15. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  MKJJ,
  Atawezaje midamu yeye siye aliyewaandaa. Yahitaji ujasiri wa kipekee kujichinja kwa msomeno. Yote hayo uliyosema ingewezekana kama asingekuwa anafungamana nao au washikaji wao. Kwa wawindaji, wanafahamu pindi myama anasapo kwenye mtego (awe simba, fisi n.k) japo wana meno, lakini wote walishindwa kung'ata sehemu ya mguu uliovunjwa na mtego ili kunusuru maisha.

  Watu wenye kuweza kufanya haya ni wachache, lakini hapa mhh.. tubaki tu kuwa "he is firm on issues" It is almost 5 yrs now, but we haven't seen yet!
   
 16. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  Naona Mkuu hujasoma ukaelewa post ya MJJ. Alichosema ni nini cha kumshauri sasa hasa baada ya huo uozo kutokea. Wewe ulitaka aseme basi tushauriane na mafisadi walau warudishe kidogo. Ndicho unachotaka?

  MKJJ, kama kawaida very good thread. Inawezekana hii makala ikawekwa ktk one or two news papers za nyumbani? Naona inaweza kumsaidia huyu bwana mkubwa katika kupanua wigo yake ya kufikiri. Or is there an email that can be sent to the president directly and then you email this stuff to him moja kwa moja. Najua wengi mtasema hataishughulikia but at least kimsaidia kupanua ufikiri wake.

  So sad that our system imeharibika to the extent that it needs to be designed upya.
   
 17. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nashangaa ni wa TZ wangapi wanaona hayo uliyoshauri?Kama wangeona nakuhakikishia pasingekalika kwa CCM 2010.Looh ni usingizi kiasi gani tumelala hata kutambua kuwa Mkuu wetu wa Kaya anatupeleka kusiko? Hebu fikiria madude yote ya kashfa katika awamu hii kwingineko duniani angeshabwaga manyanga kitambooo! Lakini hapa kwetu ndo kwanza tunasema hakuna wa kumpinga katika uchaguzi ujao.
  MM ushauri wako ni wa kina lakini hauna nafasi katika mazingira ya uongozi wa sasa.Vema tu ujikalie kimya na jembe lako ukiwaangaza watanzania kwa hoja na changamoto kibao za maisha yao ya kila siku.Huko juu hakuna wa kukusikia.Hata na hiyo kazi ya ushauri wa bure pls katoe kwa wakulima kule Idodi huko watakuelewa siyo JK.
   
 18. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mwanakijiji, kusudio la kumshauri Rais katika masuala mbalimbali yaliyotokea na kuharibu heshima ya nchi yetu ni jambo zuri. Ila ninavyojua ni kwamba hakuna ulilolisema ambalo halijulikani kwa serikali tena kwa mapana zaidi ya ulivyoyaainisha. Yote hayo na mengine mengi ambayo hukuyasema, yanafahamika kwa vyema serikalini. Kinachokosekana ni nia thabiti ya kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Hiyo linaweza kusababishwa na mambo mengi yakiwemo ya kisiasa, usalama wa Taifa na kadhalika. Yanaweza kuwa ni uoga usio na sababu.

  Mkuu, Serikali imekuwa ikifanya mambo mengi (ya aibu) ambayo yalikuwa hayawekwi hadharani kwa miaka mingi sana. Mambo ambayo kama yangewekwa hadharani, hadithi hizi zingekuwa zimezoeleka, ama zimeichafua nchi miaka mingi iliyopita. Serikali inaweza ikawa imepotoka kuyaweka mambo hayo hadharani wakati huu, au vile vile inaweza ikawa imefanya vyema, ili kukomesha tabia hizo za kiutendaji ndani ya serikali. Yote hayo yanategemea juhudi zinazochukuliwa kufikia azma inayokusudiwa.
   
 19. Jumboplate

  Jumboplate Senior Member

  #19
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwanza kabisa naomba nimuunge mkono Nurujamii kwa mawazo yake. Kama vitu havikufanyika vizuri huko nyuma na sasa kwa sababu ya "wanamtandao" basi kuanzia 2010 awe na timu mpya isiyohitaji shukrani kwa kumweka madarakani.
  Lakini naona mimi binafsi napingana mambo mengi na Mzee Mwanajamii katika ushauri wake kwa JK. Kwanza kuwaondoa Manyika na Hosea sio suluhisho la matatizo katika idara au taasisi zao. Kwa hapa ntamwongelea Hosea; tokea enzi za anti corruption squad haijawahi kutokea taasisi hii ikawa na nguvu kuliko sasa, namaanisha human resource, sheria nzuri na usimamiaji wa sheria hizo. Jaribu kufika wilayani uone kesi za rushwa zinavyoongezeka mahakamani, najua hapa mtasema ni dagaa lakini kwa wilayani mkuu wa idara anapofikishwa mahakamani ni kesi kubwa kiwilaya. Na hata kitaifa kesi kubwa zinazochunguzwa na zilizopo mahakamani ni nyingi kuliko kipindi kingine chochote. Nakumbuka Hosea kabla hajawa mkurugenzi mkuu nilishawahi kusoma magazetini aki'advocate kwa sheria mpya, (na alikuwa akitamka tokea zamani kuwa takrima ni rushwa)nadhani ameipigania mpaka imepatikana lakini hakuna anayeona hili.
  Pili ni suala la Kagoda: DPP ameshazungumzia kuhusu suala hili. Anajua taifa zima linaliangalia kwa makini. Sasa iwapo utaamua kuwafikisha mahakamani waliotumwa kuchukua fedha husika na kuwaacha mapapa waliocheza dili zima then imani ya wananchi kwa serikali yao lazima itapotea. Sasa basi anapoamua kufanya uchunguzi zaidi ili kujiridhisha kuwa mapapa waliohusikana wizi huo wanashtakiwa sisi tunaanza kulalamika, na pia akifikisha mahakamani dagaa tunalalamika, I think its not fair to him. Tumpe muda ili atakapoleta dagaa tuweze kumkosoa vizuri...
  Tatu ni suala la kutimuana CCM: mi naamini kufukuzana sio suluhisho ila kama angesema kuvuana uongozi ningemwelewa. Kumbuka Chenge na Rostam hawajashtakiwa katika mahakama yoyote mpaka sasa, everybody is innocent until proven otherwise. Sasa leo unaamua kuwafukuza hao wawili halafu kesho wewe unazushiwa maneno kama hayo utataka utimuliwe??
  Mwisho kabisa ningependa nikumbushe usemi wa JK wakati anaingia madarakani kuwa atavipa mamlaka na vitendea kazi zaidi vyombo vya dola na kuwa kamwe HATAVIINGILIA katika utendaji wao wa kazi. Kama tunamlaumu sasa basi tulipaswa kumlaumu tokea awali alipotamka maneno hayo.
   
 20. M

  Magehema JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  The big problem with Politicians is that they NEVER "walk the talk".
   
Loading...