IGP Sirro: Tutafuatilia kuhusu kifo cha Mengi ila tumalize msiba kwanza

Thank you IGP Sirro, uchunguzi makini kabisa unatakiwa, tujue ukweli, kale kadada sikaamini katu milele, usikute kafanya yake kachukue mali mapema..!! Haiwezekani mzee achoke vile aiseee.. Kulikoni? Ni ugonjwa wa Mungu tu au ugonjwa umesababishwa na mtu..!! Tunalia wote, lazima kama kuna mkono wa mtu au la tujue, thank you IGP wetu
 
Nani atakuwa mlalamikaji? Mitandaoni yalisemwa mengi kuhusu Ulimboka, Saanane, Azory na wengineo mbona hatukuona kauli ya polisi kuwahusu? Zaidi ya kuambiwa watu wasiulize.

Leteni ripoti ya MO dewji kwanza msitufanye watanzania wajinga sana

Aaah hivi yule aliyemtishia TL mitandaoni ashafatiliwa? "Hatufanyii Kazi masuala ya mitandaoni" ila kwa makada zinafanyiwa.

Hii ndo Tanzania yetu

Mtu akipigwa risasi hadhari hakuna uchunguzi,

Mtu akipotea hakuna uchunguzi

Ila mtu akifariki tena kwa maradhi halafu page za udaku zikavalia njuga uchunguzi unafanyika
 
Na naomba vyombo vya ulinzi vinavyosimamia maswala ya economic security vihakikishe kwamba IPP Group haiteteleki kutokana na chokochoko zozote za mirathi.

Kama hamna uzoefu wa kufanya kazi hiyo bila kuinationalize IPP mkajifunze Saudi Arabia au Russia haraka sana.
 
Kwani jiwe kamaliza ziara msiba wa mengi usije mfunika, vinginevyo utaendeshwa na serikali na yeye awe mgeni rasmi.
 
Tatizo la haya yote ni kwamba mzee alikua ni kipenzi cha wengi halafu akafa ghafla....
 
Mange kimambi mshenz sana, ndiye anayechafua na kuichonganisha hii familia mitandaoni. Wivu tu kwa K lyn

Maneno yote yale awe ametunga jamani? Basi atakuwa balaa kwenye utunzi ‍♀️. Mtu yoyote aliyeshuhudia zile videos za mzee na mapicha picha ya dakika za mwisho lazima atahoji kuwa kuna kitu hakikuwa sawa.
 
View attachment 1088004

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Jeshi lake litafuatilia kwa kina maneno yote yanayosemwa mitandaoni kuhusu Kifo cha Reginald Mengi ili kubaini kama yanaukweli wowote ili sheria ichukue mkondo wake.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo baada ya kufika nyumbani kwa Dr Mengi ili kutoa Pole ya msiba.

”Mzee Mengi alikuwa mshauri mzuri sana kwenye masuala ya ulinzi na usalama pamoja na misaada midogo midogo kwa vijana wetu wanapokuwa na shida. Zaidi alikuwa ‘very humble’ mara zote alikuwa anajishusha sana.

"Yako mengi yanayoongelewa kwa sasa mitandaoni, lakini jambo la msingi tumalize kwanza msiba, hayo yanayozungumzwa mitandaoni tutafuatilia,” amesema Sirro.
IGP Sirro aache upoyoyo, hivi Mo waliyemteka wao hajajua la kufanya, sasa ya Mengi aliyefia ughaibuni atayaweza?
 
Sasa kama itaonekana kauawawa wataenda kufukua mwili ili wapate ushahidi?
 
Nothing new with these people.
Mbona wengi waliotekwa na kupotea na wengine kufa na yakasemwa mitandaoni haikufuatiliwa?
Leo kwa sababu wanajua kuna fungu zuri ndo kauli zao hizi.

Sawa inaezekana kuna ukweli wa yanayosemwa bt lazma tujiulize Y only Mengi?
 
Back
Top Bottom