Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,920
Nakukumbuka sana mama yangu.
Simzunguzii yule mama ambae alichindwa kujua jukumu lake abaada ya kuzaa na kulea kwa miaka michache kisha akamtelekeza mwanae
Namzungumzia yule mama ambae nasikia watu wakimsema kuwa hawezi kulala mwanae akiwa hajalala
Namzungumzia yule mama ambae watu wanasema mwanae akiwa anaumwa anakosa kabisa amani
Namzungumzia yule mama ambae watu wanasema mwanae akishindwa kwenda shuleni kwasababu ya hali ngumu anakosa amani
Namzungumzia yule mama ambae watu wanamsema mwanae akilia usiku nae anakesha
Mama huyu ambae sifa zake hapo juu nimeweka baadhi ndie ninaemkumbuka na nahisi namkosa sana na namhitaji sasa kuliko wakati mwingine wowote ule.
Mama nimekukumbuka sana na nasikitika sijapata kukuona kabisa kwenye maisha yangu,niliyemuona ni yule ambae hata sifa hata moja hapo hana,niliishia kubebwa kwenye tumbo lake tu na kisha kuletwa duniani ambako nilikuwa mgeni na yeye ambae alikuwa mwenyeji hakunisaidia kuijua dunia hii.
Uchungu pekee alioupata yeye ni ule wa kunizaa tu lakini zaidi ya hapo hakuna.
Naendelea kukutafuta wewe iliestahili kuwa mama yangu ili nami nione sifa kukuita mama,uko wapi?
Natamani nikuone nami nikupe mapenzi ya dhati ambayo natamani kuyatoa kwako.
Nitaendelea kukutafuta milele
Pongezi za dhati kwe nu wamam wote ambao mmetimiza majukumu yenu stahiki kwa viumbe mlivyovileta duniani kwa kutaka na kupanga wakatio havipo
Mbarikiwe nyote.