ID zenu nyingine tunazijua

ID zenu nyingine tunazijua

Ila ID za JF....❗🙌🏿❗

Kwenye ishu za meditation.. Wakati huo tunaandika sana.. Kuna huyo mwana ana madini balaa kwenye ishu za meditation 🙌🏿

Basi mambo yalipopamba moto..! Wahitaji wa meditation na mambo ya kiroho wakawa wengi
Mwana akaiona fursa akatengeneza group la kwanza.. Kiingilio 20 000.. Group likajaa.. Akatengeneza la pili..😃 mambo yalikuwa faya sana

Sasa akaanza michezo ya town.. Anaweka bonge la mada lenye part nyingi.. Akifika panaponoga anadai hawezi kuendelea bundle limekata.. Watu idadi isiyojulikana wanatuma tano tano na kumi kumi za bundle..,🤣

Nadhani mnaijua JF fika.. Watu wakaanza kuhoji mengi... Akaanza kuwaleftisha wote wanaohoji.. Mambo yaliishia hapo🙌🏿🤣
Kekundu kekundu 🤣🤣🤣
 
Ila ID za JF..🙌🏿❗

Enzi za mada maalum ya nagari ikafikia mahali tukawa na group la WhatsApp la magari

Sasa yule mwana mmoja alikuwa active Sana JF na kwenye group.. Akasema yeye ni dereva wa IT na coaster za kukodi

Basi muda mwingi akawa ni mtu wa kupost matukio ya safari za usiku.. Hasa kupeleka misiba ama IT

Yani 24/7 yuko barabarani.. Sasa ikabidi watu waanze kuhoji anapumzika saa ngapi? Na anawezaje kupost JF na kwenye group wakati anaendesha?

Kidogo akapunguza ila akaja sasa kutupiga kipigo kitakatifu.. Akatutangazia msiba msiba wa mwanae pekee wa kike aliyekuwa Mombasa na mama wa jambo
Akatupiga fix mtoto kauliwa na huyo mama! Tukatumiwa na picha ya mtoto akiwa hai ..ILA
Picha za msiba hakuna
Picha za jeneza bilabila
Picha za kaburi bilabila🙌🏿🙆🏿‍♂😃
Kumbukeni hapo kwenye group tumeshamchangia sana na JF pia🤣

Alikuwa na watu wake wa kumtetea sana! Mmoja (mdada) alikuja kuomba radhi baadae baada ya jamaa kukaribishwa kwake akapewa pombe kidogo ndio vituko halisi vikajidhihiri😀
Baada ya ishu ya msiba feki wa mtoto kubumbuluka jamaa aliingia mitini na group likawa bye! Bye..!😀
Wenye mandinga yenyu😆
 
Kuna siku nililog out kwa bakht mbaya asa kila nikilog in inasema pasword sio ikabidi nijaribu kutengemeza ingine baada ya kujisajili profile inakuja kwa maandishi mekundu na inasema hadi nithibitishwe toka hivyo nikaachana na mambo za id nyingine uzuri nilikuja kukumbuka msimbo

Sijui mnawezaje kuwa na id nyingi kiasi hicho
 
Ya kulia wachuchu wa JF.
356180be-413a-478b-a5f9-311bc95ea952.jpeg
 
Back
Top Bottom