Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,252
Hali mtaani inatisha sana, karibu kila kitu kimepanda bei, kuanzia maduka ya ujenzi hadi maduka ya vyakula, hadi pipi zimepanda bei.
Kipato cha Mtanzania kiko palepale na asilimia kubwa ya vijana hawana ajira wala kipato chochote.
Sahivi ukininunua mafuta ya elfu moja ya kupikia hayatoshi kabisa kwenye mboga. Na baadhi ya maduka ya mitaani yameaacha kabisa kuuza mafuta reja reja kutokana na madai kuwa wanashindwa wauzeje kwani wateja wao Wamekuwa wakilalamika kuwa kupunjwa na Kuona kuwa wanaibiwa.
Kwenye kilimo huko wakulima wanalalamika jua limekuwa kali hakuna mvua wala mavuno, huku pembejeo zikiwa hazikamatiki kwa bei.
Kwa ujumla hali ni tete tena sanana wananchi wamekuwa wapole kupita kiasi.
Viongozi wetu wametulia tulii kama hakuna wanachojua wala kuona vile,
Kwa serikali inayojali wananchi wake tayari wangeshafanya namna yoyote iwayo kama vile kupunguza kodi kwa bidhaa zote, na haswa upande wa kodi ya mafuta na vipuri vya magari bandarini.
Kwa vile serikali yetu haipendi kukosolewa wala kunyooshewa kidole basi wananchi tutaendelea kutaabika tu.
Lakini kiukweli hali mtaani sio nzuri kwa Mwananchi wa kawaida.
Majani ya chai yale ya 600 leo ni 700,novida ilikuwa 500 leo ni 600, sabuni kipande leo ni 600, mikate nayo imepanda bei, kutokana na ngano kupanda bei, nk. Vifaa vya ujenzi ndo usiseme.
Serikali iko kimya ka hawaoni au hawajui ya kuwa wananchi wanaumia?