Igunga: Helikopta iliyotumika CUF yaanza kukivuruga chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igunga: Helikopta iliyotumika CUF yaanza kukivuruga chama

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Zak Malang, Oct 3, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau: Habari za ndani nilizopata sasa hivi ni kwamba mgogoro mkubwa unatokota ndani ya uongozi wa juu wa CUF.


  Tatizo ni helikopta iliyoletwa mwanzoni mwa wiki iliyopita kutumika katika kampeni, ambayo imebainika ilitolewa na Rostam Aziz ili kuipa nguvu CUF kuidhoofisha CHADEMA katika uchaguzi, jambo ambalo halikutokea, na badala yake CUF ndiyo imetoka katika kinyang'anyiro hicho na majeraha makubwa.

  Habari zinasema Baraza kuu la chama hicho halikushauriwa na wala kutoa baraka kwani ulikuwa ni mpango wa Ismail Jussa, Rostam na Hamad Rashid Mohamed.

  Jussa na Hamad ni maswahiba wakubwa wa Rostam katika mambo ya biashara na ni makada wa CUF ambao daima wamekuwa mstari wa mbele kuiponda Chadema.

  Habari zaidi zinaeleza kuwa Prof Lipumba hakuarifiwa kuhusu helikopta na inasemekana hakupendezewa, hasa pale ikigundulika kwa umma kwamba ni Rostam ndiye aliyeitoa.

  Chanzo changu chongeza kuwa awali CCM ilikuwa itumie helikopta zote hizo mbili kutoka kwa Rostam, lakini dakika za mwisho iliamuliwa kwamba moja wapewe CUF ili itumike kuiumiza Chadema.

  Msiniulize chanzo cha habari hii ni namna nilivyoipata kutoka CUF kwa kiongozi mmoja wa chama hicho huku Bara ambaye siwezi kumtaja jina hapa kwa wakati huu.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Mwanzo wa mwisho. Kama ni kweli na kutokana na kura walizopata, basi ni freefall kwa chama hicho.
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  JF where we dare to talk openly ndo maana ya kutumia haya majina kama Counterpunch. Mtaje mkuu, anyway back to the topic!! Inawezekana ni kweli kabisa. Prof Ibrahim Lipumba karibu kwa wapambanaji CDM.
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,829
  Trophy Points: 280
  Siasa za kicheck bob zimekimaliza chama hichi.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,544
  Trophy Points: 280
  Prof. Lipumba ni mgombea wa kudumu wa CUF kwenye urais wa Muungano hivyo hawezi kujiunga na chama kingine chochote.
   
 6. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kumbukeni movement ya pendulum bobs!!!!!!!!!!!!
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii habari ililetwa hapa JF wiki iliyopita kama tetesi lakini sasa kadri muda unavysogea ukweli unaanza kudhihirika.

  CUF wameaibika sana katika uchaguzi huu kwa kweli, na helikopta hii inathibitisha pasi na shaka kwamba CUF ni CCM-B.

  Nilibahatika kuona baadhi ya speech za Jussa, Mtatiro na Hamad Rashid kupitia tv Sibuka. Walikuwa wamejikita kuishambulia chadema na viongozi wake badala ya kueleza sera, sasa watu wa igunga wakaamua kuwashikisha adabu.
   
 8. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  CUF kwa kweli mnatia aibu kama fisadi papa anawapa helicopter na mnakubali. Mmejidhalilisha sana na mmevuna mlichopanda.
   
 9. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Hizi zaweza kuwa sababu za Hamad Rshid kumhofia Prof Safari alipotaka kugombea uenyekiti wa CUF.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mie namsikitikia Mtatiro, ambaye kenda kujinasa na siasa za mayakhe, wenye kutanguliza udini mbele. Ni kijana shupavu na angeweza kutoa mchango mkubwa katika kuikomboa nchi hii kutoka kwa mafisadi kama angekuwa ndani ya CDM.

  Mfano mwaka jana angeachana na CUF na kujiunga CDM, angeweza kumn'goa fisadi Iddi Azzan jimbo la Kinondoni bila ya wasiwasi wowote. Hata hivyo bado naweza kufanya maamuzi mazito. Unakaribishwa kwa watu serious.
   
 11. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Sasa mgogoro unafukuta kwa nini, helikopta imekausha akaunti za chama au ndio sababu ya kushindwa au helikopta imeanguka au ni nini ime wa cost mpaka wamaindiane?
   
 12. Mr.Toyo

  Mr.Toyo JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2007
  Messages: 433
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Japo ku-PM pia?
   
 13. KIDESELA

  KIDESELA Senior Member

  #13
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Hahahaha faida ya usaliti hio ndio mwisho wenu sasa unakwenda! Mlijua siri mmeumbuka kwisha kabisa! Na mtaji wenu aliosema lipumba ndio kusema mmwkula mtaji?
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nadhani katika CUF wapo viongozi makini ambao hawapendi mambo haya ya kukiachia chama kutumika na fisadi mmoja ili kukiharibia chama kingine cha upinzani.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Bila shaka viongozi wa cuf wamekubali kuvurugwa na helikopta baada ya kushindwa vibaya uchaguzi. Kama ingetokea wameshinda ama wakavuna kura ilizovuna chadema wangekuwa na la kusema.

  Sasa kinachowauma zaidi ni kwamba wamekula mtaji wa kura 11,000 kwa helikopta ya gamba kuu rostam. Inawezekana kinachowavuruga ni kulipa deni la kukodisha hiyo helikopta, siamini kama gamba kuu anaweza kuwapa chopa bure lazima kutakuwa na kamkataba fulani hivi ka kimagumashi na wao huenda hawakukasoma kwa sababu ya kiwewe cha kupata chopa.. Sasa baada ya uchaguzi wamekasoma wakaona kipengele cha malipo kinawabana, pesa watatoa wapi?
   
 16. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
   
 17. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  kuna asilimia kadhaa za ukweli, na kama ni kweli wamekwisha. Ukiiga kunya kwa twmbao utapasuka nini wajameni?

  .......................................................jibu lako kwenye dots
   
 18. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
   
 19. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,471
  Trophy Points: 280
  sasa wamefanikiwa kudhoofisha chadema au wamejidhoofisha wenye pamoja na CCM.
   
 20. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
Loading...