Ikipendeza serikali isiwatambue kama wanandoa wenza wanaoishi bila kufunga ndoa

Protector

JF-Expert Member
May 20, 2019
414
877
Habari wanajukwaa,

Nisiwachoshe sana twende kwenye mada moja kwa moja.

Siku hizi kuna kampeni kubwa ya kukataa kufunga ndoa kwa vijana wa kiume, matokeo yake wanachukua vimada wanaishi nao na baada ya muda fulani mwanamke anatimuliwa bila chochote anaondoka na kwenda kuanza maisha mapya huku akiwa amepoteza muda mwingi kwa mwanaume.

Ikiwekwa sheria ya kwamba kama umeishi na mwenza wako bila ndoa basi ikitokea mmekosana na kuachana isitambuliwe kama mlikuwa mnaishi kama mume na mke bali ijulikane mlikuwa mnachepuka tu.

Hii italeta uwajibikaji na heshima kwa wenza kwa kuwa wataogopa kuingia kwenye wenza bila kufunga ndoa. Jamii itapunguza watoto wa mtaani maana wenza watalazimika kufunga ndoa na wimbi la watoto kukataliwa au kuachwa na baba zao litapungua kwa kiasi fulani.
 
Back
Top Bottom