mkadiriajimajenzi
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 549
- 613
Wakati idara ya uhamiaji ikiendelea na zoezi la kamatakamata wahamiaji haramu kumekuwepo na baadhi ya watendaji wasio waaminifu katika idara hiyo waliogeuza zoezi hilo kama mradi wa kujipatia chumo,ikumbukwe wahamiaji hawa especially wahindi na wachina ni watu wenye pesa nyingi sana zinazotokana na kuwatumikisha watanzania kwa kuwalipa kiasi kidogo cha mishahara,hivyo baadhi ya watendaji wa uhamiaji wasio na uzalendo hujikuta wanalogeka wakitulizwa na mamiioni wanayohongwa na hawa jamaa na kuamua kuwaficha na hata kuwasaidia kuwapa mbinu za kujificha ili wasikamatwe.