IGP Sirro: Tutafuatilia kuhusu kifo cha Mengi ila tumalize msiba kwanza

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
9E64BF01-4CAC-4DEB-9783-26F5EBF7376C.jpeg


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Jeshi lake litafuatilia kwa kina maneno yote yanayosemwa mitandaoni kuhusu Kifo cha Reginald Mengi ili kubaini kama yanaukweli wowote ili sheria ichukue mkondo wake.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo baada ya kufika nyumbani kwa Dr Mengi ili kutoa Pole ya msiba.

”Mzee Mengi alikuwa mshauri mzuri sana kwenye masuala ya ulinzi na usalama pamoja na misaada midogo midogo kwa vijana wetu wanapokuwa na shida. Zaidi alikuwa ‘very humble’ mara zote alikuwa anajishusha sana.

"Yako mengi yanayoongelewa kwa sasa mitandaoni, lakini jambo la msingi tumalize kwanza msiba, hayo yanayozungumzwa mitandaoni tutafuatilia,” amesema Sirro.
 
Nani atakuwa mlalamikaji? Mitandaoni yalisemwa mengi kuhusu Ulimboka, Saanane, Azory na wengineo mbona hatukuona kauli ya polisi kuwahusu? Zaidi ya kuambiwa watu wasiulize.
Leteni ripoti ya MO dewji kwanza msitufanye watanzania wajinga sana
Aaah hivi yule aliyemtishia TL mitandaoni ashafatiliwa? "Hatufanyii Kazi masuala ya mitandaoni" ila kwa makada zinafanyiwa.
Hii awamu ni ya viongozi wa hovyo kuwahi kutokea ndani ya taifa letu. Kila Mkuu wa mhimili, idara, taasisi, wizara ni wa hovyo kuliko waliomtangulia na haikushangaza Mh. Zitto kudai kwamba hii ni zamu ya washamba na limbukeni. Hawa watu wanaliua taifa na wananchi tusipokaa macho watalizika kabisaaa! Kwa heri kisiwa cha amani...RIP!
 
Hii awamu ni ya viongozi wa hovyo kuwahi kutokea ndani ya taifa letu. Kila Mkuu wa mhimili, idara, taasisi, wizara ni wa hovyo kuliko waliomtangulia na haikushangaza Mh. Zitto kudai kwamba hii ni zamu ya washamba na limbukeni. Hawa watu wanaliua taifa na wananchi tusipokaa macho watalizika kabisaaa! Kwa heri kisiwa cha amani...RIP!

Shida wanaongozwa wana akili kuliko watawala.Maiti zimeamka.
 
Sioni kama hilo linaepukika, labda kama ameacha will.
Hata kama ameacha will, kuna situations ambazo upande mmoja unaweza kuzitumia dhidi ya upande mwingine. Kwa Mfano hizo tuhuma zinazosambaa, zinaweza kutumika dhidi ya huyo mdada aka loose custody ya watoto wake. Na hilo likitokea lake halipo. Another soap opera to come. Na hivyo uchaguzi mwaka kesho, basi polisi wameshapata tamthiliya nyingine. Watch this space!😃
 
Back
Top Bottom