Ibrahim Ajibu tatizo ni uwezo umefikia ukomo au Azam FC?

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Ibrahim Ajibu kama ilivyokuwa kwa Jonas Mkude na wenzake kadhaa wakiwemo kina Said Ndemla, wakati wanachipukia kwenye Simba B chini ya Kocha Selemani Matola walionekana ni wachezaji wenye vipaji ambao watakuja kuwa na maisha mazuri kiuchezaji uwanjani.

Hilo ilitimia kwa kiasi fulani, wakaonyesha uwezo wao walipopewa nafasi, katika lile kundi lao wapo waliotusua na wapo ambao mwendo wao ulikuwa mdogo mdogo, na wapo ambao walipotelea njiani.

Achana na wengine wote, Ajibu ilionekana ana kipaji kikubwa lakini Simba wanamchukulia poa, akahamia Yanga, huko akaonyesha uwezo mkubwa lakini bahati mbaya akakutana na uchumi mbovu, mwisho maisha yake nje ya uwanja hayakuwa mazuri na Yanga haukufana vizuri.

Kurejea kwake Simba ni kwa kuwa walitaka kuwaumiza Yanga, pia kipaji chake kilioekana kuwa juu tofauti na alivyokuwa awali Simba, hivyo ikaonekana amekomaa na sasa yuko tayari kwa mapambano.

Aliporejea alikutana na Simba ya moto hasa, akashindwa kufurukuta, akawa mtu wa kutokea benchi.

Taarifa kuwa Ajibu ni mvivu na hajitumi, zimekuwa zikisikika kwa muda mrefu japo mwenyewe anakanusha hilo.

Sasa hivi yupo Azam FC, wengi walitegemea kwa kuwa huko hakuna presha kama ilivyokuwa kwa Simba na Yanga, na kwa kuwa usajili wake wa Azam FC ulionekana ni kama anguko lake, niliamini huu ni muda wa yeye kuonyesha dunia ubora wake.

Lakini tangu atue Azam FC bado imekuwa ikionekana hajaonyesha kile ambacho wengi wanaamini anastahili kuonyesha.

Wadau tujadiliane, tatizo la Ajib ni nini? Tabia, Uwezo wake ndiyo umeishia hapo? Timu aliyopo haina ubora? Na kesho ya Ajib ipoje uwanjani?

Picha: Azam FC

275060318_365875228879690_1391835452795085808_n.jpg
 
Laana ya Yanga bado inamtafuna

Mtu alipendwa akaaminika kwa washabiki hadi alipewa unahodha kabisa wa timu lakin bado akawatosa

Bado Gadiel naye naona tia maji tia maji pale msimbazi
 
zama zake Ajibu ndo zinakwisha kiwango kimepungua sana sio muda mrefu ataanza kucheza katika timu za madaraja ya kati na sio tena timu kubwa tatu za juu nchini
 
Ni nadra sana kwa wachezaji wetu kucheza kwenye kiwango cha juu kwa mida mrefu, hata huyo Ajib pengine kajitahidi sana hadi sasa bado yupo timu kubwa...
 
Ibrahim Ajibu kama ilivyokuwa kwa Jonas Mkude na wenzake kadhaa wakiwemo kina Said Ndemla, wakati wanachipukia kwenye Simba B chini ya Kocha Selemani Matola walionekana ni wachezaji wenye vipaji ambao watakuja kuwa na maisha mazuri kiuchezaji uwanjani.

Hilo ilitimia kwa kiasi fulani, wakaonyesha uwezo wao walipopewa nafasi, katika lile kundi lao wapo waliotusua na wapo ambao mwendo wao ulikuwa mdogo mdogo, na wapo ambao walipotelea njiani.

Achana na wengine wote, Ajibu ilionekana ana kipaji kikubwa lakini Simba wanamchukulia poa, akahamia Yanga, huko akaonyesha uwezo mkubwa lakini bahati mbaya akakutana na uchumi mbovu, mwisho maisha yake nje ya uwanja hayakuwa mazuri na Yanga haukufana vizuri.

Kurejea kwake Simba ni kwa kuwa walitaka kuwaumiza Yanga, pia kipaji chake kilioekana kuwa juu tofauti na alivyokuwa awali Simba, hivyo ikaonekana amekomaa na sasa yuko tayari kwa mapambano.

Aliporejea alikutana na Simba ya moto hasa, akashindwa kufurukuta, akawa mtu wa kutokea benchi.

Taarifa kuwa Ajibu ni mvivu na hajitumi, zimekuwa zikisikika kwa muda mrefu japo mwenyewe anakanusha hilo.

Sasa hivi yupo Azam FC, wengi walitegemea kwa kuwa huko hakuna presha kama ilivyokuwa kwa Simba na Yanga, na kwa kuwa usajili wake wa Azam FC ulionekana ni kama anguko lake, niliamini huu ni muda wa yeye kuonyesha dunia ubora wake.

Lakini tangu atue Azam FC bado imekuwa ikionekana hajaonyesha kile ambacho wengi wanaamini anastahili kuonyesha.

Wadau tujadiliane, tatizo la Ajib ni nini? Tabia, Uwezo wake ndiyo umeishia hapo? Timu aliyopo haina ubora? Na kesho ya Ajib ipoje uwanjani?

Picha: Azam FC

View attachment 2143210
didcipline ndo silaha ya player yoyote
 
ajib ni mchezaji mzuri, tatizo uvivu na hajitumi, akipata kocha mkali wa kumkimbiza kimbiza ajibu ana perform vizuri tuu
 
Tatizo washauri wake hawakuangalia future ya mchezaji! Alipata ofa za nje akazikataa kisa usimba na uyanga. Naamini angeenda kutafuta maisha nje ingemsaidia sana.
 
Unaposema laana unamaanisha uchawi?

Kwa nini yanga mna tabia za kuloga wachezaji wanaohama timu yenu ili waharibikiwe?

Laana ya Yanga bado inamtafuna

Mtu alipendwa akaaminika kwa washabiki hadi alipewa unahodha kabisa wa timu lakin bado akawatosa

Bado Gadiel naye naona tia maji tia maji pale msimbazi
 
Ndio maana ni muhimu kuheshimu mtu kama Erasto Nyoni kwa kucheza muda mrefu kwa kiwango kile kile na kipindi chote kuitwa Taifa Stars, kupata namba mbele ya wageni toka akiwa enzi hizo Vita'lo ya Burundi, Azam hadi Simba
 
Nikiwakumbuka waliokuwa makapteni wa Utopolo kama Ajibu , Tshimbimbi, Lamine sijui kwasasa wanajisikiaje uko walipo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom