John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Ibrahim Ajibu kama ilivyokuwa kwa Jonas Mkude na wenzake kadhaa wakiwemo kina Said Ndemla, wakati wanachipukia kwenye Simba B chini ya Kocha Selemani Matola walionekana ni wachezaji wenye vipaji ambao watakuja kuwa na maisha mazuri kiuchezaji uwanjani.
Hilo ilitimia kwa kiasi fulani, wakaonyesha uwezo wao walipopewa nafasi, katika lile kundi lao wapo waliotusua na wapo ambao mwendo wao ulikuwa mdogo mdogo, na wapo ambao walipotelea njiani.
Achana na wengine wote, Ajibu ilionekana ana kipaji kikubwa lakini Simba wanamchukulia poa, akahamia Yanga, huko akaonyesha uwezo mkubwa lakini bahati mbaya akakutana na uchumi mbovu, mwisho maisha yake nje ya uwanja hayakuwa mazuri na Yanga haukufana vizuri.
Kurejea kwake Simba ni kwa kuwa walitaka kuwaumiza Yanga, pia kipaji chake kilioekana kuwa juu tofauti na alivyokuwa awali Simba, hivyo ikaonekana amekomaa na sasa yuko tayari kwa mapambano.
Aliporejea alikutana na Simba ya moto hasa, akashindwa kufurukuta, akawa mtu wa kutokea benchi.
Taarifa kuwa Ajibu ni mvivu na hajitumi, zimekuwa zikisikika kwa muda mrefu japo mwenyewe anakanusha hilo.
Sasa hivi yupo Azam FC, wengi walitegemea kwa kuwa huko hakuna presha kama ilivyokuwa kwa Simba na Yanga, na kwa kuwa usajili wake wa Azam FC ulionekana ni kama anguko lake, niliamini huu ni muda wa yeye kuonyesha dunia ubora wake.
Lakini tangu atue Azam FC bado imekuwa ikionekana hajaonyesha kile ambacho wengi wanaamini anastahili kuonyesha.
Wadau tujadiliane, tatizo la Ajib ni nini? Tabia, Uwezo wake ndiyo umeishia hapo? Timu aliyopo haina ubora? Na kesho ya Ajib ipoje uwanjani?
Picha: Azam FC