Ikitokea leo umeachishwa kazi! Utafanya nini?

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
929
1,277
Wakuu naomba nipate michango yenu, leo gafra umeachishwa kazi ofisini kwenu, kwa sababu ya aina yoyote ile, je vip utaingia mtaani kuanza maisha mapya, na utafanya nin ili urudi katika hari ya kawaida? kila mmoja wetu avae uhusika kuwa ndio yeye, angafanya nini?
 
Mmmh ..hyo ni kama ajari ya ghafla unapo kua dereva huwezi sema nitafunga brek au nitaruka kutoka nje.. ila utakacho kifanya hapo huaga ni maamuzi ya haraka... kwakua hii ni kazi kwa mimi nutaamua kukaa nyumbani bila kutokatoka ovyo kwa wiki kama moja huku nikiwashirikisha watu wangu wa karibu ambao sio wafanyakazi ya kuajiriwa... uamuzi utatokea tuu.
 
Wakuu naomba nipate michango yenu, leo gafra umeachishwa kazi ofisini kwenu, kwa sababu ya aina yoyote ile, je vip utaingia mtaani kuanza maisha mapya, na utafanya nin ili urudi katika hari ya kawaida? kila mmoja wetu avae uhusika kuwa ndio yeye, angafanya nini?

Kwakweli mkuu hiyo situation ni sawa na kumfumania
mke na mshikaji wako wa karibu kabisa, nadhani uamuzi wake
unaujua namna unavyokuwaga.
 
ntamwambia mke wangu najua atanisaport immotional
then nimuombe mungu anipe nyingine
huku nikipata ushauri kutoka sehem tofauti
 
Swali zuri. Ukitaka kujibu hili jiulize unapoishiwa pesa huwa unapata mawazo yapi ya kukuongezea kipato? Ukiyafanyia kazi hayo kabla hayajakukuta mabaya basi utapata jibu la swali hili.
 
maisha yapo hivi kila siku ufanyapo kazi jitahidi kuwa na mradi wowote mradi wowote
nasisitiza mradi wowote haijarishi wa aina gani.hata kama umefungua genge ni vyema sana.angalia unaishi wapi na kuna fursa zipi .
mfano ;katika maisha tumia rasilimali ulizo nazo kuwa kama machagga kama sio mchagga nawapenda hawa watu kwani mara nyingi hawaangalii aina ya kazi wanayofanya wanaangalia pesa wanayopata.......kama katika sherehe ya harusi yako afu ukapata kazawadi ka deep freezer harafu unaishi maeneo ya stand ambako vijana wanauza vinywaji ukigandisha mabarafu katika magaloni yaliyokatwa ya liter 5 kumi na kuyauza kwa 500 maana yake una 500 x10=5000
5000x30=150,000/ utalipa umeme tsh 50.000/ chenji inabaki
 
Iliwahi kunitokea hali kama hiyo. Kulikuwa na sintofaham ofisini, nikapewa barua ya kujieleza. nilijieleza kama pg 10 hivi. management ilikaa kimya zaizi ya mwezi. baadae niliugua nikakaa off duty kwa siku tatu. siku ya nne nikiwa bado sijarecover fully, nilikwenda ofisini. kufika tu, nikakumbana na barua ya termination. niliporudi home homa iliongezeka maradufu niliugua zaidi ya wiki nakumbuka mpaka nilienda kupima HIV.

Nilipopona sikukumbuka kama niliachiswa kazi badala yake niliingia mtaani na kuanza ujasiri amali kwa kazi ambayo hakuna graduate kwa wakati ule angethubutu kuifanya (low profile job).

nikiwa nafanya hiyo kazi nilikutana na mfanya kazi mwenzangu kule nilikokuwa, ki-umri alikuwa mkubwa sana kwangu ila hakuwa na elimu hivyo alikuwa chini yaku. aisee! alinitolea kashfa na kunidhalilisha tena mbele za watu! hadi leo maneno ya yule mzee bado yanapasua masikio yangu... namnukuu, "mnamuona huyu bwana mdogo? tulikuwa naye ofisini na alikuwa na nafasi nzuri sana kumbe si lolote kuachishwa kazi tu leo amekuwa machinga... wanajifanya wamesoma lakini hawana lolote"

Wiki moja baadae kampuni iliyokuwa competitor na kampuni niliyoachishwa kazi wakanitumia mjumbe kuwa wananitaka nikasaini mkata nao. nilijiuliza kama siku mbili hivi nikaamua kukataa

leo hii sijutii uamzi wangu wa kukataa offer ile
 
Hongera kwa hiyo experience yako
nadhani ulikuwa na bahati ya mtende
kuota jangwani.

Baada ya kuaachishwa kaz ....nilienda songea kuuza ufuta na degree yangu....leo hii najuta kwa nn sikuanza mapema ....kujiajiri kunalipa asa ukiwa na asira
 
Vijana hili ni swala zuri na muhimu majibu yake hayahitaji mzaha. Linagusa maisha it's not a joke ladies and gentlemen.
 
Ni kipindi kigumu sana kinaitaji utulivu wa hali ya juu sana na kujitambua imenikuta hali kama hiyo nimetoka kufunga ndoa baada ya miezi miwili nafukuzwa kazi nilikua na wakati mgumu sana nashukuru pesa nilizokua naweka akiba zilinisaidia kwa kipindi hicho mpaka nikapata kazi ila ni kipindi kigumu sana
 
Achana na nadharia ni dhahiri kuwa miongoni mwetu tumeshaacha kazi na kuachishwa kazi pia.Unapoachishwa kazi kabla ya kufanya chochote na kujipanga ni vyema ukaangalia aina ya taasisi,shirika au kampuni ulilofanyia kazi.Kuna mashirika na makampuni hufuata sheria zote na kuwapa wafanyakazi stahiki zao husika wengine hawafanyi hivyo.

Kama taasisi uliyokuwa unafanyia kazi inatoa stahiki hizo basi ni kitu kizuri na ni kitu cha kwanza unachotakiwa kuanza nacho.Dai stahiki zako NSSF,PPF,GEPF nk.

Hii itakusaidia katika kupata pesa ya kuishi bila kazi, kununua magazeti na 'bundle' na kufuatilia vyanzo mbalimbali vya nafasi za kazi,nauli ya kwenda kwenye usaili wa kazi na hata kukupatia mtaji wa kufanya jambo lolote la kukuingizia kipato.

Kama mtaji ni mkubwa basi fungua biashara uliuokuwa ukiiwaza siku zote maishani huku ukiendelea kuomba kazi na kufanya usaili wa kazi mbalimbali.

Kama taasisi uliyokuwa ukifanyia kazi haitoi stahiki hizo basi nenda pale "AKIBA House" kuna mahakama ya kazi (CMA kama nakumbuka vizuri) Onana na mawakili ambao kazi zao ni kuwatetea wafanyakazi ambao wenye matatizo kama hayo ma waajiri wao.Ni vyema ukaenda na vielelezo vyote muhimu vitakavyokusaidia kuoata haki zako.

Kitu kingine muhimu ni kwamba usiache kuomba kazi hata kama upo kazini.Hakikisha unafanya kazi ile unayoona ni kazi ya ndoto yako na ni kazi yenye maslahi yaani "Decent job" yenye sifa zifuatazo sio lazima zitimie zote:
*Mshahara mzuri unaokuwezesha kukidhi mahitaji yako yote muhimu;
*Hulipa stahiki zako kama mfanyakazi;
*Hutoa "bonus" au kiasi fulani cha faida kwa wafanyakazi wake;
*Hutoa likizo yenye malipo;
*Hutoa bima kama vile ya Afya na Ajali kazini;
*Hutoa malipo ya nyumba au usafiri kwa waishio mijini na
*Kutoa ama kuwezesha wafanyakazi kupata mikopo ili kujiongezea kipatoa au kujiwezesha kiuchumi nk.
Natumai mchango wangu huu wa mawazo utawasaidia wengi.Siku njema.
 
Bila Shaka kila mwanadamu Mungu humpa riziki. Jiulize ndege wanaishije? Hawalimi wala hawasokoti ila Mungu awalisha. Mungu Bila Shaka hufungua milango usiyoijua na kukupa riziki. Nakumbuka boss alifungia mshahara wangu kionevu gafla nashangaa atm haisomi kwa mwezi mmoja nikiwa napambana nilipata madeal ya kutosha kwa mfano kutumwa bidhaa fulani naenda duka za jumla chenji ya kutosha. Nashukuru Mungu alivyoniihifadhi wala sikumwambia ndugu yoyote. Pia nilikuwa na pikipiki ambayo sikuwa naitumia mara kwa mara nikihofia ajari lakini nilipata ujasiri wa kuanza kuitumia kuendea kazini nikifuatilia pesa zangu. Kwakweli tumshukuru Mungu na tuache kujivuna na kujisifia kuwa nguvu zetu ndizo zinazotuma mali tunakuwa tunakosea sana. Inapaswa tumshukuru Mungu sana kwani ndiye mgawa riziki.
 
Back
Top Bottom