Ni kipindi kigumu sana kinaitaji utulivu wa hali ya juu sana na kujitambua imenikuta hali kama hiyo nimetoka kufunga ndoa baada ya miezi miwili nafukuzwa kazi nilikua na wakati mgumu sana nashukuru pesa nilizokua naweka akiba zilinisaidia kwa kipindi hicho mpaka nikapata kazi ila ni kipindi kigumu sana
Achana na nadharia ni dhahiri kuwa miongoni mwetu tumeshaacha kazi na kuachishwa kazi pia.Unapoachishwa kazi kabla ya kufanya chochote na kujipanga ni vyema ukaangalia aina ya taasisi,shirika au kampuni ulilofanyia kazi.Kuna mashirika na makampuni hufuata sheria zote na kuwapa wafanyakazi stahiki zao husika wengine hawafanyi hivyo.
Kama taasisi uliyokuwa unafanyia kazi inatoa stahiki hizo basi ni kitu kizuri na ni kitu cha kwanza unachotakiwa kuanza nacho.Dai stahiki zako NSSF,PPF,GEPF nk.
Hii itakusaidia katika kupata pesa ya kuishi bila kazi, kununua magazeti na 'bundle' na kufuatilia vyanzo mbalimbali vya nafasi za kazi,nauli ya kwenda kwenye usaili wa kazi na hata kukupatia mtaji wa kufanya jambo lolote la kukuingizia kipato.
Kama mtaji ni mkubwa basi fungua biashara uliuokuwa ukiiwaza siku zote maishani huku ukiendelea kuomba kazi na kufanya usaili wa kazi mbalimbali.
Kama taasisi uliyokuwa ukifanyia kazi haitoi stahiki hizo basi nenda pale "AKIBA House" kuna mahakama ya kazi (CMA kama nakumbuka vizuri) Onana na mawakili ambao kazi zao ni kuwatetea wafanyakazi ambao wenye matatizo kama hayo ma waajiri wao.Ni vyema ukaenda na vielelezo vyote muhimu vitakavyokusaidia kuoata haki zako.
Kitu kingine muhimu ni kwamba usiache kuomba kazi hata kama upo kazini.Hakikisha unafanya kazi ile unayoona ni kazi ya ndoto yako na ni kazi yenye maslahi yaani "Decent job" yenye sifa zifuatazo sio lazima zitimie zote:
*Mshahara mzuri unaokuwezesha kukidhi mahitaji yako yote muhimu;
*Hulipa stahiki zako kama mfanyakazi;
*Hutoa "bonus" au kiasi fulani cha faida kwa wafanyakazi wake;
*Hutoa likizo yenye malipo;
*Hutoa bima kama vile ya Afya na Ajali kazini;
*Hutoa malipo ya nyumba au usafiri kwa waishio mijini na
*Kutoa ama kuwezesha wafanyakazi kupata mikopo ili kujiongezea kipatoa au kujiwezesha kiuchumi nk.
Natumai mchango wangu huu wa mawazo utawasaidia wengi.Siku njema.