Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Wadau: Habari za ndani nilizopata sasa hivi ni kwamba mgogoro mkubwa unatokota ndani ya uongozi wa juu wa CUF.
Tatizo ni helikopta iliyoletwa mwanzoni mwa wiki iliyopita kutumika katika kampeni, ambayo imebainika ilitolewa na Rostam Aziz ili kuipa nguvu CUF kuidhoofisha CHADEMA katika uchaguzi, jambo ambalo halikutokea, na badala yake CUF ndiyo imetoka katika kinyang'anyiro hicho na majeraha makubwa.
Habari zinasema Baraza kuu la chama hicho halikushauriwa na wala kutoa baraka kwani ulikuwa ni mpango wa Ismail Jussa, Rostam na Hamad Rashid Mohamed.
Jussa na Hamad ni maswahiba wakubwa wa Rostam katika mambo ya biashara na ni makada wa CUF ambao daima wamekuwa mstari wa mbele kuiponda Chadema.
Habari zaidi zinaeleza kuwa Prof Lipumba hakuarifiwa kuhusu helikopta na inasemekana hakupendezewa, hasa pale ikigundulika kwa umma kwamba ni Rostam ndiye aliyeitoa.
Chanzo changu chongeza kuwa awali CCM ilikuwa itumie helikopta zote hizo mbili kutoka kwa Rostam, lakini dakika za mwisho iliamuliwa kwamba moja wapewe CUF ili itumike kuiumiza Chadema.
Msiniulize chanzo cha habari hii ni namna nilivyoipata kutoka CUF kwa kiongozi mmoja wa chama hicho huku Bara ambaye siwezi kumtaja jina hapa kwa wakati huu.