Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 730
- 1,225
Katika siasa kuna kitu kinaitwa strategic ambiguity; mfano wake mkubwa ukiwa ni sera ya Marekani kuhusu Taiwan. Kwenye maandishi rasmi USA wanatambua One China policy, ila kila siku wanaendelea kuiuzia Taiwan silaha na kufadhili harakati zote za Taiwan kujitenga na China.
Hapa kwetu ni kama swala la Katiba mpya limeshafikia hatua hiyo. Wakati ilani ya CCM 2025-2030 iliahidi kuhuisha mchakato wa katiba mpya ndani ya siku mia moja za kwanza, hali sasa imeanza kuchukua mwelekeo tofauti.
Ingawa hoja ya kuwa na mchakato wa katiba mpya haikataliwi moja kwa moja, ukizitafakari kauli za Mh. Rais hususani wakati wa upisho wa makamu wa Rais na alipowahutubia wa wazee wa Dar es salaam, kauli ya waziri wa utumishi na utawala bora akiwahutubia wananchi Igunga na ya kauli ya mbunge wa jimbo la kibakwe hivi karibuni; ni wazi kuwa, hoja ya katiba mpya huenda siyo kipaumbele tena.
Changamoto kubwa ya maswala kama haya ambayo msimamo wa chama haupo bayana, ni kusababishiana ajali za kisiasa. Unaweza toka ukiwa na nia njema yakuisemea ilani ya chama kwa wananchi, wenzako nyuma wanaitisha vikao kukujadili.
Ni muhimu sana kwa chama, haswa kwa mambo yanayokuwa yamebeba uzito mkubwa kwenye siasa za nchi, kuwa na kauli thabiti, itakayotetewa na wanachama wote kwa pamoja.