Ikiwa tunasoma kuwa Mungu na shetani walikuwa wanapiga stori, kwa nini iwe shida kwa Mbowe na Makonda kuzungumza?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
Mpo salama bila shaka!

Mahasimu wakubwa wakihistoria katika imani na dini ambao ni Mungu muumbaji na Lusifa ambaye huitwa shetani licha ya uhasimu wao karibu kutoana roho na kutaka kupinduana katika siasa za rohoni, lakini tunasoma walikuwa Wanapiga stori na kuteta juu ya Wanachama wa vyama vyao vya siasa katika Roho.

Iweje baadhi ya Watu waone shida kwa Mbowe kuteta, kujadiliana, kupiga stori na Makonda?

Siasa za mwili zinaiga siasa za rohoni.

Itakuwaje sisi wanadamu tukigundua kuwa vita baina ya Lusifa na Mungu ni Siasa tuu na wala hakuna ugomvi mkubwa kati tuaminishwavyo?

Ingawaje mimi Taikon ndiye Mtibeli ninaamini na kujua Mungu na shetani ni mhusika mmoja. Yaani Mungu ndiye shetani na shetani ndiye huyohuyo Mungu.

Acha nipumzike sasa.
 
Back
Top Bottom