Ikulu si pango la majambazi na wezi

Ikulu si pango la majambazi na wezi

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,961
Kamwe huwezi ukasafisha haja kubwa ikawa safi hata ufanye nini. Kiwango cha kufika mpaka wakuu wa vyama kuhongwa na kuhongeka hii ni hatari sana.

Kuna mambo mengi ambayo tunashindwa kuyadadavua kwa umakini sana na kuyachukulia kiushabiki tu. Eti tukiwa na lengo lakung'oa chama fulani wakati hatujui hatima yetu itakuwa ni nini. Tunasema tumg'oe kwanza huyu halafu baadae tutaona cha kufanya. Ni ujinga uliopita mipaka na kuwafanya watanzania kama hamnazo.

Siasa za namna hii zinalifanya taifa letu lizidi kudidimia. Vyama vina maprofessa, na watu wenye elimu ya hali yajuu kabisa wanashindwa kuleta dira na kuanza kuwa na cheap politics. Kuwahadaa wananchi kwa lengo lao tu. Mtu alishachafuka tangu miaka ya 90 na nyie wenyewe mnalijua kabisa. Lengo lenu ni nini katika nchi hii? kamwe hamfai na hakika mtakaa kusubiri meli stand ya basi.

Sio kwamba hatuoni nyendo zenu, hakika tunaona. Mwizi na jambazi sugu akabidhiwe nchi je atawalipa nini wafadhili wake waliompa pesa na kuweza kuwahonga viongozi wa vyama vya siasa? Huyu lazima analengo baya sana na nchi yetu.

Watanzania tusimame kwa pamoja tuwakatae hawa wezi. Unajijua wewe ni mchafu na umechafuka kwani ni wewe tu unayeweza kuwa kiongozi wa nchi hii? Unalengo gani na Tanzania? Unajinadi wewe ni mtu wa mungu!! wewe wewe wewe jichunguze usiwadangaye wananchi. eti unasema wewe prezidaa mmetoka mbali, aibu sana. Hutakiwi kuwa kiongozi wa tanzania wewe kaa utulie upate penshen yako kwa faida yako na kizazi chako.

Tukutane na wewe 25 october 2015 utauona moto wetu. Isitoshe report ya uchunguzi ipo tayari
 
Annael

Hapa umesema ukweli mkuu "Tunasema tumg'oe kwanza huyu halafu baadae tutaona cha kufanya. Ni ujinga uliopita mipaka na kuwafanya watanzania kama hamnazo".
 
Last edited by a moderator:
Tutakuwa na Voting baada ya hapo tutakuwa na vetting.
 
Ikumbukwe waziri mkuu ni mtendaji mkuu wa serikali. Kuifanya nchi ikaingia hasara kubwa na kuudanganya umma kuwa Richmond ni kampuni halali ni wizi uliopita kiasi. Leo hii unakana utendaji wako wa kazi na kutuletea cheap politics.
1. Je hukujua majukumu ya waziri mkuu?
2. Kwanini ulijiuzulu?
3. Wale rafiki zako wanaokufadhili ni akina nani?
4. Kwanini unataka uraisi kwa nguvu hivyo?
5. Kwani lazima wewe tu uwe raisi?
 
Annael

Miaka yote hiyo mbona hamjamshitaki mahakamani?Povu jiiiiingi utadhani unaongea la maana.Mmeshaambiwa mwenye ushahidi aende mahakamani,wewe umekaa mbele ya computer unahororojoa badala ya kwenda kumshitaki mahakamani.
 
Last edited by a moderator:
Miaka yote hiyo mbona hamjamshitaki mahakamani?Povu jiiiiingi utadhani unaongea la maana.Mmeshaambiwa mwenye ushahidi aende mahakamani,wewe umekaa mbele ya computer unahororojoa badala ya kwenda kumshitaki mahakamani.
Uchunguzi ulikuwa haujakamilika umekamilika sasa mda wowote atatakiwa mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi wa nchi.
 
Annael

Ujumbe huu mwanana umeujua lini? Katika mazingira gani? Je reference yako ni kwa nani? Nakuhurumia kwa sababu inaonekana hujajipanga kwa vile umeshakuwa nje ya wakati na matukio yameshakupita. Mwl. Nyerere aliwahi kusema ili tuendelee tunahitaji vitu vinne yaani "Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi bora" Je ni nini kinachokosekana tangu tujipatie Uhuru zaidi ya miaka 54 ilopita?
 
Last edited by a moderator:
Uchunguzi ulikuwa haujakamilika umekamilika sasa mda wowote atatakiwa mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi wa nchi.

Na hivi amehama chama mtatafuta ushahidi wa uongo kwa kila namna ili mummalize kabsa..anzeni kwanza na hao walipo madarakan kwa kuwachunguza na kuwashtaki ndio mmalize na mzee wa maamuz magumu

R.I.P CCM
 
ujumbe huu mwanana umeujua lini? Katika mazingira gani? Je reference yako ni kwa nani? Nakuhurumia kwa sababu inaonekana hujajipanga kwa vile umeshakuwa nje ya wakati na matukio yameshakupita. Mwl. Nyerere aliwahi kusema ili tuendelee tunahitaji vitu vinne yaani "watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora" je ni nini kinachokosekana tangu tujipatie uhuru zaidi ya miaka 54 ilopita?
ikulu sio pango la wezi. Kaa ukijua hilo. Na mtu anaye taka kwenda ikulu kwa namna yoyote tumuepuke kama ukoma. Huyu ni mwizi na jambazi kamwe hawezi kuwa safi.
 
Uchunguzi ulikuwa haujakamilika umekamilika sasa mda wowote atatakiwa mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi wa nchi.

Dk mwakyembe alisema hivi "hatuwezi kuzungumza mambo yote tuliyoyagundua maana serikali ingeanguka hivyo tunamuomba waziri mkuu ajipime aamue" hiyo mahakama ijiandae kumtia jela jakaya kama kweli upelelezi umekamilika.
 
Katika hali ya kawaida alipaswa kuitetea hoja yake na kitendo cha kujiuzulu haikuwa solution ya tatizo. Alipaswa kutetea taifa dhidi ya hasara itakayoingia. Je alikuwa hajui wajibu wake kama PM. Kwa sisi wanasheria huwa tunapenda kuwa na msimamo hata kama umefanya kosa. Ujue utu uzima si umri. Mm ndo mana huwa sipendi siasa za bongo. Ujinga wetu ndo umasikini wetu.Naipenda nchi yangu,Magufuli kiutendaji anafaa sana. Kwa kauli yake nyepesi ameiabisha nchi na chama pia.
 
na hivi amehama chama mtatafuta ushahidi wa uongo kwa kila namna ili mummalize kabsa..anzeni kwanza na hao walipo madarakan kwa kuwachunguza na kuwashtaki ndio mmalize na mzee wa maamuz magumu

r.i.p ccm

uchunguzi upo tayari na mda wowote tu la mgambo litalia.
 
Annael

Escrow imepigiwa mjengoni humohumo.
Unajifanya hujui.
 
Last edited by a moderator:
Ikumbukwe waziri mkuu ni mtendaji mkuu wa serikali. Kuifanya nchi ikaingia hasara kubwa na kuudanganya umma kuwa Richmond ni kampuni halali ni wizi uliopita kiasi. Leo hii unakana utendaji wako wa kazi na kutuletea cheap politics.
1. Je hukujua majukumu ya waziri mkuu?
2. Kwanini ulijiuzulu?
3. Wale rafiki zako wanaokufadhili ni akina nani?
4. Kwanini unataka uraisi kwa nguvu hivyo?
5. Kwani lazima wewe tu uwe raisi?

Kojoa ukalale huna hoja,
Chopa zipo 8
Magari 300
Na safu imekaa vyema kabisa, na wizi wenu wa kula mwaka huu hamtaweza maana lowasa ndo mwenyekiti wa kamati yenu ya ulinzi.
Viva ukawa.
 
ikulu sio pango la wezi. Kaa ukijua hilo. Na mtu anaye taka kwenda ikulu kwa namna yoyote tumuepuke kama ukoma. Huyu ni mwizi na jambazi kamwe hawezi kuwa safi.

Je mahali ulipo hakuna vituo vya Polisi,Polisi Jamii, Mahakama au mawakili utusaidie kumshitaki huyo uliyekwisha mtambua? Maana unaonekana wewe unao ushahidi mujarabu na mkereketwa wa kweli na mpenzi wa nchi hii.
 
Dk mwakyembe alisema hivi "hatuwezi kuzungumza mambo yote tuliyoyagundua maana serikali ingeanguka hivyo tunamuomba waziri mkuu ajipime aamue" hiyo mahakama ijiandae kumtia jela jakaya kama kweli upelelezi umekamilika.
Mtendaji mkuu na msimamizi wa mambo katika serikali ni waziri mkuu. Panga hili lazima linagonga kichwani kwa aliyekuwa waziri mkuu wakati ule na akaliingizia taifa hasara kubwa.
 
Back
Top Bottom