IGP Sirro, hali ya usalama barabarani inatisha. Chukua hatua haraka!

Benaya-

JF-Expert Member
Jul 31, 2019
4,417
7,609
Kwako Afande IGP Sirro.

Kwanza naomba nikupongeze kwa jitihada zako nyingi unazozifanya kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanakuwa salama pamoja na mali zao.

Najua kipindi hiki ni kigumu sana hasa tukizingatia wimbi jipya la mauaji ya kikatili yaliyoibuka hivi karibuni ambapo kumekuwa na mauaji mengi sana yanayisadikiwa yanasababishwa na wivu wa mapenzi, imani za ushirikina na visasi.

AJALI
Pamoja na hayo mauaji niliyoyataja hapo juu, kuna hili wimbi la ajali ambalo karibu kila baada ya siku 3 au wiki kunakuwa na tukio la ajali.

Kamanda Sirro, haya matukio ya ajali za kila mara linatia doa sana utumishi wako uliotukuka.
Ukifuatilia matukio haya kwa undani, chanzo kikuu ni mwendo kasi wa madereva.

Maeneo ambayo ajali za hivi karibuni ni mikoa ya:

1. Mbeya, mkoa huu ajali zimetokea zaidi ya mara 5 ndani ya miezi 2 na ajali ya mwisho mkoani humo ni leo Jumanne saa 10 jioni kwa lori kugonga basi dogo la abiria na zaidi ya watu 6 kupoteza maisha na majeruhi wengi.

2. Iringa, ilitokea ajali ya lori na basi dogo la abiria na zaidi ya watu 18 kupoteza maisha papo hapo.

3. Mikoa mingine ni Arusha, Singida, Tanga, Geita, Shinyanga, Morogoro, Manya na Dodoma ambayo imetokea wiki iliyopita.

Na ajali zote hizi zimeondoa maisha ya Watanzania na kusababisha ulemavu wa kudumu.
Hii haikubaliki na haikubaliki tena.

Ajali za barabarani huwa na vyanzo mbalimbali kama uzembe wa madereva, ubovu wa magari, mwendo kasi na ubovu wa barabara pia huwa ni chanzo.

Katika utafiti mdogo nilioufanya nimegundua zaidi ni mwendo kasi wa madereva pamoja na ubovu wa magari.

Haya makosa mawili niliyainisha yako ndani ya uwezo wa udhibiti wa jeshi la polisi.

NINI KIFANYIKE?
1. Nashauri mabadiliko ya mabadiliko ya Kamanda wa kikosi cha barabarani, pamoja na juhudi zake lakini nimegundua hana mbinu mpya za udhibiti wa ajali na

2. Kamanda huyu hana sauti ya kiungozi hivyo makamanda wa mikoa na wilaya hawaiheshimu sauti yake hivyo inaonyesha ameachiwa apambane mwenyewe.

3. Inaonyesha makamanda wa usalama barabarani hawana mwitikio kumpa ushirikiano Kamanda wa usalama barabarani taifa.

Katika hiki sitaingia ndani wewe una vyanzo vingi vya kupata taarifa ukifuatilia ndani ya siku moja utafahamu yaliyojificha nyuma mgomo huu baridi.

4. Ninashauri ikikupendeza umrudishe Kamanda Fortunatus Muslim, pamoja na madhaifu yake lakini yanarekebishika sio sawa na ya kamanda wa sasa.

Ksuli mbiu yake ya KAMATA au nyakua nyakua ilisaidia sana kupunguza ajali na aliwamudu makamanda wa mikoa na wilaya yaani RTO NA DTO

Vilevile sababu ya msingi iliyokufanya umuondoe kwenye nafasi yake...mvutano wake kati yake na aliyekuwa ZTO haupo tena...

Ikiwa yupo Kamanda unayeona atafaa zaidi pia itapendeza ilimradi pawepo na usalama barabarani Afande wangu.

Ninakutakia utumishi uliotukuka na umalizie utumishii huu kwa rekodi nzuri.



AJALI YAUA WATU SITA NA KUJERUHI WANNE WAKIENDA KUZIKA TABORAAJALI YAUA WATU SITA NA KUJERUHI WANNE WAKIENDA KUZIKA TABORA







 
Unaweza ukatuwekea vyanzo vya ajali hizo mkuu.

Ninachojua tu madereva wengi sahv ni sawa na wendawazim wanapokuwa Barabarani

Ova
 
Yaan hao wenye mavaz meupe ndio kama wamejipa majukumu wamebaki kuokoteza kama wanakusanya hela za mchezo, pita maeneo haya uone utafikiri kama wao vijumbe wa michezo.

1 Mwembe yanga

2:Darajani njia hii kama unaenda kutokea keko


3:pale relini (DEVIS CONNER) kama unakwenda Buza.


Lazima ajari zitokee sana, watu wamejipa majukumu mengine badala ya kusimamia
 
Yaan hao wenye mavaz meupe ndio kama wamejipa majukumu wamebaki kuokoteza kama wanakusanya hela za mchezo, pita maeneo haya uone utafikiri kama wao vijumbe wa michezo.

1 Mwembe yanga

2:Darajani njia hii kama unaenda kutokea keko


3:pale relini (DEVIS CONNER) kama unakwenda Buza.


Lazima ajari zitokee sana, watu wamejipa majukumu mengine badala ya kusimamia
Hili linafanyika nchi nzima na makusanyo hayo mgao unapanda juu hadi kwa kamanda wa usalama barabarani
 
Utafiti wangu unaonyesha magari ya Kichina aina ya HOWO yamehusika sana kwenye ajali. Hebu chunguzeni na fuatilia workmanship ya hayo magari especiaaly mfumo wa brake
 
Back
Top Bottom