I ain't your mama

lovebitelol

JF-Expert Member
Mar 2, 2014
964
972
Habari gani wakuu?

Natumai wote mu wazima. I ain't your mama ndio kichwa cha uzi huu hapa.

Ni hivi, nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mdada mmoja hivi kwa zaidi ya mwaka na mambo yamekua yakienda fresh hamna mbaya lakini hivi majuzi niliamua kukatisha mapenzi hayo kwasababu ya wimbo wa i ain't your mama, kisa ni hivi;

Week tatu zilizopita tuliamua kutoka out na huyo aliyekuwa mpenzi wangu tulienda disco ama club. Watu walicheza sana coz DJ alikuwa vizuri sana kila nyimbo aliyotupia watu kelele weweeeeeeeeeee, ila sisi hatukuwa tunacheza bali tulikua tunakunywa mvinyo tuu na kuangalia watu wanavoamsha kwenye dansi floo coz sisi sio wachezaji wazuri wa muziki ila tunapenda muziki.

Cha kushangaza ni pale DJ alipocheza wimbo wa i ain't your mama huu wimbo nauona unachezwa mara kwa mara kwenye chanel ya Trace urban ila sijui aliyeimba ni nani. Wimbo huu ulipoanza tuu mpenzi wangu aliruka kwenye kiti moja kwa moja akicheza kuelekea kwenye dansi floor huku akiuimba wote sijui ni lini ameukariri.

Niliwaza kidogo kwanini kaenda kucheza huu wimbo na sio mwingine? Nikasema isiwe kesi may be ni mvinyo imeingia kichwani, alicheza akifurahia sana huku akinyoosha vidole na wimbo ukawa unafika ukingoja akarejea kwenye kiti huku akiendelea kuimba wimbo huo huo.

Tuliondoka na kurejea nyumba ila nikiwa na kitu kichwani kama nawaza ila sijui nawaza nini. Kesho yake tuliagana akarudi kwake na mimi nikaendela na mambo yangu.Sasa weekend hii alikuja home akapika tukala mambo yakawa yanaenda fresh. Nikakumbuka natakiwa kumtumia ndugu yangu flani hivi document alikua anaziihitaji tangu asubuhi.

Chaa ajabu nilivomwambia mpenzi wangu huyo akaniletee vocha ya halotei aliguna then akawa anaondokaa kwenda dukani huku akiimba I ain't your mama. Hasira zilinijaa sana nikaamua kumtolea kila kilicho chake na kumwekea mlangoni nikafunga mlango nikatokea uwani. Kwa ufupi penzi lilishia hapo japo nilipata taarifa alilia sana.

Ataenda kuhadithia wenzake.
 
Mkuu tueleze vizuri bana. Lazima kuna some other underlying reasons za kumuacha ila inaonekana ulikuwa unamtafutia sababu tu. I do not think that is reason enough ya kumuacha mpenzi wako. Pole zake shemeji yetu!!
Mkuu sipatani na mafumbo ya nyimbo. Mwanamke akinifikishia ujumbe kwa nyimbo namtolea nje tuu
 
Wimbo umeimbwa na JLO huo
Mmh wewe kisirani mbona sioni shida hapo
Kama alikukwaza ungekaa naye chini myamalize umekurupuka flani hivi mana hukutaka maelezo yake
Kuna shida saana. Sasa ya nini nikae na mwanamke akati anifanyii vitu nataka. Mbona hela nampa nyingi
 
Haahha ila mkuuu naona kama ulijishtukia tu kutokana na actions zako

Sijaona tatizo man.

Ila angalia usije kuruka mkojo ukakanyaga mavii, maana mkataaa pema pabaya panamwita
Wanawake wengi mkuu. Mimi siendeshwi na majivuno ya wanawake kama nampa heshima na yeye aniheshimu
 
Back
Top Bottom