Ijue biashara ya vitenge kutoka Kigoma. Fahamu namna ya kutambua Java na Wax feki utajirike

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,907
Watu wengi hawajui kwanini biashara ya vitenge hutokea Kigoma, pia wengi hawafahamu wapi watapata Vitenge halisi na original, post hii yenye urefu itakufungua zaidi ili uweze kufahamu kwanini sisi watu wa Kigoma tunahusishwa na biashara ya vazi la Vitenge.

Nifuate kwa umakini mimi mkali wako.
Kitambaa cha Batiki ilikuwa ni rasilimali kubwa iliyotumika kuandaa vitenge vya Wax huko nchini Indonesia.

Unapoambiwa vitenge vya wa Wax inamaanisha ni wax ya nyuki (Nta ya nyuki) ilipochanganywa na rangi za nguo iliimarisha ubora na haikutoka kirahisi hata iliponyeshewa na mvua.

Miaka ya 1850. Baada ya Indonesia kuwa koloni la Netherlands, ufundi huu wa vitenge ulihamishwa na kupelekwa Holland. Wakati huo huo Netherlands ilichukua Pwani ya Dhahabu Afrika (The Gold Cost today’s Ghana). Na katika bidhaa ilizopeleka Ghana ni batiki wax print. Bidhaa hii ilipokelewa kwa kasi mno na Africa ilianza kutumia batiki wax kama vazi la kila siku.

Biashara iliposhamiri meli za Netherlands na Scotland zilipeleka vitenge Ghana miaka ya 1870-1930 kipindi hiki Netherland iliajiri watu kutoka Afrika Magharibi kwa wingi katika jeshi lake ili kupigania koloni la Indonesia.

Kitenge kizima ni yadi 12 lakini mauzo ya nusu kitenge yadi 6 hufanyika pia. Yadi sita ndiyo vipande vitatu. Afrika sasa wana viwanda vya kuzalisha vitenge vya wax. Mpaka sasa hivi majina maarufu ya vitenge vya wax ni imiwax, java print, roller print, na Le fancy. Uzalishaji wa kitenge kisicho na wax ni rahisi zaidi.

Uzalishaji wa vitenge vya (nta ya nyuki) wax sikuhizi umebaki kama zamani. Vitenge vingi vya sikuhizi sio vya nta ya nyuki (non wax) print lakini teknologia imeimarika kiasi cha kuwa non wax print ni nzuri pia kutumika.

Sasa je Vitenge vya Kigoma vinatoka wapi?

Vitenge ni vazi la Afrika, kutoka Magharibi mpaka Mashariki, Kusini hadi Kaskazini. Ghana na Nigeria wana viwanda vya kuzalisha vitenge, Vitenge vya Kigoma vinatoka Ghana na Nigeria kwasababu nchi hizo mbili zinabiashara kubwa sana na nchi ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, maana yake mzigo unapita Cameroon, Congo DRC na hatimaye Burundi ndiyo vinaingia Kigoma. Nasisi watu wa Kigoma tupo karibu na Congo DRC na Burundi kuliko mkoa mwingine.

Hapo zamani Route ya Ivory Cost, kutokea Atlantic ocean ilikua inatumiwa na wachuuzi wengi wa vitenge na mavazi. Watu wa Kigoma ndio wameanza kuvaa mavazi mazuri, vito vya dhahabu, kutumia dawa ya meno na mapambo pamoja na mavazi mengine kuliko watu wowote katika nchi ya Tanzania.

Kipindi cha miaka 18 baada ya vita ya Kagera watu wa Kigoma tayari walikuwa wameshaanza kulalia magodoro, shuka, kutumia dawa za meno mafuta ya kupikia bila kusahau vitenge kutoka Cameroon, Congo, Uganda mpaka Kagera. Sababu kubwa ni hii Route ya Ivory Cost, kutokea Atlantic ocean ilikua ikipitisha bidhaa kwa wingi.

Vitenge vya Kigoma vinatoka Ghana na Nigeria, hizi nchi mbili zinabiashara kubwa sana na nchi ya Congo. Kuna mchanganyiko wa vitenge aina ya Wax Hollandaise na Nigerian Wax pia Ghana ni wazalishaji wakubwa wa vitenge.

Vitenge vingi vya Wax na Java vilivyojaa Kariakoo na kule Kitumbini huitwa Vitenge vya Kigoma kwasababu huingilia Katoro kutokea Mkoani Kigoma na Mtukula.

Unapoambiwa vitenge original inamaanisha pia kuna Vitenge feki vipo mitaani. Kuna utofauti mkubwa wa Vitenge Original na vitenge feki, Kariakoo pia kuna vitenge feki muda mwingine, yaani watu wanaenda kutoa copy yake China ila vya Congo Original vipo tofauti na vya kufyatuliwa huko China, Kwa mtazamo utaona vipo sawa mpaka ufunuliwe utofauti wake kwa ubora na uzito na jinsi vinavyopoteza rangi (kuchuja) haraka tofauti na vya Congo-Kigoma.

Biashara ya vitenge inamtajirisha mtu kwa haraka

Nakubusu hii inakuhusu
 
Asante sana, tofauti ya wax na java ni ipi?

Pia umesema kabla ya vita ya kagera watu wakigoma ndio wa kwanza kulalia magodoro, si magodoro yalikuwepo tangu kabla sanaa?

Au unamaanisha kwa wingi wake?
 
Asante sana, tofauti ya wax na java ni ipi? Pia umesema kabla ya vita ya kagera watu wakigoma ndio wa kwanza kulalia magodoro, si magodoro yalikuwepo tangu kabla sanaa? Au unamaanisha kwa wingi wake?
Hatari sana, anajipa sifa zisizokuwepo. Inafanya hata kufikilia credibility ya story yake.
 
Waholanzi waliiba teknolojia kutoka Indonesia.
Hapa napata jibu kuwa kwa nini Asia ni wazalishaji wakubwa wa nguo, kumbe hawakuanza leo.
 
Nakuunga mkono hii biashara nimeishuhudia kwa macho yangu hapa bujumbura kama ilivyoeleza (SoC03 - Jinsi Fursa nchini Burundi zinazoweza kubadili maisha na kuongeza kipato chako).. Aisee wakongo wanaupiga mwingi sana kwenye hii biashara japo pia kwa TZ vitenge ni biashara kama ya magendo tu kwasasa vinakamatwa sanaaa kusema ni biashara ya kutajirisha kwa haraka ni kulamba Uzi ili upenye kwenye tundu la sindano(kuongeza chumvi)....!!
 
Back
Top Bottom