Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,778
Msanii wa vichekesho Idris Sultan amefunguka kwa kudai kuwa uhusika aliouvaa ndani ya filamu ya ‘Kiumeni’ ya Ernest Napoleon ni vitu ambavyo viliwahi kumtokea katika maisha yake.
Filamu hiyo ambayo imewakutanisha mastaa mbalimbali wa filamu itaonyeshwa kwa mara ya kwanza Jumatano hii Century Cinemax, Mlimani City jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari Jumatano hii akiwa katika ukumbi wa Century Cinemax, Mlimani City muda mchache baada ya waandishi kuonyeshwa filamu hiyo, Idris alidai tukio la kuachwa na mwanamke ndani ya filamu hiyo ni moja kati ya matukio ambayo yametokea kwenye maisha yake.
“Kwenye hii filamu kuna part ambayo inanihusu, nadhani ni ile part ambayo nilikuja nikafuatwa nikaambiwa mwanamke wako ambaye ulikuwa naye anatoka na mtu mwingine, unashanga tu unaambiwa yule mwanamke wako anamtambulisha mwanaume kwao, hiyo imeshanitokea mimi kwenye maisha yangu,”
Katika filamu hiyo pia Idris ameigiza kama mfanyabishara wa dawa za kulevya.