Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Status
Not open for further replies.
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visivyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.

Hii idara ni ya ofisi gani?
 
Mwanahalisi ni WANAFIKI NA WAONGO SANA BORA WAANZISHE CHAMA CHA SIASA TUJUE MOJA TU

Wewe mwenye ukweli uweke hapa basi ili wote tuujue, sio kulaumu tu ooh mwanahalisi waongo, yaani wewe ndo bongolala kabisa, mwanahalisi wamekuwekea namba ya cm ya Rama nenda TCCRA ukahakiki kama si number ya Rama then uje na ukweli unaojua wewe
 
ok na usalama wa taifa nao wameanza siasa?Mungu wangu hii nchi nani? Ametuloga?.kunasiku na wenyewe watatoka adharani kujisafisha,kama wameshindwa kulizuia gazeti tu! Wataweza nini?,kulikuwa na aja gani ya idara kujibisha na taasisi ndogo kama gazeti
 
we expected nothing less,but hii issue kama vile ipo mahakamani,so...........................................
Najiuliza tu mikataba yote mibovu ya nchi hii inapoingiwa wao huwa wanakuwa wapi?Nalazimika kuamini kuwa wameshindwa kazi yao kwani wanashindwa hata kumshauri rais juu ya mwelekeo wa hali ya nchi kwa ujumla or may be its me (us) who cant read between the lines here.
 
Sitegemei kuwaona wakikubali ushiriki wao katika sakata hilo!!.

kama kuna kitu kimewezesha nyoka kutoka pangoni basi ni hii issue ya Dr. Uli. Nia ya uwepo wa idara hii ni safi ila kama mtanzania mpenda nchi yangu, lazima ifike mahala tuwe makini na watu wachache wanaotaka kutia doa sifa na uwepo wa idara hiyo. Itakuwaje kama waliohusika na kumtesa Dr ni watu wa usalama?
 
Kukana kawaida yao... 1. Walikana Zanzibar kujiunga na OIC. 2. Walikana Loliondo kuuzwa. 3. Walikana ufisadi lakini wanavuana magamba. 4. Walikana EPA, MEREMETA, KAGODA, RICHMOND lakini tunajuwa yaliyofuata na sasa wanatangaza kufungana magerezani. Kwa hiyo kukana ni jadi yao
 
Wangekuwa wamenena vyema kama wangeorodhesha 'sifa zao nzuri' ili kuepuka kuchafuliwa jina lao. Tatizo sifa za usalama wa taifa ni nzuri machoni mwao na watawala lakini ni mbaya na za kutisha machoni pa wananchi. Naamini sifa nzuri ya mwizi ni kuiba sana bila kushikwa, sifa nzuri ya mwanafunzi ni kufaulu mitihani yake kwa kiwango cha juu sana; sasa kati ya hao wawili na yuko tayari kutangaza sifa zake? Tafakari!

10% kutoka kwa investors wanaokuja Tanzania!
 
UWT-Usalama Wa Taifa au kwa lugha inayoendana na matendo yao ya kike tuwaite ni Umoja Wa Wanawake Tanzania wasitake kutufanya Watanzania kuwa HATUNA AKILI KAMA WAO! Kwa hili la Dr. Ulimboka wameshaumbuka na kila Mtanzania kwa sasa anajua hasa nini walikifanya na walitumwa na nani!

KAZI YAO CHAFU ya kutaka kumaliza mgogoro wa Madaktari kwa kumwua kiongozi wao imewatumbukia nyongo kwa MUNGU KUKATAA HUU UOVU WANAOWAFANYIA WATANZANIA.

Wao walijua Dr.Ulimboka hataishi kwa hiyo MADHAMBI YAO yasingejulikana. Hata hivyo Mungu si athumani alitaka UWT wajue kuwa huwezi kushindana na Mungu. Kama kweli wanasema hawahusiki basi wakanushe yale yote aliyoyasema Dr.Ulimboka kwa USHAHIDI USIO WEZA KUTILIWA SHAKA!

Najua hawawezi,kwa hiyo wanachotakiwa kama wana chembe ya uungwana mioyoni mwao basi WAOMBE RADHI KWA WATANZANIA NA WAJIPELEKE WENYEWE POLISI! Pambaf zao.
 
USA kila siku President anakuwa briefed na CIA, je na Bongo ni hivyo? Kama ndio, je sehemu kubwa ya utekelezaji wa TISS ni mwongozo wa Rais?
 
Kanusho la TISS limetolewa na Ikulu! Hilo moja. Lakini kubwa idara hii (TISS) na wakubwa serikalini wanatakiwa wakae chini na watumie busara ili kurekebisha mambo. Watu wanishi kwa watu wasiwasi na imani kwa idara hii nyeti imeshuka sana kama sio kutoweka. Idadi ya matukio tata yanayogusa hii idara yanazidi kuongezeka siku hadi siku. Dunia haitakaa kimya milele.

Tanzania inaishi kwa kibakuli na kama tulivyoona kwenye saga ya bendera na meli za Iran hawa watu wa magharibi wanaweza kugeuka nyuzi 360 within seconds. Kagame pamoja na kuwa kipenzi cha nchi za magharibi, sasa hivi yuko kwenye misukusuko toka huko huko magharibi. Tanzania tukiendelea na hizi comedy tusishange kuona watu wanakwenda the Hague.

Badala ya kujitetea kwa maneno matupu kwanini serikali isiunde tume huru? Ni kitu gani kinachowafanya wakatae tume huru kuangalia mkasa wa Dr Ulimboka?

Nakubaliana na wewe mkuu....Hivi siku hizi watu walio kwenye idara wana uwezo kiasi gani wa kufanya kazi ndani ya idara hiyo?

Kila siku kuna jipya Tanzania...wizi wa mali ya umma, utoroshaji wa nyara za serikali, usafirishaji haramu wa binadamu, na hata Iran kutumia bendera ya Tanzania kwenye meli zake si kitu kidogo.

Halafu wanafikiri kwa kutoa matangazo kama haya watu watawaamini kuwa ni wakweli....toka lini?
 
Hii inaonesha ndani ya Tanzania kuna watanzania ambao sio waajiliwa wa TISS lakini wanauwezo mkubwa wa intelligence kuliko wale waliopewa dhamana hiyo na kufanya TISS kuwa usalama wa watawala!!!!!!!!!!!
 
Kama wamefuta hiyo taarifa ya Rama ina maana TISS wamekubali kuhusika na suala la Dr. Ulimboka. Hawawezi zuia waende na kwenye mitandao mingine wakafute
 
They would have sound sensible if they would have deny by evidence this man called Ramadhani Ighondu is not their inside man. Otherwise its just a cat and a tail game.
 
wanasema watazidi kuunga nguvu na kujiimarisha?ili...........................................

Kubenea kawazidi maarifa...sasa hivi tishio la usalama wa Taifa sio mwanahalisi bali ni UWT wenyewe!
 
Hili jambo ni kubwa na limeenea akilini mwa watu, sio rahisi kulifuta kwa kukanusha katika vyombo vya habari hivyo hivyo ambavyo baadhi vinawatuhumu wahusika. Ingekuwa vizuri TISS kwa kushirikiana na wanachi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, wabaini ni nani alihusika kuhatarisha usalama wa huyo Daktari na kuyumbisha nchi kwa kusababisha kila mtu kuwa na mawazo tofauti kuhusiana na tukio hilo.

Aidha, kama wanafahamu kuwa gazeti linawasingizia, waende mahakamani kulishtaki ili kama likishindwa kuleta ushahidi wa kurishisha, lipewe amri ya kukanusha taarifa zilizokwisha tolewa.

Kitendo cha kusema kwamba taarifa hizo ni za kuunga unga matukio, hakiwezi kuondoa tuhuma kwa TISS. Ikumbukwe kuwa taarifa za uchunguzi zinahitaji kuunga matukio ili kupata taarifa kamili, na hata nao wanafanya hivyo katika kazi zao.
 
as simple like that? Hivi TISS washushiwe tuhuma nzito kama hizi ambazo zipo supported na data waishie kukanusha kirahisi namna ile tu wakuache? Wamekanusha specifically kitu gani? Wale sio wafanyakazi wao?
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visivyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.
HEBU TOENI HUU UCHAFU...HII SIO FORUM YA WATOTO WADOGO....elezeni yakwenu ili tukipima na ya kwenye vyombo vya habari tuamini uzushi....
 
Nadhani idara hii ni miongoni mwa Idara za serikali zinazochukiwa sana, haiaminiwi na wala wananchi tulio wengi hatuioni kama ina maana yeyote...ningelikua na ndugu yangu anafanya huko ningemshauri akalime vitunguu Ilula kuliko kuwa humo...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom