Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Hii ni mada nimetaka kuileta kwa muda mrefu sana ila naona kama ni muda muafaka kufanya hivyo. Kwa muda mrefu kumekuwa na dhana kuwa mtu ukihojiwa na BBC au DW Idhaa za Kiswahili basi dunia nzima imekusikia. Naomba leo nitoe mwanga kidogo kuhusu suala hili.
Kuna vituo mbalimbali vya kimataifa ambavyo vimeanzisha idhaa za Kiswahili, mfano kituo cha Ujerumani cha DW, cha Uingereza cha BBC na cha Marekani cha Voice of America (VOA). Vituo hivi vimetoa ajira kwa Watanzania na vimekuwa nafasi nzuri ya Watanzania kadhaa kuongeza ujuzi na maarifa katika nyanja ya Uandishi wa Habari.
Mada yangu imejikita katika idadi na aina ya wasikilizaji wa Idhaa hizi na impact yake katika majadiliano mbalimbali ya kisiasa, kijamii au kiuchumi. Tofauti na wengi wanavyodhani, vituo hivyo kutokana na lugha wanazotumia katika idhaa hizo, hawana idadi ya maana ya wasikilizaji au watazamaji kwa raia wa nchi hizo husika. Kwa hiyo mahojiano, habari au taarifa zozote nzuri au mbaya zinazoihusu Tanzania zinazotangazwa na vituo hivyo tuziweke katika mizania hiyo itatusaidia sana.
Nikitoa mfano wa Voice of America. Kituo hicho kilianzishwa mahususi kwa ajili ya kupromote image ya Marekani kimataifa. Na kama nakumbuka vizuri, sheria iliyotumika kuanzishwa kwake inasema wazi kuwa kituo hicho hakitafanya matangazo yake ndani ya Marekani (nadhani kuepuka wanasiasa wa Marekani kukitumia kushambuliana wenyewe kwa wenyewe). Kwa maana hiyo basi, Mtanzania anapoenda kufanya mahojiano Voice of America idhaa ya Kiswahili au hata ya Kiingereza, kumbuka wasikilizaji na watazamaji wake wengi wao SIYO Wamarekani.