Ifike hatua niachwe tu!

dawa yenu

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
2,690
2,000
Basi bwana nikajua nimepata, kumbe nimepatikana kinoma kinoma aisee! Huyu binti nilikuwaga namuona tu hapa kitaa na mikato yake ya akina Kim Kardashian utafikiri ameshuka toka state last night! Wa moto hatari anaongea kiswahili flani cha Kimamtoni huwezi amini! Ana life lake hilo standard za Western Union yaani Barclays kabisa achana na hizi za Mkombozi akaunti!

Huku na huku nikajikuta tu namuelewa kila nikimuona moyo unakosa utulivu nikasema cha kufia nini acha nijilipue! Nikatega mingo, binti akajaa wavuni Sasa sijui yeye ndio aliingia kwenye anga zangu au Mimi ndio niliingia kwenye anga zake but all in all viliumana!

Utamu wa penzi jipya ukawa utamu kweli! Yaani vile nikiwa nae najiona kabisa nipo level nyingine! Sasa shamra shamra za penzi jipya zikaisha ikabidi tuingie kwenye true life yaani maisha ya kweli! Aisee sikudanganyi sijawahi kuona mdada anapiga mizinga Kama huyu manzi wangu! Hakuna cha Kim Kardashian wala Kim Kadashiani, hovyo kabisa! Anapiga mziga kuliko serikali yetu, halafu akipewa hela anajifanya eti maendeleo yake yanatoka na hustle zake tu yaani pesa za ndani! Anajiita malkia wa nguvu, malkia wa nguvu halafu unategemea donor country!!!

Mara "Babe nmeixhiwa credit nitumie bx" utamtumia vocha baada ya dakika kumi,
"Babe natk niende town nitumie hata 10k ikanisaidie" yaani Hadi siku inaisha hizo buku mbili mbili buku kumi ninazotuma bora ningeenda kuweka vikoba tu ingenilipa mwisho wa mwaka! Halafu mbaya zaidi anaona kupewa hela ni haki yake yaani nilizaliwa kumpa hela yeye, Sasa najiuliza tukitoa mbususu yake kwenye mahusiano yetu ana faida gani nyingine? Nakosa jibu!

Mbaya zaidi hajui kuandika penye S anaweka X hivi mtu wa hivyo anashindwa kuniua kweli? Hapana nimechoka kwa kweli, wiki hii haiishi ataniacha tu! Imefika hatua naona Bora niachwe hakuna namna!

Pia soma: Wajua jinsi ya kumdhibiti mpenzi anayepiga mizinga?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom