I ain't your mama

I ain't your mama

Teh teh teh life ni ujasiri wa kufanya maamuzi hapo hapo hongera kijana.
Mwanaume unatakiwa unfanye maamuzi magumu haijalishi yanaumiza. Unafanya tuu kwakua wewe ni mwanaume. Watu wako bize kuwaza maisha magumu yeye anaimba mafumbo nafukuzaa. Akashitaki sehem.
 
Bhuahahahahaha dah nimecheka sanaaa. ..mleta mada nadhan una mawazo ya kimwendo kasi
 
We ulkua humpendi tu huyo mwanamke ndo maana...huwezi kumfanyia hivo MTU unae mpenda kwa dhati coz lilikua n Jambo dogo Sana lakuzungumza akajirekebisha maybe if there is something behind your relationship
 
sipendagi wanaume wenye akil kama hizi..wanaoendeshwa na matukio..aiseee huko na tabia za kivulana..ebu kua hiyo akili kabla hujaingia ndoanii!! coz inaonesha wee ni mtupu sana kwenye kupambanua mambo!!
yaan wimbo tu unamkusanyia mwenzio virago!!chaa
 
Habari gani wakuu?

Natumai wote mu wazima. I ain't your mama ndio kichwa cha uzi huu hapa.

Ni hivi, nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mdada mmoja hivi kwa zaidi ya mwaka na mambo yamekua yakienda fresh hamna mbaya lakini hivi majuzi niliamua kukatisha mapenzi hayo kwasababu ya wimbo wa i ain't your mama, kisa ni hivi;

Week tatu zilizopita tuliamua kutoka out na huyo aliyekuwa mpenzi wangu tulienda disco ama club. Watu walicheza sana coz DJ alikuwa vizuri sana kila nyimbo aliyotupia watu kelele weweeeeeeeeeee, ila sisi hatukuwa tunacheza bali tulikua tunakunywa mvinyo tuu na kuangalia watu wanavoamsha kwenye dansi floo coz sisi sio wachezaji wazuri wa muziki ila tunapenda muziki.

Cha kushangaza ni pale DJ alipocheza wimbo wa i ain't your mama huu wimbo nauona unachezwa mara kwa mara kwenye chanel ya Trace urban ila sijui aliyeimba ni nani. Wimbo huu ulipoanza tuu mpenzi wangu aliruka kwenye kiti moja kwa moja akicheza kuelekea kwenye dansi floor huku akiuimba wote sijui ni lini ameukariri.

Niliwaza kidogo kwanini kaenda kucheza huu wimbo na sio mwingine? Nikasema isiwe kesi may be ni mvinyo imeingia kichwani, alicheza akifurahia sana huku akinyoosha vidole na wimbo ukawa unafika ukingoja akarejea kwenye kiti huku akiendelea kuimba wimbo huo huo.

Tuliondoka na kurejea nyumba ila nikiwa na kitu kichwani kama nawaza ila sijui nawaza nini. Kesho yake tuliagana akarudi kwake na mimi nikaendela na mambo yangu.Sasa weekend hii alikuja home akapika tukala mambo yakawa yanaenda fresh. Nikakumbuka natakiwa kumtumia ndugu yangu flani hivi document alikua anaziihitaji tangu asubuhi.

Chaa ajabu nilivomwambia mpenzi wangu huyo akaniletee vocha ya halotei aliguna then akawa anaondokaa kwenda dukani huku akiimba I ain't your mama. Hasira zilinijaa sana nikaamua kumtolea kila kilicho chake na kumwekea mlangoni nikafunga mlango nikatokea uwani. Kwa ufupi penzi lilishia hapo japo nilipata taarifa alilia sana.

Ataenda kuhadithia wenzake.
Una tatizo si bure.....

Ni wimbo mzuri.... Ameupenda.... Umejishtukia tu...
 
sipendagi wanaume wenye akil kama hizi..wanaoendeshwa na matukio..aiseee huko na tabia za kivulana..ebu kua hiyo akili kabla hujaingia ndoanii!! coz inaonesha wee ni mtupu sana kwenye kupambanua mambo!!
yaan wimbo tu unamkusanyia mwenzio virago!!chaa
Helloo
 
Sasa unamuacha bila kumuuliza sababu ya kuimba wimbo mpya,, pengine anaupenda tuu...
 
Let her go..Safi sana, madem wenye dharau ni kufunua na kufunika tu. Juzi tu nimefanya haya maamuzi pia, tena najiona niko sahihi sana,.
 
Hahahaa duh kuna watu mna maamuzi magumu. ila kwa kuwa hujajua wimbo unaimbwa nini ni kwamba msanii (J. Lo) anamuimbia mwanaume kuwa anamfanyia kazi kama kupika na kufua sasa anataka hali ibadilike (ikibidi kila mtu afanye mambo yake) ndo anamwambia kuwa hatafanya tena mambo hayo sabab yee sio mama ake (mama wa mwanaume)
lakini for ur case ungemuuliza mwanamke wako ana maana gan kukuimbia (japo inawezekana alikuwa anajiimbia sabab anaupenda) huo wimbo.. umefanya too harsh.
yes. nymbo ukiipenda inakaa sna mdomon sdhaani kama she meant what she sang..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom