Hivi mbona CCM wako kimya mpaka sasa?

Hivi mbona CCM wako kimya mpaka sasa?

Tokea siku ya Jumatatu pale ambapo makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba walipewa taarifa za mhshimiwa Lowasa kuhama chama na kutimkia UKAWA.

Kwa kuwa vijana wa masuala ya propaganda chini ya katibu mwenezi Nape Mnauye walidhani ulikuwa utani au masihara wakapuuzia onyo hilo sasa imekuwa ngumu kutoa taarifa ya kupokea uamuzi huo.

Katika ulimweigu wa sasa wanasiasa nao wakiwa kama binadamu wengine nao wana utashi na moja ya matunda ya utashi huo ni kuweza kufanyamaamuzi na kuyatakeleza.

Pia katika nchi mbalimbali duniani vyma vya siasa vinakuwa na washauri wao ambao moja ya kazi zao ni kujaribu kuoanisha taarifa zinazopishana kuhusu sera, itikadi na suala Zima la mbinu na mikakati.

Lakini Chama cha Mapinduzi wamekuwa kimya hata baada ya kuona kwenye mitandao kwamba Tumaini Makene, mkuu G Sam na wengine walikuwa wakifanya kazi usiku na mchana, na Nape Nnauye akawa hajajiandaa angalu kujibu uamuzi huo wa mzee Lowasa kuhama CCM.

CCM si chama lelemama na kipo kinatawala nchi hii tangia ilipokuwa TAA, TANU hadi CCM ilozaliwa tarehe 5 mwezi wa 7 mwaka 1977.

CCM mtaa wa Lumumba vipi mmekaa kimya au Nape Nnauye bado ametahayari?

CCM mtaa wa Lumumba isiwaache vijana wasofahamu siasa kuja jamii forums kujaza taarifa za kizushi kuhusu UKAWA na Dr Slaa, au mjinga mmoja anakuja na kichwa cha habari kinachosema Dr Slaa is dead!.

"Spin Doctors" wa CCM wapo wapi?
 
Siasa za Tanzania ni ngumu sana, unaweza kushangaa kibao kikawageukia UKAWA ghafla na wao wakawa mabubu kama LUMUMBA hivi sasa.
 
kumekua na tatizo ama mpango ovu unaendeleaje nchini mpaka leo hii.tatizo lilikuepo lakini sio kwa kiasi hiki kwani limeongezeka mnoo tangu siku mh EL alipotangaza rasmi kuhamia upinzani hivyo kwa mamlaka waliyonayo shirika la umeme tanesco sijui wanafanya kwa makusudi ili kuzuia mafuriko ya mabadiriko kama wale wa chamwino ama ni kinyume na hapo.
hili suala la kuleta umeme usiku wa manane na kuukata asubuhi mapema usio na tija binafsi unaniumiza kiasi kukata tamaa na CCM kwani kitendo hicho hakimgharimu mtu binafsi alie ukawa Bali ni kwa watanzania kwa ujumla wao.
hivyo chukua hatua sahihi Oct 25.
nawasilisha
 
Salaam Watanzania,

Nathani kuna thred nyingi sana za Mh.Lowassa toka atoke CCM na hata wakati wa uchaguzi ndani ya chama cha ccm.
Lakini kwa ufupi ningependa kuongelea ni jinsi gani ujasiri wa lowassa uliyoadimu kwetu watanzania na hasa sisi vijana kwa taifa la leo.

Asikudanganye mtu,maamuzi ya leo ndio matokeo ya kesho.Uamuzi wa lowassa uliwacha wanasiasa wengi midomo wazi na hasa watanzania kwa udhubutu wake kuondoka ndani ya chama alichokuwa kwa zaidi ya miaka 30.Huu hata mimi leo naamini haukuwa uwamuzi wa haraka na wala wa kukurupuka.Lakini pamoja na lowassa kutoka CCM kwa jambo lolote lile,uthubutu wake unatisha na unatia moyo kwamba watanzania wote tunaweza kuthubutu na kuamua maamuzi magumu.Lowassa ameonyesha kwamba inawezeka.CCM huwa wana maneno yao kwamba bila CCM,nchi itayumba;hii ni thana potofu na isiyo na ukweli wa nusu.

Kwa mantiki hiyo basi,mimi binafsi namwona Lowassa kama my hero.Vijana wenzangu tunahitaji kufanya maamuzi magumu kama mzee lowassa aliyofanya.Potelea pote hata asipoingia ikulu,lakini alifanya maamuzi na kuamua kwamba hii inatosha.
Nchi yetu inapaswa kuwa mbali sana.Masuala ya maji na nishati sio mambo ambayo kama Tanzania ingekuwa na viongozi makini isingekuwa mahali hapa.Nasi tunapaswa kufanya maamuzi magumu.Tanzania ni ya watanzania wote bila kujali dini,kabila wa rangi.Tusiwe wepesi kuogopeshwa na maneno ya akili ndogo,watu wenye kutaka kuhothi uongozi wa nchi kwa maslahi yao binafsi huku sisi tulio wengi tukiteseka.

namaliza nikiomba watanzania tufanye maamuzi magumu sasa.Hakuna kurudi nyuma.Kwa miaka 50,CCM haijafanya chochote.Tuangalie kenya,walithani kwamba hakuna chama kingine kinachoweza kuleta maendeleo zaidi ya KANU.leo kanu ipo wapi??

Heko mzee lowassa.
 
kumekua na tatizo ama mpango ovu unaendeleaje nchini mpaka leo hii.tatizo lilikuepo lakini sio kwa kiasi hiki kwani limeongezeka mnoo tangu siku mh EL alipotangaza rasmi kuhamia upinzani hivyo kwa mamlaka waliyonayo shirika la umeme tanesco sijui wanafanya kwa makusudi ili kuzuia mafuriko ya mabadiriko kama wale wa chamwino ama ni kinyume na hapo.
hili suala la kuleta umeme usiku wa manane na kuukata asubuhi mapema usio na tija binafsi unaniumiza kiasi kukata tamaa na CCM kwani kitendo hicho hakimgharimu mtu binafsi alie ukawa Bali ni kwa watanzania kwa ujumla wao.
hivyo chukua hatua sahihi Oct 25.
nawasilisha

CCM ni lazima ing'oke.
 
Lowassa kama mwanasiasa amefuata mkumbo wa wanasiasa mufilisi waliomtangulia kwa kufanya maamuzi mabovu, ambayo hayakushirikisha ubongo wake vizuri. Maamuzi haya hayakuwa na hesabu zozote za kisiasa zaidi ya hasira na matamanio ya madaraka. Wanasiasa hawa wanaongozwa na mzee wa kiraracha. Hivo basi asitafute mchawi, kwani amejibaka mwenyewe kisiasa na sasa advantage ni ya Magufuli.
Eti kwa kukatwa tu na chama chake, chama ambacho amekuwa nacho tangu 1977 na amefanya nacho maovu na mazuri mengi tu, leo ndio anaona umuhimu wa ‘kujump ship’? Lowassa huyo huyo alikuwa party katika kuwakata wengi tu, kama vile Malecela, Mwandosya na kadhalika, leo ndio anaona demokrasia imekwaza kwake? Lowassa angekuwa shujaaa wangu kama angeondoka CCM kabla jina lake halijakatwa. Lakini sasa, hata mazombie wapindishe vipi, kwake ni kusaka URAIS kwa hali yoyote na kwa namna yoyote.

Tuwe wakweli wanamazombie, siasa za Tanzania sio kama siasa za nchi nyingine yoyote ya Africa. Wanaofananisha siasa zetu na Zambia, Malawi, Kenya na kadhalika wanapotoka. Demographic na voting patterns za siasa za Tanzania ziko tofauti sana na wenzetu. Siasa zetu ni za chama sio mtu. CCM iko very strong kwenye grassroot, na katika sehemu nyingi huko, watakipigia kura chama na sio mtu. TAKE THIS TO THE BANK. Lowassa ushabiki wake ni kwenye mitandao na mijini, tena kwa kutoa hela na kusomba watu kwenye malori ili waje kumshabikia (kama tutavyoona leo atakapoenda kuchukua form pale mtaa wa Ufipa). Nawapiga kura wengi wamjini ni MASHAROBARO. Akifika kwenye kituo cha kupigia kura na akakuta watu wengi, huyo anaishia zake. Huko kwingine hawafanyi hivo, wanangoja kupiga kura mpaka lala salama. Boda boda wengi si wapiga kura. Kaulize wangapi wamejiandikisha….utashangaa. Let us refuse to be a country of speculators and constant gossipers. Mazombie wanatulazimisha tuwe watu wakuspeculate tuuuu.

Lowassa umejibaka mwenyewe baba yangu. GAME OVER.
 
daaaa mm kila siku nikufika nifoleniiii tuuu mara ya mwiaho jana nikajiona nimelamba dume maana nilijihimu vilivyo na kweli nikawa mtu wa 5.daaa jamaa wakafika kutugawia namba walivyoanza mchakato wakasema wanamalizia watu wa jana duuuuu.kilichotokea mpaka saa 11 bado wajana hawajaisha tuu.
 
Tatizo walijua wamewafubaza watanzania kwa kuwang'oa kucha baadhi yao hivyo watu wangeendelea kuwa mabubu milele bila kuwatoa kasoro zao, sasa kibao kimegeuka mabubu wanasema tena wanatiririka haswa hawaogopi tena sasa watang'oa kucha wangapi? Makombora yanarushwa ccm mpaka lumbumba wanajificha uvunguni nape anatoa waraka bila kuweka sign ili baadae aseme si mimi bado sana wata nyooka tu.
 
mkuuu wewe jidanganye tuu hakuna kazi nzuri ambayo chadema wameifanya kama ya kuhamasisha vijana aiseee.ukitaka kulijua hili kama ulishiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakuwa ushajua nn na maanisha.

na kama utakuwa umetembelea kwenye vituo vya kupigia kura hakika pia utakuwa ushapata jibu.

vijana wana mwamko sana siku hizi.
 
Mimi na familia yangu tutampigia kura Lowasaa panapo majaliwa October 25
 
Magufuli ni msanii wa nyimbo za asili na ana nyimbo mbili tu; Alenselema na Sitawaangusha. Prof.Mwandosya amesema Magufuli hajawahi kuwa hata kiongozi wa chama ngazi ya tawi.Ni mgombea pandikizi la waliomtangulia hivyo anaenda kulinda maslahi yao na siyo kuwatumikia wananchi.
 
Richard,
Binafsi katika mambo ambayo siku nyingi nilijua yanakipeleka kuzimu CCM ni kufa kwa idara ya Propaganda,au kukua kwa Propaganda machine ya Chadema,kiasi kwamba ika-counter ile ya CCM. Maana miaka ya nyuma CCM walikuwa wanaweza kuaminisha uma kuwa Majambia haya yenye rangi nyekundu ni na blue ni ya CUF,au Chadema ni chama cha dola ya KIchaga,na Ikaaminika..na wananchi wakakipigia ccm kula,ikawa jioni,aikawa asubuhi,miaka mitano ,kumi,...adfinitum!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom