Nelson Jacob Kagame
JF-Expert Member
- Dec 26, 2022
- 9,473
- 12,883
- Thread starter
- #921
Sasa mzee wangu....wewe ukifadhiliwa....sio lazima na mimi nifadhiliwe.......mm nina uwezo wa kujikimu katika kazi zangu.Jagina,
Akili yake inakataa kukubali kuwa niko kazini napewa tiketi ya ndege, malazi na nalipwa fedha kwa ujuzi nilionao.
Ujuzi niliopata kwa kusoma na kupasi mitihani yangu.
Chuo kikinialika kinanilipa kwa elimu yangu.
Nisingeweza kuzunguka kote huko laiti nikialikwa inabidi nijilipie nauli, malazi nk.
Haya hayakubali kuingia akilini kwake.
Anaona mimi siko kazini na sistahili kunufaika kwa elimu niliyonayo.
Kwa kuwa yeye hajaweza kufikia kiwango hichi basi mimi nisiwe hivi nilivyo.
Siwezi kulipwa kwa kisomo changu.
Nafadhiliwa.
Namwekea picha hapo chini aangalie niko kazini.
Narekodi kipindi cha historia ya David Livingstone kwa ajili ya BBC Bush House, London.
Huu ni mwaka wa 1991.
Kwa kazi hii BBC wanalipa fedha.
Kote niliposafiri nilijilipia mwenyewe.
Hasa katika majukumu yangu ya mwandishi wa habari wa kujitegemea.
Tuendelee na mada kuhusu UBORA ULIOTUKUKA WA MOSSAD NA IDF KATIKA NYANJA ZA UJASUSI