Nimesoma upesi upesi na nikaamua niisome tena kwa ukimya mzuri nikagundua mawili au matatu yafuatayo;
- Una tatizo la kutojiamini, huamini kama umeoa, huamini kuwa uan familia bado unaamini kwenye ujana
- Una asili ya ubinafsi kwahio inakuapa shida sana ku-share na wengine, mkeo ndio mtu wako wa ku-share naye mambo mengi sijasema mambo yote nimesema mambo mengi.
- una kiburi na kujikweza, hutaki kushindwa, hutaki kuelewa, ndio yako ndio NDIO na hapana yako ndio Hapana, misimamo ya style hii haiwezi kamwe kukupa amani
- Umejiingiza kwenye mahusiano mengine kwa kisingizio cha kutendwa vibaya na mkeo, japo umeshindwa kusema kosa lako at least kwa ujumla wake tu
- Hauko tayari kushaurika, hivyo utapotea zaidi badala ya kufanikiwa.
- Wanawake wengi watakuumiza zaidi na hakuna atakayekupa faraja.
Hao wanawake unaowadanganya nao watakuja kuumia siku moja wakiujua ukweli, kwahio na wewe jiweke kwenye nafasi yao. Kumbuka kuna ujana na kuna utu uzima. Huwezi kuwa mtu mzima kisha ukaishi maisha ya ujana....utapotea.
The way forward; jifunze kujishusha, jifunze kuzungungumza, jifunze communication skills, soma maandiko mbali mbali jinsi ya kupunguza hasira na kiburi. Jichanganye na usitake kujiona wa maaana kuliko wengine, Brother, utaishi kwa amani tele out of that ujue kisukari, cancer, presha na mengineyo yanakusubiri. Pole, njoo inbox