Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,063
40,724
Tukubaliane na hali halisi, walimu wanaosubiri ajira mtaani ni wengi mno, na ambao wako mbioni kuhitimu na ni wengi, maelfu kwa maelfu, ukijumlisha na walio mtaani wanaweza kufika makumi ya maelfu.

Tusipochukua hatua hii, ipo siku idadi ya walimu itakuwa sawa na wanafunzi. Hivyo basi tujiulize, nini hupelekea mtu kusomea ualimu huku akijua kabisa tatizo lilipo la over-supply ya walimu? Je ni kukosa taarifa ya hali ya soko la ajira ya ualimu? Je, ni viwango vidogo vya ufaulu vinavyowekwa kama vigezo vya kusomea ualimu? Au ni nini hasa? Maana mishahara ni midogo, na mazingira ya kazi ni magumu pia, so then why mnasomea ualimu?

USHAURI:
1.) Vijana muende mkasome VETA, achaneni na ualimu, huku mtaani kuna demand kubwa ya watu wenye technical skills mbali mbali, huu mtego tuliowekewa na mkoloni kwa mfumo wake wa elimu umetutesa vya kutosha jamani, inatosha!!!! Enough is enough, huu uchawi wa mkoloni ufike mwisho, ni uchawi hatari sijawahi ona, ufike mwishoo!

2.) Serikali ipige kodi nzito mno bidhaa yeyote inayoagizwa toka nje ambayo pia inadhalishwa hapa nchini; tumeanza na fenicha toka China, angalau sasa vijana tunaona jinsi wanavyotusua kwenye biashara za useremala huko Instagram, vijana wamejiajiri na wanauza vitanda, masofa, makabati ya nguo , meza, dressing table n.k, kabla ya hapo waChina walikuwa wanaua kabisa hizi ajira na makabati yao ya pumba za maranda ya mbao. Na bado ongezeni kodi hizo fenicha ili walau vijana watakaoenda VETA wakitoka huko wajiachie na kujimwayamwaya kwenye nchi yao, tusiwanyanyase, pigeni kodi nzito!!!!

3.) Wachomelea mageti, Alluminium na glass nao naona wanakula kiulaini sana huko instagram, majengo mengi siku hizi watu wanaweka magrill ya chuma, glass na alluminium kwenye madirisha, vijana wanajimwayamwaya sana kwenye hii sekta, sasa kikubwa ni kuhakikisha wale wazalishaji wa ndani wa vitu kama alluminum , steel nk. wapewe upendeleo wa aina yake ili yale washindane na zinazotoka nje, vijana wapate ajira huko. Either way, vijana mkasomee huu utalaam wa kuchomelea mageti yale ya kisasa na madirisha ya alluminum, fungueni ma-account Instagram, tangazeni kwa fujo (sponsored ads) mle mema ya nchi yenu nyei, achaneni na ualimu.

3.) Washonaji wa seatcover za magari nao nimeona wanafaidi vinono huko instagram, sasa kikubwa yale maseat cover ya kutoka China yapigwe kodi nzito hadi waagizaji waone kizunguzungu, kiukweli huu utaalam inabidi vijana muende VETA mkasomee hii taaluma, inaitwa ‘CAR UPHOLSTERY’ aisee hii ni tamu, nadhani zile ngozi zinazotupwa vinginguti zitakuja kiwa lulu, maana Upholstery inakuwa tamu kupindukia ukitumia ngozi halisi, achana na yale maleather famba toka China, yaani gari inarekebishwa Dashboard inakuwa tamu hadi unatamani uilambe, seat covers za ngozi zinautamu wake jamani, Instagram watu wanafaidi sana kwenye hiki kitengo, achaneni na ualimu, tumieni akili vijana, magari yenye uchakavu wa interior ni mengi kupita maelezo, go where the demand is!

Nikiamka asubuhi naweka list ya vitengo kama kumi hivi ambapo watu wanalamba asali kiulaini huko instagram, ila kwenye mzinga wangu sitawaambia, bado nalamba lamba mwenyewe kwanza, nikishiba nitawaambia.😂

==================================

4.) Huko Instagram nimebaini pia kuwa kitengo cha BAKERY (CAKES) wananyonya vitamu kiulaini sana! Siku birthdays zimekuwa ni kitu cha kawaida, hadi watu wazima wanafanya birthday, na hii shughuli kiungo chake muhimu ni Keki, halikadhalika graduations za vyuo, maharusi nk; kote huko keki zinahitajika. Vifaa vya kutengeneza keki vinapatikana kwa urahisi na ni bei nafuu sana; mkosomee kozi za bakery jamani, tena ukija kubabatiza order za keki za harusi ndio utaona utamu wa bakeries, keki unatumia laki2 kutengeneza ila unauza laki8. Unatafuta hata bodaboda unaemuamini anakuwa anafanya deliveries sehemu mbalimbali, anapewa pesa on delivery anakuletea. Tena hii unaweza kufanya baking ya keki hata chumbani kwako, unatangaza Instagram kwa sponsored ads wateja wanamiminika tu, keki ziko on high demand jamani, tukajifunze BAKERY!

=============================
Update: 25/10/2021

==========================
Update: 10/08/2022

===========================
Update: 05/03/2023

Serikali imetoa nafasi kwa vijana wote wa kuanzia miaka 18 - 35 kusomeshwa bure kwenye vyuo vya ufundi stadi VETA, unatakiwa kwemda kuchukua fomu na kuijaza tu, serikali itakulipia ada kwa 100% , walemavu watapewa kipaumbele

==========================
Update: 08/02/2024

Haya, nadhani sasa tunaelewana..
1D8574DF-82A7-40B5-87D0-7A1B3538A90A.jpeg
 
Shida ni mfumo wa elimu.

Tubadilishe mfumo wa elimu.

Haiwezekani mtu anasoma hadi chuo kikuu anamaliza halafu hana skills yoyote, hiyo ni elimu ama takataka?

Tupunguze miaka ya masomo shuleni, tuongeze vyuo vya ufundi na stadi za maisha.

Shida iko kwenye mfumo wa elimu, lakini najua soon huu mfumo uta collapse.
 
Ukweli mtupu umasikini mkubwa unachangiwa na sera mbalimbali ...sasa serikali haizuii bidhaa fulani fulani ambazo tunauwezo nazo. Hata kodi hazipigwi ipasavyo halafu utegemee uchumi ukue na maarifa kwa wananchi wako? Imekua kama shamba la bibi. Takataka kibao hadi stick za meno...vijana watajiajiri vipi...nchi yenye rutuba kama hii inakosa ma plantation ya maana. Wanakata kila kijana akimaliza chuo atafutiwe mchongo mahali ofisini apachikwe na ndugu zake ale maisha.,...umasikini huu kwa vijana unasababishwa na vingi sana
 
Mi nadhani upepo huwa unabadilikaga wenyewe kutokana na namna serikali inavoajiri na fursa za kujiajiri kwa kada husika.

So wahitimu kidato cha nne/ sita ni wengi, ko walimu wataenda wengi, na saiz upepo unahamia course za afya.. so clinical medicine wataenda wengi, pharmacy wengi, nurses wengi.

Hii inatokana na serikali inatoa fursa kwa kada zipi.

Mfano kama serikali ikaanza kuajiri kwa kasi Wataalamu wa ufugaji nyuki, tegemea wazazi na walezi kuanza ku direct vijana wao wasomee course husika sababu wameona serikali yao inaajiri sana watu wa kada hiyo.

Ni maoni tu
 
Mi nadhani upepo huwa unabadilikaga wenyewe kutokana na namna serikali inavoajiri na fursa za kujiajiri kwa kada husika..
So wahitimu kidato cha nne/ sita ni wengi, ko walimu wataenda wengi, na saiz upepo unahamia course za afya.. so clinical medicine wataenda wengi, pharmacy wengi, nurses wengi..
Hii inatokana na serikali inatoa fursa kwa kada zipi..

Mfano kama serikali ikaanza kuajiri kwa kasi Wataalamu wa ufugaji nyuki, tegemea wazazi na walezi kuanza ku direct vijana wao wasomee course husika sababu wameona serikali yao inaajiri sana watu wa kada hiyo.

Ni maoni tu
Wewe ndo umeandika mkuu. Asante sana
 
Umeandika ukweli mtupu. Una akili sana ndugu yangu
Tukubaliane na hali halisi, walimu wanaosubiri ajira mtaani ni wengi mno, na ambao wako mbioni kuhitimu na ni wengi, maelfu kwa maelfu, ukijumlisha na walio mtaani wanaweza kufika makumi ya maelfu.

Tusipochukua hatua hii, ipo siku idadi ya walimu itakuwa sawa na wanafunzi. Hivyo basi tujiulize, nini hupelekea mtu kusomea ualimu huku akijua kabisa tatizo lilipo la over-supply ya walimu? Je ni kukosa taarifa ya hali ya soko la ajira ya ualimu? Je, ni viwango vidogo vya ufaulu vinavyowekwa kama vigezo vya kusomea ualimu? Au ni nini hasa? Maana mishahara ni midogo, na mazingira ya kazi ni magumu pia, so then why mnasomea ualimu?

USHAURI:
1.) Vijana muende mkasome VETA, achaneni na ualimu, huku mtaani kuna demand kubwa ya watu wenye technical skills mbali mbali, huu mtego tuliowekewa na mkoloni kwa mfumo wake wa elimu umetutesa vya kutosha jamani, inatosha!!!! Enough is enough, huu uchawi wa mkoloni ufike mwisho, ni uchawi hatari sijawahi ona, ufike mwishoo!

2.) Serikali ipige kodi nzito mno bidhaa yeyote inayoagizwa toka nje ambayo pia inadhalishwa hapa nchini; tumeanza na fenicha toka China, angalau sasa vijana tunaona jinsi wanavyotusua kwenye biashara za useremala huko Instagram, vijana wamejiajiri na wanauza vitanda, masofa, makabati ya nguo , meza, dressing table n.k, kabla ya hapo waChina walikuwa wanaua kabisa hizi ajira na makabati yao ya pumba za maranda ya mbao. Na bado ongezeni kodi hizo fenicha ili walau vijana watakaoenda VETA wakitoka huko wajiachie na kujimwayamwaya kwenye nchi yao, tusiwanyanyase, pigeni kodi nzito!!!!

3.) Wachomelea mageti, Alluminium na glass nao naona wanakula kiulaini sana huko instagram, majengo mengi siku hizi watu wanaweka magrill ya chuma, glass na alluminium kwenye madirisha, vijana wanajimwayamwaya sana kwenye hii sekta, sasa kikubwa ni kuhakikisha wale wazalishaji wa ndani wa vitu kama alluminum , steel nk. wapewe upendeleo wa aina yake ili yale washindane na zinazotoka nje, vijana wapate ajira huko. Either way, vijana mkasomee huu utalaam wa kuchomelea mageti yale ya kisasa na madirisha ya alluminum, fungueni ma-account Instagram, tangazeni kwa fujo (sponsored ads) mle mema ya nchi yenu nyei, achaneni na ualimu.

3.) Washonaji wa seatcover za magari nao nimeona wanafaidi vinono huko instagram, sasa kikubwa yale maseat cover ya kutoka China yapigwe kodi nzito hadi waagizaji waone kizunguzungu, kiukweli huu utaalam inabidi vijana muende VETA mkasomee hii taaluma, inaitwa ‘CAR UPHOLSTERY’ aisee hii ni tamu, nadhani zile ngozi zinazotupwa vinginguti zitakuja kiwa lulu, maana Upholstery inakuwa tamu kupindukia ukitumia ngozi halisi, achana na yale maleather famba toka China, yaani gari inarekebishwa Dashboard inakuwa tamu hadi unatamani uilambe, seat covers za ngozi zinautamu wake jamani, Instagram watu wanafaidi sana kwenye hiki kitengo, achaneni na ualimu, tumieni akili vijana, magari yenye uchakavu wa interior ni mengi kupita maelezo, go where the demand is!

Nikiamka asubuhi naweka list ya vitengo kama kumi hivi ambapo watu wanalamba asali kiulaini huko instagram, ila kwenye mzinga wangu sitawaambia, bado nalamba lamba mwenyewe kwanza, nikishiba nitawaambia.

==================

Angalizo: Marufuku ku-comment bila kusima uzi wote, narudia, Marufuku!
 
Kwa nini watu kama nyie mlio na maono makubwa hampati nafasi ya kuwa viongozi wa juu? Hata mkibahatika kuwa viongozi maono yote huisha!sijui aliyetuloga ni nani.

Umeandika vema sana ndugu,ualimu umekuwa ni janga kubwa, mbaya zaidi hata walio kwenye mfumo hawathaminiwi tena kutokana na wingi wao.
 
Mkuu kongole kwa kuleta bandiko hili, mimi ninavyoona serikali inatumia pesa nyingi sana kwenye kuelimisha watu maana mishahara inayotumika kuwalipa walimu peke yao ni pesa nyingi kweli kweli. Sasa, kwa maendeleo ya kiteknolojia tulipofikia mwalimu mmoja anao uwezo wa kufundisha wanafunzi kwenye madarasa hata 50 kutoka shule mbalimbali kwa wakati mmoja kwa kupitia tu njia ya TEHAMA.

Mimi ningeshauri serikali wawekeze kwenye hii njia ya TEHAMA kufundisha wanafunzi angalau kwa kuanzia ngazi ya sekondari. Hivi majuzi kulikuwa na uhaba mkubwa wa walimu wa physics na mathematics, wizara ikaona suluhisho ni kuajiri hao walimu ili kufidia upungufu. Lakini wangetumia njia ya TEHAMA walimu walewale wachache wangeweza kufundisha madarasa mengi zaidi kutoka shule nyingi kwa wakati mmoja. Ukipunguza mzigo wa kuajiri walimu wengi nguvu kubwa itatumuika kuajiri wataalamu wa maeneo mengine ya kimaendeleo na hivyo nchi kusonga mbele.​
 
4.) Huko Instagram nimebaini pia kuwa kitengo cha BAKERY (CAKES) wananyonya vitamu kiulaini sana! Siku birthdays zimekuwa ni kitu cha kawaida, hadi watu wazima wanafanya birthday, na hii shughuli kiungo chake muhimu ni Keki, halikadhalika graduations za vyuo, maharusi nk; kote huko keki zinahitajika. Vifaa vya kutengeneza keki vinapatikana kwa urahisi na ni bei nafuu sana; mkosomee kozi za bakery jamani, tena ukija kubabatiza order za keki za harusi ndio utaona utamu wa bakeries, keki unatumia laki2 kutengeneza ila unauza laki8.

Unatafuta hata bodaboda unaemuamini anakuwa anafanya deliveries sehemu mbalimbali, anapewa pesa on delivery anakuletea. Tena hii unaweza kufanya baking ya keki hata chumbani kwako, unatangaza Instagram kwa sponsored ads wateja wanamiminika tu, keki ziko on high demand jamani, tukajifunze BAKERY!
 
Back
Top Bottom