Ifakara: Dr. Slaa Hakusalimiana na JK! Kwanini?

@dr slaa

Tunatumaini upo online tungependa tupate undani wa jambo hili lakini wengi wetu tunaamini kuwa hakuna chuki kati yenu ingawa kuna mazingira ya kuibiana kura za urais , lakini hizo ndizo siasa kwani michezo ya kijanja ndio sifa kuu ya siasa
 
Update.
Nimekuta na Dr. Slaa mahali na kupata fursa ya kumuuliza yale maswali yangu yaliyobakia.

Amenithibitishia kuwa hajawahi kumkacha Jk hata mara moja, bali imekuwa ikitokea by chances tuu hawajakutana!,

Hivyo ile dhana yangu ya muendelezo wa misuso nimeifuta.

Asanteni kwa kunielewa!.

Pasco!.

@Pasco
Mbona siku hizi unaleta mambo mezani kisha ukitikisiwa kiodogo unanaadika kauli au dhana yangu nimeifuta. Usiwe mwoga wa kusimamia unachoamini la sivyo jitahidi uwe makini na uchambuzi wako wa mambo.Haya mambo ya kuta futa yatakufany uonekane mbabaishaji na wengine ndio tutasema............

Sasa kama wewe ndio kidogo unajua ABC za unadishi uko hivi sisi wengine .

Kituko kigine ukaandika kuhusu michango ya wana JF ya msiba wa RM ........... Badilika Aisee........

Yaani thread zako kwenye huu msiba wa Regia . Nikichanganya na comment zako za EL mhhh.

Na hii ya EL nayo unasubiriwa ufute kauli zako.
teh teh teh
 
@dr slaa
Tunatumaini upo online tungependa tupate undani wa jambo hili lakini wengi wetu tunaamini kuwa hakuna chuki kati yenu ingawa kuna mazingira ya kuibiana kura za urais , lakini hizo ndizo siasa kwani michezo ya kijanja ndio sifa kuu ya siasa
Undani wa jambo gani na hiyo "tu..." ndiyo unawahusisha watu gani hao? Mbona hekima ni kama zimehama ndani ya vichwa vingi tu humu. Yaani Dr. Slaa unamtaka aje atupatie undani hasa wa nini, porojo ? What's wrong with you people ? Mnageuza JF inakuwa kama kijiwe cha kahawa ! Nina hakika Dr. ana mambo muhimu zaidi ya kushughulikia na si huu upuuzi.
 
kwa hivyo baada ya kuambiwa Hivyo akaondoka au kaondoshwa? maziko si yalikuwa ya Chadema, Jk ananguvu gani ktk msiba ule/

Jamani hv kwa niniwatu huwa tunakuwa wagumu kuelewa?kumbuka kuwa Regia alikuwa mbunge wa chadema katika bunge la jamuhuri ya muungano wa tz ambalo lipo chini ya serikari ya jk hvyo msiba ule uliratibiwa na bunge na ndio maana hata jeneza lilifunikwa kwa bendela ya taifa na waka si ya chadema walmagamba.
 
Pasco,
Watu wengi wanakuheshimu sana hapa ndani. Mimi ni mmoja wao.
Nadhani utajifunza kuwa kuandikahapa bila research kuna impact!....Negative impact!...suppose ungekuwa umeongea kwa krefu na Dr.Slaa ndio uje kuandika, usingeandika ile biasness ya kwenye original thread!
Umenisikitisha sana kwa vile unatafuta mambo ambayo yana'insinuate chuki kati ya wakuu wa vyama, hadi level ya wafuasi!.
Tumia kalamu kujenga ndugu Pasco!
Mkuu Paka Jimmy, heshima mbele. Nilikufahamu vizuri wakati wa msiba wa Sipo. Wewe ni miongoni mwa jf pioneers wa jf kusaidiana kwenye shida na raha na hata tulipopata msiba huu, nikahamasisha jf tujiorganise tuhudhurie maziko na nikamsisitizia Max kama PK aliweza kwenye msiba wa Sipo kwa nini tushindwe?!.

Hivyo safari yangu Ifakara, you are my inspiration!. Thanks far that!.

Nakushukuru kwa kuniheshimu, heshima hailazimishwi inakuwa earned kwa michango yako humu jukwaani au lost kwa kupost pumba, crap au utumbo. Hivyo kama nimepost crap, nitajivunjia heshima mwisho nitabaki crap!.

Hoja ya kuitumia kalamu yangu kujenga badala ya kubomoa ni hoja ya msingi ila katika ujenzi imara, kuna wakati unatakiwa kubomoa ili ku reinforce na hivyo kuwa imara zaidi!.

Kama una bondia wako ambaye unapenda ashinde pambano, utamuandaa kwa mapambano ya utangulizi na mabondia wa ukweli ambao watamkong'ota kisawasawa ili kumuimarisha na sio kumpa mazoezi na mabondia weak ili wasimuumize ukifikiri kumuhurumia ndio kumsaidia kumbe ni kumuangamiza!.

Nakiri kuwa ni kweli mimi ni miongoni mwa wakosoaji wakuu wa Chadema na pia ni mkosoaji mzuri wa Dr. Slaa ndio maana nampigia chapuo Lowassa!. Dr. Slaa kwa Lowassa ni cha mtoto, hivyo ndio mwana wetu, sasa mchelea mwana kulia, hulia yeye!. Kuliko mimi 2015 nilie tena bora chapa bakora za nguvu Dr. Slaa!.

PJ nakuhakikishia japo mimi naonekana ndio mbomoaji, amini nakuambia sisi wabomoaji humu ndio wajengaji na hao mnao waona kama ndio wajengaji ni maneno mengi ila matupu vitendo sifuri!.

Nakuhakikishia wakati muafaka ukifika mtanishukuru kwa kuwapitisha viongozi wenu wa Chadema kwenye tanuru la moto!.
 
eti
ndio maana nampigia chapuo Lowassa!. Dr. Slaa kwa Lowassa ni cha mtoto,
sijakusoma hapa Pasco,unajaribu kulinganisha dinosour (dr Slaa) na kenge. labda unipe dondoo kidogo kuwa ni cha mtoto kivipi
samahani kwa usumbufu
 
Pasco nakuomba sana uache ushabiki pindi unapotoa thread ambazo unajua zitagusa wengi. Ni bora uka base kwenye facts kuliko matakwa na utashi.

Siyo mara ya kwanza kuinanga CDM jukwaani, lakini ukiona hali inataka kuwa tete unatumia ujanja ujanja kufanya conclusion. Acha ubabaishaji haukusaidiii.
Mkuu Losambo, bahati mbaya mimi sio nwana Chadema kusema mkifanya madudu tukosoane kwenye vikao!. Mimi ni Pasco wa jf tunakutana hapa ukumbini tunaambiana ukweli, nyinyi na Chadema yenu mna hiari mmeze au mteme hiyo ni juu yenu!. Naahidi nitaendelea kuikosoa Chadema mpaka ikae kwenye mstari ulionyooka!.
Moja ya matatizo makubwa ya Chadema ni wafuasi wanaowaabudu viongozi wao kama miungu watu!. Kwangu mimi viongozi wetu ni binadamu wakifanya ndivyo sivyo wanaambiwa tuu!.
 
bye-regia.jpg
Askari wa Bunge wakiuingiza kaburini mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema) Regia Mtema wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Ipangalala Ifakara mkoani Morogoro jana. Picha na Juma Mtanda

AKWEPA KUKAA JUKWAA KUU, WENGI WAMZIKA REGIA
Juma Mtanda na Shakila Nyerere, Ifakara
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, jana alimkwepa tena Rais Jakaya Kikwete safari hii ikiwa katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema yaliyofanyika katika Kijiji cha Lipangalala.Tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana.

Katika hafla ya kutangazwa matokeo ya urais iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, Dk Slaa hakuhudhuria tofauti na ilivyokuwa kwa waliokuwa wagombea wenzake wote.

Jana, Dk Slaa tofauti na viongozi wenzake wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, hakutaka kujiweka katika mazingira ambayo yangemkutanisha na Rais Kikwete katika mazishi hayo.
Nyumba kulikofanyika shughuli za awali za mazishi, waandalizi waliandaa majukwaa mawili, moja maalum kwa ajili ya wabunge huku jingine likiwa ni maalumu kwa ajili ya viongozi wakuu ambalo alikaa Mbowe, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe.

Mbali ya kukaa viongozi hao, kulikuwa na nafasi ambayo ilikuwa imetengwa maalumu kwa ajili ya Rais. Mbali ya nafasi hiyo, pia kulikuwa na kiti ambacho ilitegemewa kwamba Dk Slaa angekalia.
Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Chadema alikikwepa na kwenda kujichanganya katika jukwaa la wabunge na kiti hicho kubaki bila ya kuwa na mtu.

Hata hivyo, Rais Kikwete hakuweza kufika nyumbani hadi mwili wa marehemu Regia ulipopelekwa katika Viwanya vya Viungani ambako uliagwa na mamia ya waombolezaji.

Uwanjani hapo nako kulikuwa na majukwaa mawili. Kama ilivyokuwa nyumbani, jukwaa moja lilikuwa la wabunge na jingine la viongozi wa ngazi za juu lakini bado, Dk Slaa alilikwepa jukwaa hilo ambalo Rais alitarajiwa kuwa angefikia. Rais hakuweza kufika Viungani pia.

jk-udongo.jpg
Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema) Regia Mtema wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Ipangalala Ifakara mkoani Morogoro jana. Picha na Juma Mtanda

Baadaye wakiwa eneo la mazishi, Rais Kikwete alifika na kushiriki tukio hilo na kisha kusalimiana na wabunge mbalimbali na viongozi waliokuwa wamefika akiwemo Mbowe, Mbunge wa Rombo Joseph Selasini, Zitto na viongozi wengine lakini Dk Slaa hakuonekana.

Ilitegemewa kuwa tukio hilo la msiba lingewaleta wanasiasa hao lakini hadi Rais Kikwete alipoondoka hakuna mahali ambako walisalimiana.
Mbali ya tukio hilo, hata katika hafla mbalimbali ambazo viongozi wa Chadema wamekuwa wakialikwa ikiwemo Ikulu, Dk Slaa hakuwahi kuhudhuria.

Novemba mwaka jana viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe, walifanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu ya Dar es Salaam kujadili suala la Katiba Mpya, lakini Dk Slaa hakuhudhuria.


Chadema wahaha
Wakati viongozi wa Chadema wakihaha kumaliza mgogoro ndani ya chama hicho wilayani Kilombero, Pacha wa marehemu Regia, Remigia Mtema amesema ndugu yake Regia alikuwa akipeleka malalamiko kwa Dk Slaa mara kadhaa kuomba asuluhishe bila mafanikio.

Hata hivyo, Remigia alisema marehemu Regia alikuwa amepanga kuonana tena na Dk Slaa katika siku za hivi karibuni kumweleza kinachoendelea.

Akizungumzia suala hilo, Dk Slaa alisema alishaanza kushughulikia mgogoro huo lakini msiba huo ndiyo uliomkwamisha.

"Ni kweli nimekuwa nikielezwa tatizo hilo na tayari nilishaanza kulifanyika kazi ila sasa siwezi kusema suala hilo limefikia wapi kwani wote tuko kwenye mazishi," alisema.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wabunge wa Chadema waliotangulia kufika katika msiba huo, Mchungaji Peter Msigwa, Ezekia Wenje na Lucy Owenya, walikutana na uongozi wa kata wa Chadema ili kumaliza mgogoro huo.

Katibu mwenezi wa Chadema kata ya Ifakara, Antony Kamonalelo alisema viongozi hao walikaa na wanachama hao na kuwataka wapunguze munkari ili kumruhusu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilombero, Salum Ngozi na Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga kuhudhuria mazishi.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba wanachama hao waliukubalia uongozi huo kumruhusu Susan peke yake kuhudhuria mazishi hayo.


Juzi, wanachama hao walimtimua msibani Ngozi kiasi cha kuwalazimu polisi waliokuwa eneo hilo kuingilia kati kwa kumchukua mwenyekiti huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Wilaya.

Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Ngozi kutimuliwa katika msiba huo. Mara ya kwanza ilikuwa siku moja iliyotangulia ambayo ilimlazimu Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Francis Miti kuingilia kati.

Ngozi amekuwa akidai kwamba anafanyiwa fujo na kikundi cha watu aliowaita wahuni na kwamba amefungua kesi ya kufanyiwa vurugu katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero na kwamba baada ya kumalizika kwa mazishi atasimamia suala hilo ili haki itendeke.

Chanzo. Mwananchi
 
Halafu kamwambia Pasco eti kapangiwa kiti cha nyuma, zuga yake hata kwa mtoto haiingii akilini, Katibu Mkuu wa wafiwa upangiwe kiti cha nyuma? Basi kuna mijitu humu itatetea. Ikulu kakacha kwenda, hiyo huiita inferiority complex.
 
Huwezi kukaa pamoja na jambazi, heko Dr. kwa kukataa katakata kukaa na mwizi wa kura ambaye ati anajivunia ushindi wa wizi.
 
Slaa ni visasi, chuki na fitna; siyo mstaarabu hata kidogo (uncivilized and backward behaviour)
 
Kuna watu wanaongea kwa machuuungu kujaribu kuonesha kuwa Kikwete kafanya jambo la maana saaana kwenda msibani. Hivi kuna msiba ambao kikwete haendi? Hebu muacheni jamani, hata na yeye anachoka kukaa magogoni na tausi bila kazi yeyote na ukizingatia tusafari twa nje wenyeji wamemchoka. Bora alivyoenda zake Moro kusafisha macho
 
mkuu, nadhani hapo penye bold ndiopenye majibu sahihi................

lakini naomba nikuulize, ....................... ni kwa nini unadhani dr ndiye kasusa na hudhani hata kidogo kuwa (huenda) jk kaambia watu wake kuwa hataki kumshika mkono huyo mtu???...................... nakuomba ujaribu kuwa neutral kidogo ili tupate habari isiyoegemea upande wowote..................

pole na hekaheka za ifakara mkuu....................... RIP regia.......................

Mkuu umenikuna sana na comments zako kweli wewe ni akili mkichwa kama jina lako linavyojieleza.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom