Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 5,175
- 10,484
Unapopambana na ambaye taswira yake kwako ni adui na ni mwenye nguvu kuliko wewe inakubidi utumie akili ya kusoma mazingira, kutambua umakinifu wake, udhaifu wake na kuutambua wakati muafaka! Na si udhaifu, bali ni ufahamu.
Nyakati tuliyonayo ni nyakati isiyokuwa tambuzi ya kuiheshimu katiba ambayo ni sheria mama. Tuna akili itumike vyema kwa kufikiri. Idris ameshindwa kutumia akili, ameshindwa kusoma mazingira, ameshindwa kuutambua umakinifu wa aliyemfanyia mzaha, ameshindwa kuutambua udhaifu wa aliyemfanyia mzaha na ameshindwa kuutambua wakati muafaka na ameshindwa kutambua aliyenao hawajali sheria.
Unafikiri kwa nini vyama vya siasa vinakwenda hatua kwa hatua kukabiliana naye? Mipango ni muhimu. Ukifika wakati muafaka nao watashambulia.
Inakubidi ufahamu sanaa ya picha/vibonzo na sanaa ya video anayoifanya Idris ukiziweka kwenye mizani ipi inayoeleweka na kusambaa kwa kasi ndani ya jamii yetu ni ambayo anayoifanya Idris. Sanaa ya vibonzo/uchoraji anahitaji mtu awe mfuatiliaji wa mambo na inahitaji utumie akili kuelewa ujumbe. Sanaa ya vibonzo/uchoraji inawagusa wale wafuataliaji na wenye upeo wa kufikiri. Ndiyo maana Utawala haihangaiki nayo sana! Ila ya Idris inasambaa sana tena kwa urahisi.
Huyo dogo watamnyoosha!
Utambue wakati! Utambue mazingira uliyoko nayo! Vita ni akili.