Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

Tukubaliane na hali halisi, walimu wanaosubiri ajira mtaani ni wengi mno, na ambao wako mbioni kuhitimu na ni wengi, maelfu kwa maelfu, ukijumlisha na walio mtaani wanaweza kufika makumi ya maelfu.

Tusipochukua hatua hii, ipo siku idadi ya walimu itakuwa sawa na wanafunzi. Hivyo basi tujiulize, nini hupelekea mtu kusomea ualimu huku akijua kabisa tatizo lilipo la over-supply ya walimu? Je ni kukosa taarifa ya hali ya soko la ajira ya ualimu? Je, ni viwango vidogo vya ufaulu vinavyowekwa kama vigezo vya kusomea ualimu? Au ni nini hasa? Maana mishahara ni midogo, na mazingira ya kazi ni magumu pia, so then why mnasomea ualimu?

USHAURI:
1.) Vijana muende mkasome VETA, achaneni na ualimu, huku mtaani kuna demand kubwa ya watu wenye technical skills mbali mbali, huu mtego tuliowekewa na mkoloni kwa mfumo wake wa elimu umetutesa vya kutosha jamani, inatosha!!!! Enough is enough, huu uchawi wa mkoloni ufike mwisho, ni uchawi hatari sijawahi ona, ufike mwishoo!

2.) Serikali ipige kodi nzito mno bidhaa yeyote inayoagizwa toka nje ambayo pia inadhalishwa hapa nchini; tumeanza na fenicha toka China, angalau sasa vijana tunaona jinsi wanavyotusua kwenye biashara za useremala huko Instagram, vijana wamejiajiri na wanauza vitanda, masofa, makabati ya nguo , meza, dressing table n.k, kabla ya hapo waChina walikuwa wanaua kabisa hizi ajira na makabati yao ya pumba za maranda ya mbao. Na bado ongezeni kodi hizo fenicha ili walau vijana watakaoenda VETA wakitoka huko wajiachie na kujimwayamwaya kwenye nchi yao, tusiwanyanyase, pigeni kodi nzito!!!!

3.) Wachomelea mageti, Alluminium na glass nao naona wanakula kiulaini sana huko instagram, majengo mengi siku hizi watu wanaweka magrill ya chuma, glass na alluminium kwenye madirisha, vijana wanajimwayamwaya sana kwenye hii sekta, sasa kikubwa ni kuhakikisha wale wazalishaji wa ndani wa vitu kama alluminum , steel nk. wapewe upendeleo wa aina yake ili yale washindane na zinazotoka nje, vijana wapate ajira huko. Either way, vijana mkasomee huu utalaam wa kuchomelea mageti yale ya kisasa na madirisha ya alluminum, fungueni ma-account Instagram, tangazeni kwa fujo (sponsored ads) mle mema ya nchi yenu nyei, achaneni na ualimu.

3.) Washonaji wa seatcover za magari nao nimeona wanafaidi vinono huko instagram, sasa kikubwa yale maseat cover ya kutoka China yapigwe kodi nzito hadi waagizaji waone kizunguzungu, kiukweli huu utaalam inabidi vijana muende VETA mkasomee hii taaluma, inaitwa ‘CAR UPHOLSTERY’ aisee hii ni tamu, nadhani zile ngozi zinazotupwa vinginguti zitakuja kiwa lulu, maana Upholstery inakuwa tamu kupindukia ukitumia ngozi halisi, achana na yale maleather famba toka China, yaani gari inarekebishwa Dashboard inakuwa tamu hadi unatamani uilambe, seat covers za ngozi zinautamu wake jamani, Instagram watu wanafaidi sana kwenye hiki kitengo, achaneni na ualimu, tumieni akili vijana, magari yenye uchakavu wa interior ni mengi kupita maelezo, go where the demand is!

Nikiamka asubuhi naweka list ya vitengo kama kumi hivi ambapo watu wanalamba asali kiulaini huko instagram, ila kwenye mzinga wangu sitawaambia, bado nalamba lamba mwenyewe kwanza, nikishiba nitawaambia.

==================================

4.) Huko Instagram nimebaini pia kuwa kitengo cha BAKERY (CAKES) wananyonya vitamu kiulaini sana! Siku birthdays zimekuwa ni kitu cha kawaida, hadi watu wazima wanafanya birthday, na hii shughuli kiungo chake muhimu ni Keki, halikadhalika graduations za vyuo, maharusi nk; kote huko keki zinahitajika. Vifaa vya kutengeneza keki vinapatikana kwa urahisi na ni bei nafuu sana; mkosomee kozi za bakery jamani, tena ukija kubabatiza order za keki za harusi ndio utaona utamu wa bakeries, keki unatumia laki2 kutengeneza ila unauza laki8. Unatafuta hata bodaboda unaemuamini anakuwa anafanya deliveries sehemu mbalimbali, anapewa pesa on delivery anakuletea. Tena hii unaweza kufanya baking ya keki hata chumbani kwako, unatangaza Instagram kwa sponsored ads wateja wanamiminika tu, keki ziko on high demand jamani, tukajifunze BAKERY!

=============================
Update: 25/10/2021
Unaweza summarize kidogo uzi wako? Inaonekana una hoja ila uzi wako ni mrefu sana.
 
Mkuu kongole kwa kuleta bandiko hili, mimi ninavyoona serikali inatumia pesa nyingi sana kwenye kuelimisha watu maana mishahara inayotumika kuwalipa walimu peke yao ni pesa nyingi kweli kweli. Sasa, kwa maendeleo ya kiteknolojia tulipofikia mwalimu mmoja anao uwezo wa kufundisha wanafunzi kwenye madarasa hata 50 kutoka shule mbalimbali kwa wakati mmoja kwa kupitia tu njia ya TEHAMA.

Mimi ningeshauri serikali wawekeze kwenye hii njia ya TEHAMA kufundisha wanafunzi angalau kwa kuanzia ngazi ya sekondari. Hivi majuzi kulikuwa na uhaba mkubwa wa walimu wa physics na mathematics, wizara ikaona suluhisho ni kuajiri hao walimu ili kufidia upungufu. Lakini wangetumia njia ya TEHAMA walimu walewale wachache wangeweza kufundisha madarasa mengi zaidi kutoka shule nyingi kwa wakati mmoja. Ukipunguza mzigo wa kuajiri walimu wengi nguvu kubwa itatumuika kuajiri wataalamu wa maeneo mengine ya kimaendeleo na hivyo nchi kusonga mbele.​
Marekani imeendelea kwa TEHAMA haifanyi hivyo. Ukiambiwa uwiano ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi 40 maana yake sio kufundisha tu, mtaala wa elimu una mambo mengi.
 
Umeandika dhania tu, hivi bila huo ualimu ungeweza kuwasilisha mawazo yako hapa? Jamii inayoubeza ualimu katika dunia hii ya tatu ni ya kusikitikia sana. Wanaofundisha uko VETA siyo walimu? Suluhisho la ajira siyo kuzalisha bidhaa tu, bila mzunguko mzuri wa fedha kwa wananchi. Wanaojilipa mifungu minono wapo, watoto wao wanasoma ng'ambo elimu hii hii inayobezwa hapa nchini. Na wanaporudi mnaanza kuwatafutia idara kwa kuwaundia mikoa mipya, na wilaya mpya, wapate kula keki ya taifa kwa kijiko. Halafu, mna wahadaa watoto wetu, wajiajiri kwa kusoma, VETA, utadhani gharama za kununua vifaa mnawapa wakiisha hitimu, ni watoto wengi nawaona wako vijiweni baada ya kuhitimu VETA, kwa kukosa mtaji na vifaa vya kujiajiri, ambavyo jumla yake siyo chini ya shilingi milioni moja na zaidi za Kitanzania. Yaani mnatengeneza tatizo juu ya tatizo lingine baadala ya kuyatatua. Muda ni mwalimu mzuri na umuhimu somo lake ujulikana baadae. Somalia, ni mfano mzuri, kwa wote wajipendeleao na koo zao wawapo madarakani.
 
Spot on....vyuo vianzishe vibadili mitaala ya wakati wa uhuru ambapo nchi ilikuwa inatafuta wafanyakazi wa serikali na mfumo.ulikuwa ujamaa, sasa waangalie zaidi skills za mtu kujiajiri na sio kuajiriwa.

Bila vyuo kubadili mfumo kwakweli vijana wanaendelea kuwa wafungwa wa fikra kisa degree....
 
Ukweli mtupu umasikini mkubwa unachangiwa na sera mbalimbali ...sasa serikali haizuii bidhaa fulani fulani ambazo tunauwezo nazo. Hata kodi hazipigwi ipasavyo halafu utegemee uchumi ukue na maarifa kwa wananchi wako? Imekua kama shamba la bibi. Takataka kibao hadi stick za meno...vijana watajiajiri vipi...nchi yenye rutuba kama hii inakosa ma plantation ya maana. Wanakata kila kijana akimaliza chuo atafutiwe mchongo mahali ofisini apachikwe na ndugu zake ale maisha.,...umasikini huu kwa vijana unasababishwa na vingi sana
Watazuiaje wakati wao na familia zao ndo wanaoingiza hayo makontena toka China?
 
Umeandika dhania tu, hivi bila huo ualimu ungeweza kuwasilisha mawazo yako hapa? Jamii inayoubeza ualimu katika dunia hii ya tatu ni ya kusikitikia sana. Wanaofundisha uko VETA siyo walimu? Suluhisho la ajira siyo kuzalisha bidhaa tu, bila mzunguko mzuri wa fedha kwa wananchi. Wanaojilipa mifungu minono wapo, watoto wao wanasoma ng'ambo elimu hii hii inayobezwa hapa nchini. Na wanaporudi mnaanza kuwatafutia idara kwa kuwaundia mikoa mipya, na wilaya mpya, wapate kula keki ya taifa kwa kijiko. Halafu, mna wahadaa watoto wetu, wajiajiri kwa kusoma, VETA, utadhani gharama za kununua vifaa mnawapa wakiisha hitimu, ni watoto wengi nawaona wako vijiweni baada ya kuhitimu VETA, kwa kukosa mtaji na vifaa vya kujiajiri, ambavyo jumla yake siyo chini ya shilingi milioni moja na zaidi za Kitanzania. Yaani mnatengeneza tatizo juu ya tatizo lingine baadala ya kuyatatua. Muda ni mwalimu mzuri na umuhimu somo lake ujulikana baadae. Somalia, ni mfano mzuri, kwa wote wajipendeleao na koo zao wawapo madarakani.
Umejibu kisicho hojiwa, una elimu duni sana, hata kama umesoma.
 
Umejibu kisicho hojiwa, una elimu duni sana, hata kama umesoma.
Mimi n mwalimu tena wa history na literature lakini nafanya kazi kwenye NGO inayohusika na masuala ya kuelimisha jamii tatizo watu wamekariri kuwa mwalimu basi n kwenda kufundisha tu shuleni hy n mawazo mgando
 
Unaendelea kujibu nisicho hoji. Mimi nimesema watu wasisomee ualimu kwa sasa kwa sababu 1,2,3. Wewe unakuja kusema nimedharau ualimu. Umesoma lakini elimu yako ni duni.
 
Unaendelea kujibu nisicho hoji. Mimi nimesema watu wasisomee ualimu kwa sasa kwa sababu 1,2,3. Wewe unakuja kusema nimedharau ualimu. Umesoma lakini elimu yako ni duni.
We mwenyewe uwasilishaji wako m mbovu kajifunze communication skills unatumia command,badala ya kipropose kitu Elimu yako pia n duni kwasababu haikusaidii chochote zaidi ya kukurupuka,Fanya research ndo utoe proposal usikurupuke tu.
 
Sasa hapa umeandika nini, na unategemea nijibu nini. Hilo ni wazo sio lazima.
 
Back
Top Bottom