Elections 2010 Igunga wakisahihisha makosa yao tutawasamehe... ?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,358
39,065
rostam.png

UAMUZI wa wapiga kura wa Igunga mwaka 1994 ndio uliotupatia Rostam. Ni uamuzi huo huo ndio uliotupatia Rostam mwaka 1995 na ni uamuzi ule ule ndio uliomrudisha tena mwaka 2000. Ni uamuzi wa wapiga kura wa Igunga mwaka 2005 uliomrudisha tena Rostam tena akiwa meneja wa kampeni ya Rais Kikwete. Naam, ni uamuzi wa wananchi wa Igunga uliomrudisha tena Rostam mwaka 2010 kwa ushindi wa zaidi ya asilimia 70. Ni wao wananchi wa Igunga waliolipatia taifa Rostam Aziz. Ni wao waliofanya kosa hili na kulirudia mara nne, tena kwa furaha.


Rostam alipoingia bungeni alikwenda na kupigania maslahi ya chama chake na ya biashara zake. Kwa kutumia migongo iliyopindika na nyuso zilizochoka za wana Igunga alikwenda bungeni na huko akajitengenezea mtandao wa watu wenye kuamini itikadi yake na matokeo yake ni kuwa siasa za Tanzania zikachafuliwa rasmi. Si kwa makosa ya Rostam peke yake tu, tukisema hivyo tutakuwa hatumtendei haki bali kwa kushirikiana na wabunge wengine na viongozi wengine wa CCM kututengenezea mfumo mbovu, dhalimu wa utawala.


Ni mfumo huu ambao umeendelea kuligawa taifa kati ya wale walio nacho na wale wasiokuwa nacho, wale wenye madaraka na wale wasio na madaraka, wale wenye nguvu na wale walio dhaifu. Ni mfumo ambao RA (kama anavyojulikana na wengi) ameshiriki kuujenga.
Hakuna wakati wowote ambapo RA amewahi kusimama kuukosoa mfumo huu au hata kuonesha kuwa anajua madhara yake.
Tunaambiwa ni miongoni mwa wabunge wa chache ambao hawajawahi kuuliza maswali bungeni au hata kumbana waziri fulani. Alikataa bungeni kama mahali pa kufanyia biashara, kukutana na washirika mbalimbali, kukubaliana madili ya hapa na pale na hatimaye alipochoka aliweka manyanga chini na kulaani "siasa uchwara" za majitaka.


Lakini wakati wote huo alikuwepo mwana Igunga ambaye angeweza kutoa changamoto kwa Rostam na kuonesha uzalendo wa kupigania wananchi wake kwelikweli. Tangu mwaka 1994 mwana Igunga huyo alijionesha kuwa anata nia ya kuwatumia wananchi wa Igunga. Aliionesha nia hiyo hadi mwaka 2010 lakini mara zote hizo alikubali kukaa pembeni na kimya mbele ya RA. Huyu si mwingine bali ni Dk. Dalaly Kafumu. Dk. Kafumu alikubali kukaa pembeni – japo kwa manung'uniko – kumpisha RA. Hajawahi kusimama na kuwahimiza wananchi wake kumkataa RA kwa sababu ya mambo ambayo yalikuwa yanaendelea kitaifa. Aliamua kula njama ya ukimya akifurahia nafasi yake kwenye vyeo vya juu akiwa ni Kamishna wa Madini nchini.


Kama kweli Kafumu alikuwa na nia ya kupigania masilahi ya watu wa Igunga angeweza kabisa kujitoa CCM na kusimama dhidi ya Rostam. Hakufanya hivyo. Kafumu angeweza kusema kuwa RA hajawa kichocheo cha maendeleo Igunga na amekuwa tatizo kwa taifa. Kwamba kuhusishwa kwake kwa kashfa mbalimbali kulikuwa kunaletea CCM sifa mbaya. Hakufanya hivyo. Kwanini? Kwa sababu wote wako chama kimoja na masilahi yao yamefungamana na yale ya chama.


Ndiyo maana hadi leo Kafumu hajasimama kuzungumzia vita dhidi ya ufisadi au msimamo wake kuhusu wahusika wa kashfa za madini. Hajasimama kuonesha yuko upande upi katika vita ya magamba ndani ya chama chake. Na badala yake yeye kama baadhi ya viongozi wa CCM wameamua kuchukua ukimya ule ule ili wasijulikane wako upande gani. Kafumu aliamua kuipenda CCM na kazi yake zaidi kuliko kuwapigania wananchi wa Igunga. Kwa maneno mengine kama RA asingeamua kujiuzulu baada ya kuzidiwa na shinikizo la kisiasa Kafumu angeendelea kula bata kwenye ofisi yake huku akisubiri mwaka 2015 au 2020. Kweli huyu ni kiongozi ambaye Igunga wanamtaka?

Ndipo hapa basi wananchi wa Igunga wanapaswa kutambua. Kufanya kosa (mwaka 1994) si kosa. Kurudia kosa (1995) ni kosa, kulirudia kosa tena (2000) ni kosa kubwa.


Lakini kulirudia kosa kubwa (2005, 2010) si kosa tena ni uzembe wa kufikiria. Iweje mtu analima kwa mtindo ule ule, na shamba lile lile na mavuno yanazidi kupungua na yeye anaendelea kulima vile vile akitarajia labda mambo yatabadilika? Kama nyumba imeanza kuwa na nyufa mwenye nyumba akiendelea kupiga magoti kuwa nyufa zisitokee ukuta ukianguka atalalamika kuwa "sala" zake hazikusikilizwa? Wananchi wa Igunga wanahitaji malaika gani atoke ahera madukani kuja kuwaambia kuwa wamefanya makosa vya kutosha?


Lakini kinachonisumbua miye zaidi ni kuwa hivi wanapopiga kura hawajui matokeo yake kwa taifa? Hivi hadi leo hii wapo watu ambao wanafikiria kupiga kura ya mbunge ni swala la mahali tu? Wapo watu wanaotaka wananchi wa Igunga wapige kura kwa kuangalia masilahi ya Igunga peke yake. Haya ni makosa. Maamuzi ya Igunga yanaathari kubwa sana kwa taifa kama wakichagua vibaya.


Tayari tunaona maamuzi yao yalivyogusa taifa kwa miaka hii karibu 18. Uamuzi wa wana Igunga utagusa taifa kwa namna nyingine tena.
Ni kwa sababu hiyo naamini kuwa wananchi wa Igunga wamepewa nafasi ya pekee ya kusahihisha makosa yao. Nafasi ya kutakafakari na kutambua kuwa ni maamuzi yao ndio ambayo yamechangia sana kuleta matatizo ya kisiasa nchini. Wazee, kina mama na vijana wa Igunga ambao walishabikia ubunge wa RA na ambao pasipo haya wala hisia ya hatia waling'ata alipowaambia anajiuzulu ndio hawa ambao waliweza kufurahia kidogo lakini kwa gharama kubwa sana kwa taifa.


Yawezekana kabisa kama wananchi wa Igunga wangechagua kwa umakini na kwa usahihi mwaka 1994 yawezekana kabisa kashfa za Richmond, EPA na Dowans zisingetikisa taifa hivi. Yawezekana kabisa kama wananchi wa Igunga wangefanya uchaguzi sahihi yawezekana hata utawala mzima uliopo madarakani sasa hivi usingekuwepo. Hivyo nafasi hii ni ya kihistoria kwa wana Igunga. Ni nafasi ambayo inahoji kama wametambua thamani yao na thamani ya utu wao. Ni nafasi ambayo inahoji kama wako tayari kufanya maamuzi ambayo matokeo yake wanayatarajia. Kwamba, wako tayari kuamua kubadilisha mwelekeo wa jimbo lao na mwelekeo wa Tanzania kwa kumchagua mgombea ambaye chama chake kinawakilisha mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini.


Je, wanajua kuwa wanaposhika lile karatasi la kura ni kwamba wameushika utu wao mkononi mwao? Je, wanajua kuwa mpiga kura anaposhika karatasi ya kura ameshikilia njozi zake, matamanio yake, maisha ya watoto wake na taifa lake kwenye vidole vyake? Je, anajua anapopiga kura hiyo anapigia kura hatima ya maisha yake?


Hivyo, siku ya Jumapili wananchi wa Igunga watakuwa wamepewa nafasi ya kuamua wanataka kufanya nini na utu wao. Wanaweza kuamua kuendelea na watu kutoka chama kile kile, chenye sera zile zile zilizoshindwa au wakaamua kuwa sehemu ya mabadiliko na hivyo kuweka historia ya aina yake mkoani Tabora ambako tangu zamani sana kilikuwa kiini cha fikra za mabadiliko. Wananchi wa Igunga watapewa nafasi ya kuamua wanataka kuuza utu wao kwa sababu wametishwa, kwa sababu wanaogopa au wako tayari kupigia kura yao kwa gharama yoyote ile?


Njia pekee ni kuwa wananchi wa Igunga wanaitwa na historia kujitokeza mwa maelfu yao kupigia kura maisha yao. Wanaitwa kama ni malaika toka Mbinguni wajitokeze bila kujali kejeli, bila kujali maneno, bila hata kujali polisi na mitutu yao kuamua kutumia haki pekee ya uhuru wao ya kuamua kiongozi wanayemtaka. Wananchi wa Igunga wanaitwa kutokukaa nyumbani na kuombea wengine "wawachagulie" kiongozi wao. Ni witu mtakatifu, wito wa utu wao.


Hivyo, kwetu sisi wengine tunawaita kuwa sehemu ya mabadiliko. Wafanye uamuzi ambao unaendana na matamanio ya wananchi wenzao. Lakini bado wana uhuru ule ule. Wakiamua wanaweza kurudia kosa lile lile mara ya tano! Hakuna tofauti kati ya Rostam na Kafumu. Hakuna. Wote wamelelewa na mfumo ule ule na mitazamo yao kuhusu Tanzania ni ile ile. Lakini wananchi wa Igunga wanaweza kabisa kuamua kurudia kosa hilo hilo, sisi tutawalaumu lakini hatuna jinsi bali kuheshimu uamuzi wao wa makosa.


Lakini wakiamua kubadilika na kutuma ujumbe usio na utata kwa watawala kuwa Igunga ya sasa si ya 1994 au ya 2005 basi watakuwa wametuma ujumbe ambao unaweza hata kukisaidia CCM katika jitihada zake za kujivua gamba. Wakitumia haki hii kukataa geresha, vitisho, udini, na siasa za dharau wanaweza kujikuta wamefungua ukurasa mpya katika historia yao.


Na wakisahihisha makosa yao hayo ambayo yameligharibu taifa hivi, na sisi wengine tutawasemehe. Wajitokeze kupiga kura, walinde kura zao zote zihesabiwe na wafurahie ushindi na kuwa tayari kuanza ngwe mpya ya siasa Igunga.


Naomba nijisahihishe mimi mwenyewe kwanza. Nimesema kwa kirefu kuhusu "wananchi wa Igunga" na kuwa "wapiga kura wa Igunga" wasahihishe makosa yao. Ukweli ni kuwa watu pekee wanaotakiwa kusahihisha makosa haya ni wana CCM na mashabiki wa CCM waliompigia kura mgombea wa CCM na kuliletea matatizo taifa kwa karibu miaka 18. Hawa wajisahihishe na hapo ndio tutafikiria kuwasamehe.


Kila la heri!
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,189
Lao Wananchi wa Igunga ni pamoja na:

1. Kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura bila kukosa kutumia haki yao,

2. Kuendana na AZMA YA TAIFA zima kung'oa ufisadi na wafadhili wake nchini kwo kurusha mbali harufu zozote za Rostam Aziz na chama chake,

3. Kutokuruhusu mtu yeyote kununua kura zao ama kwa ubwabwa, mahindi ya bure wala viji-DINERO 30 au zaidi.

4. Kujitokeza kwa hiari KULINDA KURA ZAO mpaka kutangazwa wazi mbele yao kwa pamoja hadharani.
 

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,427
Ni kweli kujisahihisha kwao ndiko kutasababisha watu kuwasamehe,lakini yawezekana wakaamuwa kujisahihisha kwa kumchagua tena mgombea wa Ccm wakifikiri kuwa huyu si RA ni sura nyingine kabisa,Je katika masahihisho kama hayo wataweza kusamehewa?

tatizo nilionalo Igunga kwa sasa kuwa kutakuwa na mgawanyo wa Kura na hicho ndicho kitacho wapa ushindi wana magamba kama hivi vyama vingeweza kuunganisha nguvu basi magamba wangekuwa mashakani sana

lakini acha tusubiri tarehe husika ndio utakuwa mwanzo wa msamaha ama la
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,358
39,065
Mwanakijiji

Na vyama vilivyokuwa havikusimamisha mgombea uchaguzi uliopita kwa mfano, tuwachukulieje?

to tell you the truth kati ya vitu vinavyonishangaza sana ni kwanini CDM hawakusimamisha mgombea Igunga wala kushambulia Igunga iivyopaswa. This still baffles me. Kama kuna majimbo ambayo walitakiwa kuyashambulia kwa nguvu hata kama si kwa ajili ya kushinda bali kwa kuonesha kuwa wakkoserious ilikuwa ni majimbo ya EL, RA an AC. Hawakufanya hivyo. Hata leo hii wote wanaogopa kutaja jina la RA huko Igunga na jinsi uwepo wako umekuwa matatizo kwa taifa! why why why?

Maana yake ingewalazimu CCM kuja kumtetea!
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,400
Ukiangalia kwa undani kabisa kosa si la WanaIgunga. Ni la CCM. CCM wana kila nyenzo za kumfahamu vizuri mgombea kabla hawajamteua. Hawakufanya hivo na hadi leo hawafanyi hivo sio tu kwenye ngazi hii ya Ubunge bali hata wagombea wa URAIS. Wapiga kura wetu wengi elimu ya darasani na ya uraia ni ndogo mno. Wengi hadi leo hii wanaamini CCM hii ni ileile ya Mwalimu.
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,400
to tell you the truth kati ya vitu vinavyonishangaza sana ni kwanini CDM hawakusimamisha mgombea Igunga wala kushambulia Igunga iivyopaswa. This still baffles me. Kama kuna majimbo ambayo walitakiwa kuyashambulia kwa nguvu hata kama si kwa ajili ya kushinda bali kwa kuonesha kuwa wakkoserious ilikuwa ni majimbo ya EL, RA an AC. Hawakufanya hivyo. Hata leo hii wote wanaogopa kutaja jina la RA huko Igunga na jinsi uwepo wako umekuwa matatizo kwa taifa! why why why?

Maana yake ingewalazimu CCM kuja kumtetea!
Kwa namna ambavyo RA, EL, AC na Mkono wanavyoendesha majimbo haya kwa "pesa zao wenyewe" sio rahisi CHADEMA au chama kingine chochote kusema lolote na wananchi wa kawaida wa maeneo yale wakawaelewa. Jamaa wana "hati miliki" za majimbo haya kwa sababu ya umasikini wa kipato na ule wa kufikiri wa watu wetu.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,358
39,065
Ukiangalia kwa undani kabisa kosa si la WanaIgunga. Ni la CCM. CCM wana kila nyenzo za kumfahamu vizuri mgombea kabla hawajamteua. Hawakufanya hivo na hadi leo hawafanyi hivo sio tu kwenye ngazi hii ya Ubunge bali hata wagombea wa URAIS. Wapiga kura wetu wengi elimu ya darasani na ya uraia ni ndogo mno. Wengi hadi leo hii wanaamini CCM hii ni ileile ya Mwalimu.

Unajua hili si kweli. Watanzania ni miongoni mwa watu wanaojua haki zao za uraia zaidi labda kuliko watu wengi sana duniani. Tanzania hawajaanza siasa leo, kampeni za siasa zina historia ya karibu miaka sitini sasa katika Tanzania. Tena vijijini wameshirikishwa sana toka zamani. Kilichotokea ni kuwa Watanzania wengi wamekata tamaa. Ndio maana unaona kuwa kule kujijini wakipata hamasa ya kweli wanafanya mabadiliko hili halijaanza wakati wa vyama vingi.

Watu ambao nafikiri wanahitaji kuonesha wanayo elimu ya uraia ni watu wa Dar ambako unaweza kudhania kuwa ndio watu watakuwa wanajua zaidi kuhusu haki zao za uraia n.k. Au utaelezea vipi Tarime, Kigoma Kaskazini, Moshi Mjini au hata Karatu?
 

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,912
1,125
Utawasamehe Wewe ni nani? na usipo wasamehe ni Madhira gani yatawafika, hebu fafanua kidogo ili watu tukuelewe.
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
Kwa namna ambavyo RA, EL, AC na Mkono wanavyoendesha majimbo haya kwa "pesa zao wenyewe" sio rahisi CHADEMA au chama kingine chochote kusema lolote na wananchi wa kawaida wa maeneo yale wakawaelewa. Jamaa wana "hati miliki" za majimbo haya kwa sababu ya umasikini wa kipato na ule wa kufikiri wa watu wetu.

Chama cha siasa hakitakiwi kuonyesha kumuogopa mtu tena hasa mwenye kashfa nyingi Rostam. Kutokwenda uchaguzi uliopita kunathibitisha kuwa Rostam ni "larger than life" na hata CHADEMA kinamuogopa or else kingeenda kupambana nae jimboni.

Na ikiwa hadi sasa kwenye kampeni hawamtaji Rostam kwa ubaya huko jimboni, inaleta shaka kwenye nia hasa ya kuwania kiti hicho cha Igunga
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,400
Siwezi kukubishia Mwanakijiji kwa kuwa nje ya Tanzania sina ninalolifahamu ingawa hapa jirani Kenya makabila yao yanawasaidia sana kufanya mabadiliko. Tarime pia inaathiriwa na siasa za koo ndio maana safari hii waliiondoa CHADEMA. Mkoa wa Kigoma siufahamu vizuri lakini huduma za reli kukosekana kumeiponza sana CCM. Moshi mjini na Wachagga kwa ujumla wao wanafahamika kwa mapenzi mazito kwa vyama vinavyoongozwa na watu wao. Wao ni kama ilivyo Kenya tu. Mtu pekee ambaye amejitahidi kwenye elimu ya uraia jimboni kwake na anafanya kazi ni Dr Slaa na Karatu yake.
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,400
Chama cha siasa hakitakiwi kuonyesha kumuogopa mtu tena hasa mwenye kashfa nyingi Rostam. Kutokwenda uchaguzi uliopita kunathibitisha kuwa Rostam ni "larger than life" na hata CHADEMA kinamuogopa or else kingeenda kupambana nae jimboni.

Na ikiwa hadi sasa kwenye kampeni hawamtaji Rostam kwa ubaya huko jimboni, inaleta shaka kwenye nia hasa ya kuwania kiti hicho cha Igunga
Sio chama cha siasa kinachoogopa bali wagombea. Baadhi ya wagombea wanathubutu hata kugombea lakini wananunuliwa kabisa na mafisadi hawa. Yupo jamaa mmoja alijitokeza kugombea kwa tiketi ya CHADEMA kule Musoma(V) mwaka 2005 jina nimelisahau. Alivyotokomea gizani baadae ni hadithi ndefu.
 

Rafikikabisa

JF-Expert Member
Nov 6, 2009
252
46
Kwani tanzania wakina Rostam unafikiri ni yule wa Igunga tu? Akina Rostam, AC and EL ni wengi tu na ndio maana anaatetewa. Ukiangalia akina Jairo style utagundua ni wengi sana. Kilichomponza RA ni siasa. Wana Igunga ni watu masikini ambao hawawezi kusema chochote kwa RA upige kura usipige RA ilikuwa lazima ashinde. Kwenye Chama hakuna aliyekuwa na uwezo wa kuondoa jina lake. Ukombozi wa Tanzania unahitaji kujitoa sana.
 

Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,893
7,196
Siwezi kukubishia Mwanakijiji kwa kuwa nje ya Tanzania sina ninalolifahamu ingawa hapa jirani Kenya makabila yao yanawasaidia sana kufanya mabadiliko. Tarime pia inaathiriwa na siasa za koo ndio maana safari hii waliiondoa CHADEMA. Mkoa wa Kigoma siufahamu vizuri lakini huduma za reli kukosekana kumeiponza sana CCM. Moshi mjini na Wachagga kwa ujumla wao wanafahamika kwa mapenzi mazito kwa vyama vinavyoongozwa na watu wao. Wao ni kama ilivyo Kenya tu. Mtu pekee ambaye amejitahidi kwenye elimu ya uraia jimboni kwake na anafanya kazi ni Dr Slaa na Karatu yake.
Mkuu, nakubali kwamba kwa baadhi ya maeneo nchini, makosa ya ccm na serikali yake ndio mtaji wa upinzani, isipokuwa sikubaliani na swala la kigoma na reli yake. Jimbo la Kafulila ni jimbo remote kweli kweli, hakuna mawasiliano ya simu katika sehemu kubwa, hakuna barabara (kwa hiyo haawezi kudai reli wakati barabara ya tope haipo), kuna vituo kama sio viwili ni vitatu tu vya afya, yet still wamebadilika.

Mkuu, swala la moshi ni gumu zaidi ya ''uchaga'' uliousema. unafikiri mwenyekiti wa CCM akiwa massawe flani leo, basi ccm itachaguliwa moshi kwasababu hiyo?? I dont think so.

Mfano mdogo, unajua kwa nini Selasini alishinda Rombo?? sio kwasababu CDM inaongozwa na mchaga, NO, it was a tactical error upande wa mzee Pesambili kipindi cha kampeni. Alisimama akamnyanyua mama yake mkono na kuwaambia watu kwenye mkutano kuwa hakuna mwanamke anayeweza kuzaa kidume kama mimi atakayeweza kuwa mbunge wa Rombo. aliyafanya mambo hayo sokoni. wakina mama wakaamua kwamba watamuonyesha. and they did.

Lakini ni swala lilio wazi kwamba kuna maeneo ambayo watu wake wapo open minded kwenye siasa. Iringa mjini kwa mfano, iliwahi kuwa na mbunge mpinzani enzi za Mrema, mwanzoni kabisa mwa siasa za vyama vingi. hii inaonyesha kwamba kuna maeneo ambayo huwezi kuwaburuza ki vile.
 

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,667
Maneno yako Mkuu yangekuwa yanaweza kuwafikia vijana wa Igunga wenye umri wa kuanzia miaka 15 mpaka 45 tungeona mabadiliko makubwa sana Igunga ambayo pia ingetoa mwamko mpya kwa zone kubwa na muhimu sana kwa Taifa [Kwa Makabila ya Wasukuma, Wanyamwezi, Wanyiramba na kwa kiasi Wanyaturu].Tatizo tulilonalo kwa makabila hayo ni mfumo wao wa maisha wa kijadi wa kuwa very royal pasipo kupinga kwa mwenye madalaka japo mhusika atendewi haki na mwenye madaraka.

Upole wa kitabia wa makabila hayo na mfumo wa utawala toka ukoloni na mpaka Serikali huru,tatizo limeendelea kuwepo kwa makabila hayo la kufuata maamuzi ya watawwala [order] pasipo kuhoji na ukitokea kuhoji au kupingana na kiongozi basi wewe ni tatizo kijamii,Na kwa kiwango kikubwa wazee wa kijadi au kijamii wakisimama na kusema kwa umoja wao basi sauti yao ni maamuzi ya jamii.

Na tatizo ili kwa upande fulani pia uligharimu sana Serikali husika kwenye mipangao ya maendeleo japo,kwa kipindi kama hiki cha uchaguzi upole ule na vimbwenga vya wenyeji wa makabila hayo basi ni BONGE YA MTAJI KWA CHAMA TAWALA.Japo ni msiba wa kujiundia kwa siku za usoni.

Umbumbu wa kiufahamu wa wenyeji wa vijijini wa makabila hayo imekuwa sumu hata katika maisha ya kawaida ya kusujudia watawala.Imewagalimu sana kwa majimbo mengi umeona hata aina [silika] ya Wabunge wanawaowachagua kama yule mheshimiwa wa Bastora.

Kwa kiwango kikubwa ninavyowajua makabila hayo ambayo kwa kiwango kikubwa wapiga kura wake walio wengi ni Wanawake na kwa tabia ya makabila hayo iliyowazi ni kuwa kiongozi wa familia ni Mwanamke,basi tegemea ushindi mwingine wa CCM wa Kisayansi.Na CCM kwa kulijua hilo kama ni kanuni ya kimasoko na ambayo hiko sahihi kuwa marketing segment yake ni target halisi ya ushindi wa kuuza bidhaa yake ambayo ni Mbunge wake mtarajiwa.

Chadema inategemea sana kundi la vijana ambao kwa kiwango kikubwa kwa mfumo wa kitabia wa makabila hayo vijana kwa umri huo wa miaka 15-30 huwa na unafiki unaozingatia maslahi yao binafsi na sio kijumuhiya.Na pia umefundishwa kuwa na nidhamu ya woga kwa wakuu wao wa kifamilia ambao ukilejea kwenye staili yao ya kuogopa watawala basi kunauwezekano dakika za mwisho vijana wakatenda ndivyo sivyo kwa CDM.

Ndio maana mwanzoni kabisa mwa mada za uchaguzi wa Igunga nilisema CHADEMA waende IGUNGA kuleta Mwamko ambao kwa ASILIMIA kubwa wametimiza hilo na kuibua nafasi mpya kwa chama hicho kujitizama na kuijsahihisha kama si kujifua na si kujivua gamba kwa kuwa kwa kujivua inaweza kuwa imeshindikana.

CCM watachukua jimbo hilo ila haitakuwa kama KAWAIDA,bali kumeshaibuka CHACHU MPYA YA KISIASA kwa WANA IGUNGA hofu na woga woga wa kijinga na usio na msingi wa kuhofia MAMLAKA baada ya KUHESHIMU MAMLAKA UTAPUNGUA kama si KWISHA.

Hakika yangu vijana wenye umri wa miaka 15-45 ndio wafaidika wa chachu hii kwa kuwa kizazi cha kuanzia miaka 45-kuendelea tayari si mageuzi ya kuleta mwamko dhidi ya Watawala dhalimu.Mpaka sasa kwa makabila hao wenye umri mkubwa bado wanaamini kuwa Baba wa Taifa bado ni moja ya CCM ya leo.

Yote kwa yote TUMEJIFUNZA NA TUTAENDELEA KUJIFUNZA, ukiona mpaka MKUU JOHN POMBE MAGUFULI kaingia ULINGONI [Frontline] ujue hali si sawa kwa CCM,ambao kwa taarifa zisizo na vyanzo rasmi Magufuri kwa vigogo walio wengi ndani ya CCM umuogopa sana kwa kuwa wana imani kuwa uwa ni UNDEFINE CHARACTER.Na hakika kwa kuwa ni Mwana wa Nchi [Son of the Land] amefanya kile kile ambacho ni fumbo kwa wasio ipenda Tanzania kwa kusalimia vyama vyote vya UPINZANI.Kwa picha hiyo Magufuli anajipambanua kuwa CCM kwake ni mfumo tu lakini lililo bora kwake ni Tanzania.

Kwa hilo pia hii zama mpya kwa mabadiliko ndani ya vyama vya kisiasa katika mbinu na mikakati ya kuwajenga [wenyeji wanasema kupepembela] kujiunga na vyama vyao na kuongeza idadi ya wanachama.Maarifa yaliyopatikana IGUNGA na Mbinu na Mikakati imeongeza misamiati katika makarabrasha ya vyama husika.Leo hii tuna tindi kali na Bastora viunoni na risasi nje nje,basi kwa wahusika ni mwanzo mpya wa kuangalia sheria zetu za uchaguzi.

Hakika baada ya IGUNGA nafikilia CCM, watatusaidia tena kutuimizia Wazee wa kujivua Gamba mapacha Watatu sasa itakuwa ni zamu ya Monduri au Bariadi Mashariki.Ni vyema wakafanya hivyo wakatumia chaguzi hizo kujiimarisha huku wakijisafisha.Wakiishia hapo du picha itakuwa nyingine na story ya kujivua gamba ilihairishwa kwa muda kulenga uchaguzi wa igunga kufanyika. Kwa uchaguzi huo kupita tunahakika wapiga kelele wa kujivua gamba wataludi jikoni kuendeleza libeneke.

CCM wajipange upya kwa hilo!!!!!!!!!!!!!
 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
ujumbe siyo wa watu wa igunga bali ni ya watanzania wote mambo mengi watanzania wanayoyaona hivi sasa wengine tulishayaona miaka 10 iliyopita lakini still some of us don't get inasikitisha.
 

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,569
8,024
i hate wana igunga! mfumuko wa bei ni kosa la wanaigunga, ufisadi chanzo chake kikuu, au mizizi ya ufisadi ni kosa la wanaigunga.
 

Pancras Suday

JF-Expert Member
Jun 24, 2011
8,081
3,662
Watanzania wengi wanahitaji mabadiliko kwa sasa kuliko wakati mwingine, watu wanatamani huu uchaguzi wa Igunga ungekuwa kila mahali Tanzania, hivyo basi macho na masikio ya watanzania yapo Igunga kuona wanaigunga watafanya nini ili kuleta hayo mabadiliko tunayoyahitaji kwa sasa, wakifanya makosa tena itakuwa inadhihirisha jinsi gani watanzania wengi wasivyojikomboa kifikra, na wataendelea kupiga vuvuzela la umasikini pasipo wao kujua kuwa chanzo cha umasikini ni wao wenyewe. baada ya hapo utawasikia wanasema serikali legelege ilihali wao ndio legelege walioichagua serikali legelege.
A friend of my enemy is my enemy too.:fencing:
 
6 Reactions
Reply
Top Bottom