Salaam Watanzania,
Nathani kuna thred nyingi sana za Mh.Lowassa toka atoke CCM na hata wakati wa uchaguzi ndani ya chama cha ccm.
Lakini kwa ufupi ningependa kuongelea ni jinsi gani ujasiri wa lowassa uliyoadimu kwetu watanzania na hasa sisi vijana kwa taifa la leo.
Asikudanganye mtu,maamuzi ya leo ndio matokeo ya kesho.Uamuzi wa lowassa uliwacha wanasiasa wengi midomo wazi na hasa watanzania kwa udhubutu wake kuondoka ndani ya chama alichokuwa kwa zaidi ya miaka 30.Huu hata mimi leo naamini haukuwa uwamuzi wa haraka na wala wa kukurupuka.Lakini pamoja na lowassa kutoka CCM kwa jambo lolote lile,uthubutu wake unatisha na unatia moyo kwamba watanzania wote tunaweza kuthubutu na kuamua maamuzi magumu.Lowassa ameonyesha kwamba inawezeka.CCM huwa wana maneno yao kwamba bila CCM,nchi itayumba;hii ni thana potofu na isiyo na ukweli wa nusu.
Kwa mantiki hiyo basi,mimi binafsi namwona Lowassa kama my hero.Vijana wenzangu tunahitaji kufanya maamuzi magumu kama mzee lowassa aliyofanya.Potelea pote hata asipoingia ikulu,lakini alifanya maamuzi na kuamua kwamba hii inatosha.
Nchi yetu inapaswa kuwa mbali sana.Masuala ya maji na nishati sio mambo ambayo kama Tanzania ingekuwa na viongozi makini isingekuwa mahali hapa.Nasi tunapaswa kufanya maamuzi magumu.Tanzania ni ya watanzania wote bila kujali dini,kabila wa rangi.Tusiwe wepesi kuogopeshwa na maneno ya akili ndogo,watu wenye kutaka kuhothi uongozi wa nchi kwa maslahi yao binafsi huku sisi tulio wengi tukiteseka.
namaliza nikiomba watanzania tufanye maamuzi magumu sasa.Hakuna kurudi nyuma.Kwa miaka 50,CCM haijafanya chochote.Tuangalie kenya,walithani kwamba hakuna chama kingine kinachoweza kuleta maendeleo zaidi ya KANU.leo kanu ipo wapi??
Heko mzee lowassa.
Dalili zote zinaonyesha mkamio uliopo Kwenye kambi kuu za vyama vwili ccm na cdm < ukawa ni kiini macho tu> ni kuwa ktk uchaguzi wa mwaka huu kupita mingine yote, kiu ya kuingia ikulu ni kubwa, hii inatokana na kuwa nchi iko kwenye mazingira mazuri kiuchumi kuliko wakati mwingine wowote kwakua karibuni nchi inategemea kuingia kweye utajiri wa mafuta na gesi, kwa hali hiyo mosi,
ccm ni kufa na kupona ku consolidate power, siamini wataacha nchi kwa urahisi hivyo, hiyo inapaswa kuzingatiwa sio kitu cha kupuuzia. Hata ningekua mimi nisingekubali, nihangaike kutafuta halafu nije ni waachie wengine wavune!!Ni wachache wenye ubavu huo, <omar bongo, Dos santos na obien nguema ni mifano hai, hawatoki ngo!! Nchi zao tajiri wa mafuta >na
Pili, iwe iweje Lowasa nae kwa mwendo wake huu wa fisi mlafi na jinsi alivyo ukamia ukuu ni wazi kuwa kaona pesaaa!!! mhemko wote huu wa kuhangaika usiku kucha mashariki na magharibi na maswahiba zake ni kwa kuwa wanajua kuna harufu ya pesa !! na wanaitaka kwa udi na uvumba, pili anataka pia kulipiza visasi, majibu yake ya hasira ni kielelezo tosha,
kwa ccm usalama wao kwa huyu jamaa ni ndogo sana pindi itokeapo kushinda, hiyo nayo inaongeza msumari wa kufa na kupona kubakiza nchi mikononi mwao, Cdm nayo inamilikiwa na wafanya biashara kwa hiyo nao wameshanusa harufu ya pesa, ndio maana wameziba masikio pua na vinywa ili kumyaka mmasai, wao wenyewe walimnanga fisadi, ni ile kiu yao ya lazima ikulu iingiwe kwa njia yoyote! Funika kombe mwanaharamu apite!
wanajua iwapo wataingia ikulu matarajii yao ya kuvuna, njia nyeupeeee!! itakua within their reach hivyo msishangae kufunga macho na masikio na huku wakiwadanganya wapiga kura wao kwa visababu vya kipuuzi, ni kuhakikisha kwa hali, mali na hila wanaingia ikulu, hapo ndio watanzania wata lijua jiji, nawaomba wa TZ kupima kwa weledi hapo october nani anastahili kuingia ikulu, zimwi ulijualo au jini ndani ya chupa!! Kazi kwenu...