Ibrahim Traore afuta Tume ya Uchaguzi Burkinafaso

Ibrahim Traore afuta Tume ya Uchaguzi Burkinafaso

Binafsi bado niko upande wa Traore na Sahel Nations brothers hadi pale watakaponi prove wrong baadae. Ukizingatia nchi iko kwenye kipindi cha vuguvugu la mageuzi ya kisiasa, kiuchumi na kisera, si sahihi kufanya chaguzi na mkaishia kuwekewa pandikizi mkarudi nyuma tena.

Demokrasia ya ulaya sio ya AFRIKA. Huku kwetu wanasiasa wanaingia madarakani kutafuta kula na sio kuwaletea wananchi maendeleo. Hivyo ni rahisi sana mtu kushawishika na kuanza kusukuma ajenda za wakubwa badala ya mustakabali wa maisha ya raia wao.

Kinachotuponza Afrika ni kutokuwa na malengo ya kitaifa kiasi kwamba kiongozi haijulikani anapimwa ,afanikio kwa vigezo gani, matokeo yake wanasiasa wanaahidi t shirt kwa wapiga kura wao kama moja ya mafanikio ya ndani ya kipindi cha miaka 5.

Tujifunzeni kwa Rusia, China, North Korea, Iran, Saudi Arabia, kama kweli hiyo demokrasia ina maana kubwa kama tunavyoaminishwa sasa.
Ibrahim Traoré kufuta Tume ya Uchaguzi ya Burkina Faso inaonyesha nia ya kuimarisha mamlaka yake na kupunguza ushawishi wa nje. Hii inaweza kuwa dalili ya kuimarisha udikteta, kuchelewesha uchaguzi, na kuzuia demokrasia, huku akidai kuokoa gharama na kuhakikisha usalama wa taifa
 
Kuna namna democracy ni pure scam
dictatorship ingelikuwa imeshatupa majibu dhidi ya matatizo ya Africa.
Kuna Nchi zaidi 50 ndani ya Africa na zinazo practice democracy ya kweli hazizidi nchi tano zingine zote ni dictatorship lakini hadi leo Africa inajadili matundu ya Vyoo na zile nchi chache zinazo practice democracy zina unafuu kuliko the rest.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Ukizingatia hoja yangu ya kipindi cha vuguvugu ilicho nacho nchi ya Burkina, maendeleo yanayolenga watu na kukubalika kwake kwa jamii ya wengi, huwezi kumfananisha Traore na Mobutu kwenye hoja hii mkuu.

Xi anaongoza China inayopiga hatua kila uchwao, Putin ameitoa Russia chini na sasa inasonga mbele, n.k lakini hawapigiwi kelele kama anavyofanyiwa Traore sasa.

Kama nchi inakuwa na vision na akaingia mtu akaitekeleza vizuri hata kama amekaa miaka 100 madarakani sioni shida ila kama anaenda kinyume na hapo, tun ahaki kumjadili.
Naunga mkono hoja. Hata mama samia na ccm yake wana vision na ndio maana wametoa dira ya maendelo 2050 hivyo wabaki madarakani mpaka 2050
 
dictatorship ingelikuwa imeshatupa majibu dhidi ya matatizo ya Africa.
Kuna Nchi zaidi 50 ndani ya Africa na zinazo practice democracy ya kweli hazizidi nchi tano zingine zote ni dictatorship lakini hadi leo Africa inajadili matundu ya Vyoo na zile nchi chache zinazo practice democracy zina unafuu kuliko the rest.
ni kweli mkuu.


ila mbadala wa pepsi sio lazima uwe coca
 
Yule amepindua, suala la kumkubali/kumkataa watu wa mapinduzi wala hawajali, unajisumbua bure mkuu.
Kwa umri wake haitakuja kutokea atoke madarakani kifala aende wapi kwa umri wake? Huyu ni Museveni anayekuja, muda ni mwalimu wangu mzuri
 
Kwa umri wake haitakuja kutokea atoke madarakani kifala aende wapi kwa umri wake? Huyu ni Museveni anayekuja, muda ni mwalimu wangu mzuri
Poa tu, kama atakua anafanya mazuri kwa watu na akae milele.
 
Mimi nikiwa Rais, napiga marufuku bangi inayoitwa DEMOKRASIA ndani ya nchi.
 
Poa tu, kama atakua anafanya mazuri kwa watu na akae milele.
Mpaka sasa Ibrahim Traore anatawala 60% ya Burkinafaso, wakati 40% ipo mikononi mwa vikundi vya waasi.

Suala la kufanya mema kwa watu halipo, ni uroho wa madaraka tu ndiyo unao msukuma. Na hili ni tatizo kubwa sana kwa Afrika
 
Back
Top Bottom