#COVID19 Ikulu, Dar: Tanzania na Kenya zakubaliana kushirikiana katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tanzania na Kenya zimekubaliana masuala mbalimbali ikiwemo kuimarisha Mpaka, kushirikiana katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona na kushirikiana kwenye Sekta ya Utalii.

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza hayo Ikulu Dar es Salaam baada ya Utiaji Saini wa Hati za Makubaliano na Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Kenya.

Kwa upande wake, Rais Uhuru Kenyatta amesema Mataifa ya Afrika Mashariki yakiweza kuimarisha Umoja na Biashara, italeta manufaa makubwa kwa Wananchi wa pande zote.

5D1E5D7F-6494-4978-9A80-7030EA17EC82.jpeg
D51EDD1C-E463-4C5F-94CF-B2D8194ADDA3.jpeg
64CDED80-0585-4B3B-9B01-C27D6E6C8577.jpeg
 
Sisi ni wamoja ila kuna watu walitaka kutugawa kipindi fulani kwa kujifanya wapo na uhuru na kumtenga Odinga kisa ni rafiki ya hayati Magufuli shujaa wa Africa!
 
kuhusu ugaidi lazima Uhuru kakataa kwamba tutakua waongo tukisema tushirikiane ,labda ingea sudani ,Somalia Hilo tungekubaliana
 
Wakenya wajanja sana, Magufuri hakuwa kichaaa kuwapiga Vita, kwa nini asipige Vita Nchi zingine na iwe ni Kenya pekee? Hawa Jamaaa mkiwachekea mtalia
 
Kenya ni jirani tena ni ndugu hasa,
Yaani humo mipakani watu wameoleana sana,
Kuna watu walitaka kufuta historia hii
Ila ikashindikana asante sana mwenyezimungu,
Ninachoshauri tu serikali ziruhusu uraia pacha kwa inchi hizi mbili, kwani kuna watu wengi tu wanateseka
Huku wanakataluwa na kule wanakataliwa kisa wazazi mmoja wa Huku na mwingine wa kule
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom