I lost My Only Brother I have

I lost My Only Brother I have

Jamani nadhani kama nikianza kuwashukuru mojamoja sintaweza kumaliza kwa kutumia thread hii naomba kusema kwa ujumla asanteni sana wana JF wote kwa ujumla ni kweli hii ni familia ni ya marafiki wa tofauti sana na ninathamini sana faraja zenu na michango kwa wale wa Arusha naomba kusema faraja zenu zimenifanya kujiona kuwa ni mtu ninayethaminika kwenye kundi la watu wenye imani,itakadi na tabia tofauti kuacha tofauti zao na kunifariji kwa kipindi chote cha msiba namshukuru Mungu tumemaliza salama na ni ombi langu kwamba tuendelee kuwa na moyo zaidi ya huo kwa ajili ya kujenga Jamii inayopendana, kuthaminiana na inayoheshimika Kitaifa na Kimataifa. Asanteni sana God Bless you All!
 
Pole sana kwa Msiba, tunaamini kaka alikuwa muhimu sana lakini Mungu amempenda zaidi. Tunamuomba mungu awape moyo wa Imani wafiwa wote haswa ktk kipindi hiki kigumu cha Msiba. Sisi ni waja wake na kwake tutarejea.
 
Back
Top Bottom