ID zenu nyingine tunazijua

ID zenu nyingine tunazijua

Wapo wengi tu mfano; ana andika post yake isiyo na ushahidi wowote/porojo za kijiweni unamjibu, anakuja na Id nyingine kutukana? Na akishatukana, anakuja na Id nyingine kujipa like?
Tunawajua ILA tunawapotezea. Ushauri acheni kutukana watu na ID zenu feki!
Watu wenye maarifa hushindana kwa hoja na sio kwa matusi!
 
Kuna siku nitaandika kitabu The book of JF...!🔥
a666375f-b9e2-42bc-8603-43ce7c12e2ca.jpeg
 
Wapo wengi tu mfano; ana andika post yake ya kuunga unga unamjibu, anakuja na Id nyingine kutukana?
Na akishatukana, anakuja na Id nyingine kujipa like?
Tunawajua wengi tu ILA ushauri; acheni kutukana watu na ID zenu feki!
Watu wenye maarifa hushindana kwa hoja na sio kwa matusi!
huwa akifanya hivyo huwa anapata faida gani? mie nikiona una ID mbili mbili una badili badili na kuona CHIZI FRESH
 
Wapo wengi tu mfano; ana andika post yake ya kuunga unga ana kuja ID nyingine kujipa like.
au unamjibu, post yake ya kuunga uka anakuja na Id nyingine kukutukana?
Tunawajua wengi tu ILA tunawapotezea kwa sababu jukwaa lina ruhusu.
ILA ushauri tu; acheni kutukana watu na ID zenu feki!
Yule mwana aliyefiwa na mkewe Kibaha.. Halafu mdogo wake ndio akawa ana report huo msiba na kuomba assist JF kumbe ni scam tulikuwa tunapigwa😂🙌🏿
 
Nimecheka kinoma! 😊
Kuna mwanetu aliomba msaada hapa ishu ya usikivu miaka imepita kidogo, basi na mimi nikaguswa na suala lake, nikamfuata PM, lengo lilikuwa ni kumwezesha aje mjini, akutane na specialist, ambaye pia ni mshikaji wangu na apate hearing aids. Nilipompa hilo wazo, hakulikataa ila akadai yupo bize anamuuguza mke wake, hivyo angekuja baadae, lakini hili la kuja halikuwahi tokea. Akanambia kuhusu situation yake kimaisha, ikabidi niwe nampiga tafu kiume. Sasa akaja badae kuniambia amepata chance aje mjini, na kwamba familia yake anaipeleka Mwanza, hivyo atahitaji nauli, yake na familia yake n.k. Basi nikampa fedha ambayo niliona itamfaa kusafirisha familia, na yeye kuja mjini. 😊
Huo ndio ukawa mwisho wa mimi kuwasiliana nae. Hakupatikana hewani kwa namba zote, na ID yake hajawahi jibu sms mpaka hii leo. 😊
Na kweli tatizo la usikivu alikuwa nalo. Huwa nabaki tuu kucheka nikikumbuka hiki kisa.
Ulikuwa na hela za kuchezea 😂
 
Back
Top Bottom